Miaka Niliposoma Vitabu 1000 na Zaidi

Miaka Niliposoma Vitabu 1000 na Zaidi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,184
Reaction score
44,051
Na. M. M. Mwanakijiji
Kama nilivyodokeza wiki iliyopita wiki ijayo kuanzia Novemba 24 hadi Novemba 29 baadhi yetu tumeamua kuanzisha kampeni ya kusoma na watoto wetu vitabu angalau vitano; vitatu vya masimulizi (fiction) na viwili vya mambo ya uhalisia. Wiki hiyo pia itakuwa ni nafasi kwa baadhi yetu kutumia muda kuunga mkono maktaba zetu kwa kuwapeleka watoto na wadogo zetu. Pia itakuwa wiki ya kuangalia na kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kusaidia shule zilizoko kwenye maeneo yetu kwa kuzipatia vitabu. Hizi ni juhudi za pili baada ya zoezi kama hili kufanyika mwaka 2012. Tunatarajia kufanya tena robo ya kwanza ya mwaka ujao, InShaAllah.

Nilianza kupenda kujisomea mwenyewe mara baada ya kuanza shule ya Msingi huko Tanga. Kila Jumamosi Mama yangu alitupeleka mimi na ndugu zangu kwenye Maktaba ya Mkoa wa Tanga pembezoni mwa bahari ya Hindi kwa ajili ya kujisomea. Kuanzia saa mbili asubuhi hivi hadi kwenye saa sita mchana hivi tulikaa maktaba ambapo tulijisomea, kushiriki michezo mbalimbali ya watoto na kusikiliza masimulizi ya hadithi na vitendawili. Ni hapa ndipo nilipotambua mapenzi ya vitabu. Pamoja na maktaba kila siku tulikuwa tunaletewa magazeti ya Serikali na lile la Chama (Daily News, Mzalendo na Uhuru) na kila Jumamosi tulipata gazeti la Mfanyakazi.

Nilipoenda sekondari huko huko Mkoani Tanga nilibahatika nikiwa kidato cha pili kuwa kinara wa usomaji vitabu baada ya taasisi moja ya Kimarekani kutoa msaada wa kujenga maktaba ndogo pale shuleni na kutupatia zawadi ya vitabu. Hadi naingia kidato cha tatu nilikuwa tayari nimesoma vitabu 1000! Miongoni mwa vitabu nilivyosoma wakati huo ni kama vile vya Oliver Twist Mtunzi Charles Dickens, 20,000 Leagues Under The Sea mtunzi Jules Verne, na vingine vingi.

Kutokana na mapenzi haya ya kujisomea sikuishia kusoma vitabu vya Kiingereza tu. Nilisoma vitabu vya riwaya za Kiswahili vile vile kitu ambacho napendelea kusoma hata hivi sasa. Vitabu vya kina Ben R Mtobwa na shujaa wake Joram Kiango katika Salamu Toka Kuzimu, Tutarudi na Roho Zetu? Na Malaika wa Shetani nilivisoma katika mkao mmoja. Sipendi kuacha viporo. Kina Elvis Musiba na riwaya zake za yule Mpelelezi Willy Gamba katika Kikosi cha Kisasi na Kikomo (nikitaja chache) navyo hazikunipita. Masimulizi ya kina Balisidya na michezo ya Kuigiza ya kina Penina Mlama n.k zote zilipitia katika vidole vyangu! Nisahau vipi kina Rosa Mystika ya Agoro Anduru? Au niseme nini kuhusiana na masimulizi ya Shaaban Robert kama katika Adili na Nduguze au Mashairi yake ambayo mimi ni mwanafunzi mzuri na mpenzi mkubwa? Au Mzimu wa Watu wa Kale hadithi ya kipelelezi na yenye mambo ya kutisha mtunzi akiwa M. S. Abdula utasahau vipi hilo? Na hapa sijaelezea masimulizi ya vitabu vya Kasri ya Mwinyi Fuad Kuli Mtunzi ni Shafi Adam Shafi, Alfu Leila Ulela , Simu ya Kifo Mtunzi akiwa Faraji Katambala, au masimulizi ya kwenye magazeti kama simulizi la Usiku wa Manane; utawasahau vipi kina Mzee Ole na Kibibi Gula!? Hapo sijawagusa kwa undani kina Hammie Rajab na kundi la waandishi wa riwaya za magazetini.

Naweza kujaza orodha bila kujitamba sana ya vitabu vingi vya riwaya nilivyosoma na ambavyo leo vimechangia sana katika uandishi wangu iwe katika utunzi wa riwaya zangu au katika uandishi wa kujenga hoja na kushawishi. Pamoja na kupendelea kusoma riwaya nimekuwa mpenzi sana wa kusoma vitabu vigumu vya Falsafa; niliwasoma kina Plato katika Republic, na Mtakatifu Augustino katika The City of God na Confessions. Na hapa sijagusia kabisa vitabu vya kusoma kama sehemu ya kutafuta elimu ya juu nikiwa Chuo Kikuu.

Ninachotaka kudokeza hapa ni kuwa baadhi ya watu wanaponisoma au kusoma maandishi yangu mbalimbali wanafikiri ni matokeo ya kipaji tu au "najua sana kuandika". Karibu kila wiki makala yangu inapotoka Napata barua pepe kadha wa kadha za watu wakikosoa hoja zangu au kuunga mkono; lakini wengi wa hawa pia wanakiri kufurahia uandishi wangu. NImejijengea marafiki wengi (Tanzania nan je ya Tanzania) kutokana na uandishi huo. Bila ya shaka uandishi pia umenitengenezea maadui. Lakini katika yote haya ukweli ni kuwa mimi name ni zao la Maktaba zetu nchini. Hakuna mjini ambao niliishi ambapo sikuwahi kwenda maktaba; iwe Tanga yenyewe, Dar, Mbeya, Mwanza, Arusha au sehemu nyingine. Mahali popote papya nilipofika baada ya kuzoea mji vitu vya kwanza kutafuta ni Kanisa na Maktaba tena kwa mfuatano huo.

Bahati mbaya sana katika uandishi huu nimekutana na watu wengi ambao kwa sababu moja au nyingine kwao kusoma ni kama adhabu. Anaweza kusoma mistari miwili mitatu au vichwa vya habari; ukimwambia asome kitu chenye hata kurasa tano hatochelewa kukuambia "kwani limekuwa gazeti"? Watu wengine hawapendi kusoma vitu viregu kwa sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni uvivu, kukosa uwezo wa kufuatilia hoja kwa urefu wake na wakati mwingine kutokuwa na uwezo wa kutulia kusoma. Na bila ya shaka zipo sababu nyingine nyingi.

Matokeo yake ni kuwa taifa letu lina watu wengi ambao kwao habari ni ile wanayoona kwenye luninga au kusikia radioni. Kwa watu kama hawa hoja wanaweza kuifuatilia kwenye mikutano ya kisiasa pale wanasiasa wanapokuja na kupiga porojo. Matokeo yake tumejenga taifa la watu wanaotawaliwa kijanja kabisa. Watu wamezoea kulishwa maneno n ahata kama kuna kitu kinahitaji umakini wao hawawezi kukifuatilia kwa kina ili kukielewa hasa kama kitu hicho kimefichwa kwenye maandishi.

Rais mstaafu Mkapa wiki iliyopita amesema ukweli huu kwenye mahafali ya kwanza ya shule ya Mt. Peter Claver nje ya mji wa Dodoma. Akihutubia mahafali hayo mwishoni mwa juma Rais Mkapa alihimiza watu kujenga utamaduni wa kupenda kujisomea. "Tumekosa utamaduni wa kupenda kujisomea, watu ni wavivu, hawataka kusoma. Naomba tupende kusoma kwa faida yetu binafsi na hata Taifa" alinukuliwa kusema. Japo nina tatizo nay eye Mkapa kuzungumzia hili kwa sababu sikumbuki wakati wowote wa uongozi wake wa miaka 10 alionekana kwenda maktaba kuonesha mfano huu wa kujisomea au hata baada ya kutoka sijui ni kwa kiasi gani taasisi yake ya Mkapa imesaidia kuchochea kusoma! Hata Kikwete ambaye ni Rais wa sasa sijaona akionesha mfano huo; na siyo wao tu hata viongozi wa upinzani zaidi ya kuwaita watu kuandamana sijawahi kuona hata mmoja wao akienda maktaba kusoma au kupeleka watoto wake au hata kutoa mchango wa vitabu! Ni rahisi sana kuwatawala watu wasiopenda kusoma; lakini ni hatari zaidi kutawaliwa na watu wasiopenda watu wasome!!

Ndugu zangu; unaweza kufikiria kuwaachia watoto urithi wa nyumba, magari, fedha n ahata jina kubwa. Na unaweza kabisa kuacha watoto wake wasome na kupata elimu ya darasani; wanasoma na kufaulu mitihani na kuhitimu. Lakini kijana au mtu ambaye hashiki vitabu ni wa hatari sana; kwanza anajinyima ujuzi mpya lakini pia anaweza kuonekana nyuma ya wakati. Msomi yeyote ni mtu anayependa vitabu; si kwa ajili ya kufaulu mitihani au kujionesha ila pia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa ubongo wake mar azote uko katika hali ya kutatufa maarifa. Kumbe msomi wa kweli haitimu; anaendelea kujifunza kila anachoweza kujifunza. Ubongo wa mwanadamu una uwezo mkubwa wa kujifunza. Na hili halihitaji hata digrii; hata mtu asiye na digrii anaweza kuendelea kujifunza endapo atapewa nafasi hiyo.

Na hili ni muhimu sana kulizungumzia kidogo. Kuna watu wanafikiria kuwa nahimiza wasomi kujisomea. La hasha, ninachohimizia ni mtu yeyote kujisomea. Mojawapo ya matatizo ya baadhi ya wazee waliostaafu ni kuacha kujisomea. Mojawapo ya bahati nilizopita katika miaka hii karibu ishirini ya kujenga hoja kwenye magazeti na mitandao ni kuwa nimepata kuwa karibu na wazee wengi katika siasa za Tanzania wengine wakiwa watumishi wa umma wa zamani wengine wako sasa na wengi hawa huwa wanafurahia maandishi yangu na mimi nasikia heshima kubwa sana kufahamiana nao kwani natambua wanaoendelea kusoma wanajiweka pia vizuri katika hali ya afya kiakili. Ubongo wa mwanadamu hauchoki; ukiamua kuupa mazoezi ya kujisomea, kufanya mafumbo, kuandika basi unajijengea mazingira mazuri tu ya kuhakikisha kuwa akili yako inaendelea kubakia katika hali nzuri katika uzee.

Kijana anayependa sana kujisomea na kutafuta maarifa anaweza kabisa ndani ya miezi sita tu kujikuta ameongeza hekima yake na kujitofautisha na watu wengine hadi watu wanashangaa hekima ameitoa wapi.

NI kwa sababu hiyo basi nawakaribisha wale wote wanaopenda kusoma vitabu tushirikiane kuanza tena kupandikiza mbegu ya kupenda vitabu kwa watoto, wadogo na wajukuu zetu. Wiki ile ijayo amua kufanya mambo yafuatayo kama mchango wako katika kuchochea kusoma vitabu.

a. Soma vitabu angalau vitano kwa watoto wako; unaweza ukipenda kupiga picha na kuwashikirisha wengine. Utashangaa furaha ya watoto kusoma na wewe!
b. Angalia ni namna gani unaweza kutembelea maktaba iliyo jirani yako. Bahati mbaya wengi hawana maktaba jirani n ahata zilipo wakatimwingine ni ngumu kufikika kwa watu walio mbali hivyo. Ni kwa sababu hiyo nimeandaa kijitabu kidogo ambacho kinaelezea jinsi gani mtu au taasisi au kikundi cha watu kinaweza kuanzisha maktaba yake ndogo ya jumuiya. Kijitabu hiki kinapatikana katika mtandao wa
www.Tafakari.Com na www.jamiiforums.com na mitandao mingine. Katika kijitabu hiki utaweza kujifunza jinsi ya kuanzisha na kuendesha maktaba ndogo ya kijumuiya (community library). Hii pia inaweza kutumiwa na vijana/wanafunzi kuanzisha Klabu za Kujisomea.

c. Angalia ni namna gani unaweza kushiriki kusaidia shule katika eneo lako kupata vitabu au kuboresha maktaba zao.
Ndugu zangu tukianzia hivi unaweza kushangaa ni kwa jinsi gani tunakuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyataka. Hatuwezi kusubiri wazungu, NGOs na wageni kutuanzishia vitu vilivyo ndani ya uwezo wetu. TAyari tumeshakubali wakati fulani kupokea hadi misaada ya kuchimba vyoo; sidhani kama tunaweza kuendelea kujiheshimu kama hata watoto wetu tunataka wasomewe na Televisheni!
Tuwe sehemu ya mwamko huu unaoanza taratibu; tutakapofanya ngwe nyingine mapema mwakani tutaona matunda ya kazi hii. Tusome kwa furaha!

Niandikie kwa mawazo, ukosoaji au ushauri: mwanakijiji@tafakari.com au mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Wazo zuri. Community library inafaa sana hususani kipondi hiki - kama ilivyo kipindi kingine chochote, kuhimiza kusoma hususani watoto. Hatahivyo inawezekana kuanza na idea ya kutembelea vituo vya watoto na kuwasomea.

Camera muhimu, usisahau.

Na ahidi J mosi hii nitaenda kufanya appointment na shule ya jirani primary school. Nipo na vitabu vizuri vya watoto kati ya darasa la 3 hadi 4. Nitaomba nitembelee kuwasomea watoto vitabu mara mbili kwa week. Nitatafuta marafiki pia. Tukiwa watatu au wanne, ke na me inakua vizuri zaidi.

Hebu fikiri baada ya week, mwezi, au mwaka hapo kwenye community yako unaandaa event kuwapongeza watoto waliosoma vitabu vingi na kuvielewa viziri. Kabla ya hapo unaandaa competition watoto waandike mchanganuo wa kitabu chochote walichosoma. Unachagua bora kati ya wote waliowakilisha mchanganuo kwako. Unaanza na watoto wachache, labla wanakuiya uncle, hao hao anzanao. Utaona mabadiliko. Moyo wako utapata amani watoto wanaenda kuwa mshujaa. Utashangaa jamii yako inaanza kukuamini. Wataanza kuku support. Utafanikiwa sana.
 
Jina lako hapa linaakisi kwa haki kabisa mtazamo wako; wewe ni mwelewa! Ni kweli sana. Mojawapo ya shida kubwa watu wengi nawasoma huwa wanalaumu ati "Watanzania hana elimu" au "Watanzania hawajielewi" au "Watanzania wana ujinga" n.k ndio maana ati wanafanya maamuzi yale yale. Wengine wanalalamika kuona shule zinafanya vibaya na wanafunzi wanafeli kwa namna ya ajabu. Ukiwauliza wao wamefanya nini kubadilisha hili kauli zao hazichelewi kuanzas na "Serikali" au "CCM"..

Kuna baadhi ya vitu raia wanapaswa kuvivalia njuga wao wenyewe. Mojawapo ni hili.
 
Napenda nitolee mfano wa watoto wa Dar wa siku hizi wao wakiingia Tanganyika library pale wao wamefata mihadi yao.Lakini library zile zilizotujenga watu wengi ndio maana leo tunajivunia kuwa na upeo wa kuchanganua mambo na kuandika lugha yetu ya kiswahili kwa ufasaha bila kuchanganya herufi.
Mzee Mwanakijiji kwenye kampeni hii tupo pamoja maana tutaokoa kizazi hiki kwenye kupiga porojo na kuwa na stori zisizokuwa na vyanzo.
 
Huenda thread hii muhimu haijapata wachangiaji wengi kwa sababu watu wengi hawapendi tabia ya kujisomea.

Nakumbuka wakati nasoma sekondari, mimi na wanafunzi wenzangu wakati ule tulikuwa ni wanachama wa maktaba ya Tanganyika pale Dar es salaam.

Karibia kila siku ilikuwa ni lazma twende pale kujisomea lakini haikuwahi kutokea hata mara moja tukaazima kitabu pale bali tulikuwa tunajisomea madaftari yetu ya notes za masomo mbali mbali tuliokopi kutoka kwenye ubao wakati mwalimu anafundisha ili tufaulu mitihani.

Wengi tulifaulu mitihani lakini kwa miaka yote minne tuliyokuwa tukihidhulia maktaba hatukuwahi kusoma kitabu chochote cha pale maktaba. Tulitumia maktaba ile kama sehemu tulivu kwa ajili ya kusoma madaftari yetu tuu ya darasani ili tuweze kujibu mitihani.

Nachelea kusema kuwa huenda hata leo hii vijana wanaojaa pale maktaba hawaendi kusoma vitabu bali wanaenda kujisomea madaftari yao ili wafaulu mitihani.

Hivyo mtakaobahatika kuanzisha community libraries msije mkahisi mafanikio kuona lundo la vijana wanaingia kujisomea lakini ukweli ni kwamba huenda wasiguse kitabu hata kimoja.
 
Mkuu kwa hiyo hata ulikuwa ukichoka ulikuwa hauendi kwenye shelves kuchukua yale maencyclopidia maana wakati ule ilikuwa google search yetu.
 
Ni mara chache sana tena nilikuwa nikichagua yale yenye picha tuu.
Sikujisumbua kusoma zaidi ya kuangalia picha.
 
Mimi hadi kesho nikumbuka maktaba ya Tanga huwa najisikia furaha moyoni maana kupenda vitabu kulianzia pale bana. Japo sikuwa nasoma mavitabu makubwa lakini ile nguvu ya kujua kuwa naweza kusoma chochote nadhani ilinipa moyo sana. Nilikuwa sikosi kupitia maduka ya vitabu ya zama hizo... duh..
 
Kuna wakati nilipokuwa mhudhuriaji wa maktaba ya Taifa nilikuwa naona kila jumamosi watu wanaleta watoto zao kuja kujisomea vitabu, sina uhakika kwa sasa kama kuna muendelezo wa tabia hiyo.Maana kwa sasa wazazi wanajidai wapo busy mama kupiga umbea saluni baba kupombeka bar mpaka wanasahau mustakabali wa watoto wao.
 
Na. M. M. Mwanakijiji
Kama nilivyodokeza wiki iliyopita wiki ijayo kuanzia Novemba 24 hadi Novemba 29 baadhi yetu tumeamua kuanzisha kampeni ya kusoma na watoto wetu vitabu angalau vitano; vitatu vya masimulizi (fiction) na viwili vya mambo ya uhalisia. Wiki hiyo pia itakuwa ni nafasi kwa baadhi yetu kutumia muda kuunga mkono maktaba zetu kwa kuwapeleka watoto na wadogo zetu. Pia itakuwa wiki ya kuangalia na kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kusaidia shule zilizoko kwenye maeneo yetu kwa kuzipatia vitabu. Hizi ni juhudi za pili baada ya zoezi kama hili kufanyika mwaka 2012. Tunatarajia kufanya tena robo ya kwanza ya mwaka ujao, InShaAllah.

Nilianza kupenda kujisomea mwenyewe mara baada ya kuanza shule ya Msingi huko Tanga. Kila Jumamosi Mama yangu alitupeleka mimi na ndugu zangu kwenye Maktaba ya Mkoa wa Tanga pembezoni mwa bahari ya Hindi kwa ajili ya kujisomea. Kuanzia saa mbili asubuhi hivi hadi kwenye saa sita mchana hivi tulikaa maktaba ambapo tulijisomea, kushiriki michezo mbalimbali ya watoto na kusikiliza masimulizi ya hadithi na vitendawili. Ni hapa ndipo nilipotambua mapenzi ya vitabu. Pamoja na maktaba kila siku tulikuwa tunaletewa magazeti ya Serikali na lile la Chama (Daily News, Mzalendo na Uhuru) na kila Jumamosi tulipata gazeti la Mfanyakazi.

Nilipoenda sekondari huko huko Mkoani Tanga nilibahatika nikiwa kidato cha pili kuwa kinara wa usomaji vitabu baada ya taasisi moja ya Kimarekani kutoa msaada wa kujenga maktaba ndogo pale shuleni na kutupatia zawadi ya vitabu. Hadi naingia kidato cha tatu nilikuwa tayari nimesoma vitabu 1000! Miongoni mwa vitabu nilivyosoma wakati huo ni kama vile vya Oliver Twist Mtunzi Charles Dickens, 20,000 Leagues Under The Sea mtunzi Jules Verne, na vingine vingi.

Kutokana na mapenzi haya ya kujisomea sikuishia kusoma vitabu vya Kiingereza tu. Nilisoma vitabu vya riwaya za Kiswahili vile vile kitu ambacho napendelea kusoma hata hivi sasa. Vitabu vya kina Ben R Mtobwa na shujaa wake Joram Kiango katika Salamu Toka Kuzimu, Tutarudi na Roho Zetu? Na Malaika wa Shetani nilivisoma katika mkao mmoja. Sipendi kuacha viporo. Kina Elvis Musiba na riwaya zake za yule Mpelelezi Willy Gamba katika Kikosi cha Kisasi na Kikomo (nikitaja chache) navyo hazikunipita. Masimulizi ya kina Balisidya na michezo ya Kuigiza ya kina Penina Mlama n.k zote zilipitia katika vidole vyangu! Nisahau vipi kina Rosa Mystika ya Agoro Anduru? Au niseme nini kuhusiana na masimulizi ya Shaaban Robert kama katika Adili na Nduguze au Mashairi yake ambayo mimi ni mwanafunzi mzuri na mpenzi mkubwa? Au Mzimu wa Watu wa Kale hadithi ya kipelelezi na yenye mambo ya kutisha mtunzi akiwa M. S. Abdula utasahau vipi hilo? Na hapa sijaelezea masimulizi ya vitabu vya Kasri ya Mwinyi Fuad Kuli Mtunzi ni Shafi Adam Shafi, Alfu Leila Ulela , Simu ya Kifo Mtunzi akiwa Faraji Katambala, au masimulizi ya kwenye magazeti kama simulizi la Usiku wa Manane; utawasahau vipi kina Mzee Ole na Kibibi Gula!? Hapo sijawagusa kwa undani kina Hammie Rajab na kundi la waandishi wa riwaya za magazetini.

Naweza kujaza orodha bila kujitamba sana ya vitabu vingi vya riwaya nilivyosoma na ambavyo leo vimechangia sana katika uandishi wangu iwe katika utunzi wa riwaya zangu au katika uandishi wa kujenga hoja na kushawishi. Pamoja na kupendelea kusoma riwaya nimekuwa mpenzi sana wa kusoma vitabu vigumu vya Falsafa; niliwasoma kina Plato katika Republic, na Mtakatifu Augustino katika The City of God na Confessions. Na hapa sijagusia kabisa vitabu vya kusoma kama sehemu ya kutafuta elimu ya juu nikiwa Chuo Kikuu.

Ninachotaka kudokeza hapa ni kuwa baadhi ya watu wanaponisoma au kusoma maandishi yangu mbalimbali wanafikiri ni matokeo ya kipaji tu au "najua sana kuandika". Karibu kila wiki makala yangu inapotoka Napata barua pepe kadha wa kadha za watu wakikosoa hoja zangu au kuunga mkono; lakini wengi wa hawa pia wanakiri kufurahia uandishi wangu. NImejijengea marafiki wengi (Tanzania nan je ya Tanzania) kutokana na uandishi huo. Bila ya shaka uandishi pia umenitengenezea maadui. Lakini katika yote haya ukweli ni kuwa mimi name ni zao la Maktaba zetu nchini. Hakuna mjini ambao niliishi ambapo sikuwahi kwenda maktaba; iwe Tanga yenyewe, Dar, Mbeya, Mwanza, Arusha au sehemu nyingine. Mahali popote papya nilipofika baada ya kuzoea mji vitu vya kwanza kutafuta ni Kanisa na Maktaba tena kwa mfuatano huo.

Bahati mbaya sana katika uandishi huu nimekutana na watu wengi ambao kwa sababu moja au nyingine kwao kusoma ni kama adhabu. Anaweza kusoma mistari miwili mitatu au vichwa vya habari; ukimwambia asome kitu chenye hata kurasa tano hatochelewa kukuambia "kwani limekuwa gazeti"? Watu wengine hawapendi kusoma vitu viregu kwa sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni uvivu, kukosa uwezo wa kufuatilia hoja kwa urefu wake na wakati mwingine kutokuwa na uwezo wa kutulia kusoma. Na bila ya shaka zipo sababu nyingine nyingi.

Matokeo yake ni kuwa taifa letu lina watu wengi ambao kwao habari ni ile wanayoona kwenye luninga au kusikia radioni. Kwa watu kama hawa hoja wanaweza kuifuatilia kwenye mikutano ya kisiasa pale wanasiasa wanapokuja na kupiga porojo. Matokeo yake tumejenga taifa la watu wanaotawaliwa kijanja kabisa. Watu wamezoea kulishwa maneno n ahata kama kuna kitu kinahitaji umakini wao hawawezi kukifuatilia kwa kina ili kukielewa hasa kama kitu hicho kimefichwa kwenye maandishi.

Rais mstaafu Mkapa wiki iliyopita amesema ukweli huu kwenye mahafali ya kwanza ya shule ya Mt. Peter Claver nje ya mji wa Dodoma. Akihutubia mahafali hayo mwishoni mwa juma Rais Mkapa alihimiza watu kujenga utamaduni wa kupenda kujisomea. "Tumekosa utamaduni wa kupenda kujisomea, watu ni wavivu, hawataka kusoma. Naomba tupende kusoma kwa faida yetu binafsi na hata Taifa" alinukuliwa kusema. Japo nina tatizo nay eye Mkapa kuzungumzia hili kwa sababu sikumbuki wakati wowote wa uongozi wake wa miaka 10 alionekana kwenda maktaba kuonesha mfano huu wa kujisomea au hata baada ya kutoka sijui ni kwa kiasi gani taasisi yake ya Mkapa imesaidia kuchochea kusoma! Hata Kikwete ambaye ni Rais wa sasa sijaona akionesha mfano huo; na siyo wao tu hata viongozi wa upinzani zaidi ya kuwaita watu kuandamana sijawahi kuona hata mmoja wao akienda maktaba kusoma au kupeleka watoto wake au hata kutoa mchango wa vitabu! Ni rahisi sana kuwatawala watu wasiopenda kusoma; lakini ni hatari zaidi kutawaliwa na watu wasiopenda watu wasome!!

Ndugu zangu; unaweza kufikiria kuwaachia watoto urithi wa nyumba, magari, fedha n ahata jina kubwa. Na unaweza kabisa kuacha watoto wake wasome na kupata elimu ya darasani; wanasoma na kufaulu mitihani na kuhitimu. Lakini kijana au mtu ambaye hashiki vitabu ni wa hatari sana; kwanza anajinyima ujuzi mpya lakini pia anaweza kuonekana nyuma ya wakati. Msomi yeyote ni mtu anayependa vitabu; si kwa ajili ya kufaulu mitihani au kujionesha ila pia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa ubongo wake mar azote uko katika hali ya kutatufa maarifa. Kumbe msomi wa kweli haitimu; anaendelea kujifunza kila anachoweza kujifunza. Ubongo wa mwanadamu una uwezo mkubwa wa kujifunza. Na hili halihitaji hata digrii; hata mtu asiye na digrii anaweza kuendelea kujifunza endapo atapewa nafasi hiyo.

Na hili ni muhimu sana kulizungumzia kidogo. Kuna watu wanafikiria kuwa nahimiza wasomi kujisomea. La hasha, ninachohimizia ni mtu yeyote kujisomea. Mojawapo ya matatizo ya baadhi ya wazee waliostaafu ni kuacha kujisomea. Mojawapo ya bahati nilizopita katika miaka hii karibu ishirini ya kujenga hoja kwenye magazeti na mitandao ni kuwa nimepata kuwa karibu na wazee wengi katika siasa za Tanzania wengine wakiwa watumishi wa umma wa zamani wengine wako sasa na wengi hawa huwa wanafurahia maandishi yangu na mimi nasikia heshima kubwa sana kufahamiana nao kwani natambua wanaoendelea kusoma wanajiweka pia vizuri katika hali ya afya kiakili. Ubongo wa mwanadamu hauchoki; ukiamua kuupa mazoezi ya kujisomea, kufanya mafumbo, kuandika basi unajijengea mazingira mazuri tu ya kuhakikisha kuwa akili yako inaendelea kubakia katika hali nzuri katika uzee.

Kijana anayependa sana kujisomea na kutafuta maarifa anaweza kabisa ndani ya miezi sita tu kujikuta ameongeza hekima yake na kujitofautisha na watu wengine hadi watu wanashangaa hekima ameitoa wapi.

NI kwa sababu hiyo basi nawakaribisha wale wote wanaopenda kusoma vitabu tushirikiane kuanza tena kupandikiza mbegu ya kupenda vitabu kwa watoto, wadogo na wajukuu zetu. Wiki ile ijayo amua kufanya mambo yafuatayo kama mchango wako katika kuchochea kusoma vitabu.

a. Soma vitabu angalau vitano kwa watoto wako; unaweza ukipenda kupiga picha na kuwashikirisha wengine. Utashangaa furaha ya watoto kusoma na wewe!
b. Angalia ni namna gani unaweza kutembelea maktaba iliyo jirani yako. Bahati mbaya wengi hawana maktaba jirani n ahata zilipo wakatimwingine ni ngumu kufikika kwa watu walio mbali hivyo. Ni kwa sababu hiyo nimeandaa kijitabu kidogo ambacho kinaelezea jinsi gani mtu au taasisi au kikundi cha watu kinaweza kuanzisha maktaba yake ndogo ya jumuiya. Kijitabu hiki kinapatikana katika mtandao wa
www.Tafakari.Com na www.jamiiforums.com na mitandao mingine. Katika kijitabu hiki utaweza kujifunza jinsi ya kuanzisha na kuendesha maktaba ndogo ya kijumuiya (community library). Hii pia inaweza kutumiwa na vijana/wanafunzi kuanzisha Klabu za Kujisomea.

c. Angalia ni namna gani unaweza kushiriki kusaidia shule katika eneo lako kupata vitabu au kuboresha maktaba zao.
Ndugu zangu tukianzia hivi unaweza kushangaa ni kwa jinsi gani tunakuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyataka. Hatuwezi kusubiri wazungu, NGOs na wageni kutuanzishia vitu vilivyo ndani ya uwezo wetu. TAyari tumeshakubali wakati fulani kupokea hadi misaada ya kuchimba vyoo; sidhani kama tunaweza kuendelea kujiheshimu kama hata watoto wetu tunataka wasomewe na Televisheni!
Tuwe sehemu ya mwamko huu unaoanza taratibu; tutakapofanya ngwe nyingine mapema mwakani tutaona matunda ya kazi hii. Tusome kwa furaha!

Niandikie kwa mawazo, ukosoaji au ushauri: mwanakijiji@tafakari.com au mwanakijiji@jamiiforums.com

Kwani kwa sasa unafanya kazi wapi mbona naona muda mwingi uko kwenye mablog...do you really get time to work?
 
Hiyo quote sijaelewa inahusiana vipi na hii mada. Kama hutojali naomba ufafanuzi tafadhali.

Soma vizuri post #1 uone jinsi huyu anayejiita Mzee Mwanakijiji anavyojisifu kabla hajasifiwa. Hiyo ni dalili na asili ya mtu duni.

Waswahili wana msemo mwingine, kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.

Fikiri.
 
Last edited by a moderator:

Mimi nadhani anaihamasisha jamii ijenge utamaduni wa kujisomea na kusoma vitabu badala ya kutumia mda mwingi kufanya yasiyo na tija. Sidhani kama hukwo ni kujisifu, unless uwe na tatizo na mleta mada lakini mada yenyewe ni nzuri.
 
Last edited by a moderator:
wazo lako zuri na limekuja wakati muafaka wakati tuko wadogo kulikuwa na vitabu vingi vya watoto na vingi vilikuwa vinajenga tabia ya udadisi,pia ukienda maktaba ulikuwa unapata vitabu vingi sana vya watoto ila sasa hivi nasikitika hatuna watunzi wengi wa vitabu vya watoto matokeo watoto wanapoteza muda mwingi kwenye michezo ya computer pamoja na kusoma majrida au vigazeti vya udaku ambavyo kwa kiasi kikubwa vimechangia mmonyoko wa maadili pia sidhani kama maktaba zetu zinapewa fungu kla kutosha kununua vitabu.Lakini tukumbuke kuwa kipindi huicho hata viongozi wetu walikuwa na tabia ya kuandika vitabu kitu ambacho viongozi wetu wengi hawafanyi hivyo,nakumbuka wakati nikiwa mtoto nilivyosoma vitabu vya akina patrick Lumumba,Kwame nkurumah,Naser raisi wa misri na viongozi mbalimbali mashuhuri wa Afrika hali ambayo ilinijengea moyo wa kizalendo na nikikumbuka kitabu cha pepo ya mabwege kilichoandikwa na Mwakyembe ni baadhi ya vitabu ambavyo vilikuwa vinafundisha watoto badala ya kulalamika inabidi tuanze kuonyesha kwa vitendo nini tunatakiwa kufanya vijana wa siku hizi kwa sababu wamerahisishiwa sana mambo hata uwezo wa kufanya uchambuzi wanashindwa ingawa ukizungumzia mambo ya wasanii na ngono ni wachangiaji wazuri
 
Mimi nadhani anaihamasisha jamii ijenge utamaduni wa kujisomea na kusoma vitabu badala ya kutumia mda mwingi kufanya yasiyo na tija. Sidhani kama hukwo ni kujisifu, unless uwe na tatizo na mleta mada lakini mada yenyewe ni nzuri.

Wewe u"nadhani" lakini uhakika zaidi, isome post #1 bila kudhani.
 
[Nisahau vipi kina Rosa Mystika ya Agoro Anduru]? [/QUOTE]

Rosa Mystika ya E. Kezilahabi (Professor)
 
Mimi nadhani anaihamasisha jamii ijenge utamaduni wa kujisomea na kusoma vitabu badala ya kutumia mda mwingi kufanya yasiyo na tija. Sidhani kama hukwo ni kujisifu, unless uwe na tatizo na mleta mada lakini mada yenyewe ni nzuri.

Alivyo mshari huyu hachelewi kuja na sera zake za udini hapa
 
Back
Top Bottom