Miaka 97 ya Mzee Mwinyi na amani ya moyoni pasipo nongwa na visasi

Hivi mama Sitti yupo?

Ule msemo wa Ikulu ni pango la walanguzi lilianza kipindi kipi?

Sio vema kuanza kutafuta mabaya ila pia sio vema kuamua kuwa na Selective amnesia na kujifanya kusahau kwamba hili shamba la bibi na kichwa cha mwendawazimu kipindi chake lilibadilika na kuwa shamba la babu na kichwa cha mwerevu
 
Aliachiwa nchi maskini sana na Nyerere. Tulikuwa tumetoka vitani mwaka 1978 madhara yake yakiwa dhahiri kwa kila sekta.

Ndio miaka ya mwanzoni ile, tofauti na hawa kina Samia na hayati JPM waliokuta kuna wasomi wa kila aina.

Aliuza kila kitu kitu. Mke wake alikuwa dalali. Nyerere alisikitika sana.

Kuna vitu vya msingi lazima viwe ndani ya serikali kama miundombinu, mashirika ya umeme, maji, mafuta, nyumba nafuu nk.
 
Happy birthday, Mzee Mwinyi! Article nzuri ila umeharibu pale ulipotaka kuonyesha kuwa viongozi Waislamu ni wazuri kuliko Wakristo.

Maisha ni zawaidi kutoka kwa Mungu. Yeye ndiye mwenye kuyatoa. Amemzawadia Mzee Mwinyi maisha marefu. Bwana ashukuriwe kwa hilo.
 
Alijitahidi chini ya Nyerere. Alipochukua nchi kila kitu alisikiliza Mabeberu, IMF, World Bank.

Aliuza kila kitu, kuviweka vyote sekta binafsi. Walipewa kama bure sekta zote muhimu Mafisadi wote. Matajiri wa sasa. Madhara yake tunapambana nayo hadi leo.

Mrema alipambana akamshinda kwenye uchaguzi. Nyerere alimuunga mkono Mrema kugombea, kui -challenge CCM.

Sababu kubwa ni uhuni kama huu unaondeleo. Unahitaji watu kama JPM, Mrema, Nyerere watu kama hao kuutokomeza.
Uzuri Mungu hapangiwi,godfather wenu alishamnyakua na kutupa aliyepo.
 
Aliuza kila kitu kitu. Mke wake alikuwa dalali. Nyerere alisikitika sana.

Kuna vitu vya msingi lazima viwe ndani ya serikali kama miundombinu, mashirika ya umeme, maji, mafuta, nyumba nafuu nk.
Hakuna ushahidi wa kuuza kila kitu ni habari zile zile za kizushi za watanzania. Wakasema mke wake na hayati Hassan Diria walikuwa wauza madawa ya kulevya. Sio habari za kweli.

Ni kama Samia wanavyomhusisha na biashara za maeneo ya mbugani, ni habari za kimbeya zisizo na ukweli.
 
Alijitahidi chini ya Nyerere. Alipochukua nchi kila kitu alisikiliza Mabeberu, IMF, World Bank.

Aliuza kila kitu, kuviweka vyote sekta binafsi. Walipewa kama bure sekta zote muhimu Mafisadi wote. Matajiri wa sasa. Madhara yake tunapambana nayo hadi leo.

Mrema alipambana akamshinda kwenye uchaguzi. Nyerere alimuunga mkono Mrema kugombea, kui -challenge CCM.

Sababu kubwa ni uhuni kama huu unaondeleo. Unahitaji watu kama JPM, Mrema, Nyerere watu kama hao kuutokomeza.
Kama hutojali unaweza kutufafanulia para ya tatu?
" Mrema alipambana.............kui- challenge CCM"
 
Nikiri kwamba sijaisoma makala yote ! Lakini Ali Hassan Mwinyi ndio anakula capacity charges za IPTL ! Hana usafi wowote ule babu yule!!

Ni kiri kwamba sijaisoma makala yote ! Lakini Ali Hassan Mwinyi ndio anakula capacity charges za IPTL ! Hana usafi wowote ule babu yule!!
Dadavua kdg mkuu. How? Maana hata mimi najua ni msafi kama amekula sawa lkn sio kiviiiiile kiasi cha kuwaumiza raia. Au huenda mifumo ya nawasiliana kipindi chake ilikuwa tofauti na Sasa ndio maana mbanga zake nyingi hazikuvunja.

So hebu njoo na udadavuo wenye takwimu nasi tujionee ukweli ulipo.
 
Na ni hapa marais wastaafu waislam wanapokuwa ni waalimu wa uungwana unaoambatana na maisha marefu
Kauli yako sio sahihi.

Kumbuka kiongozi mbora wa waislamu alikuwa mtume muhammad sala na salamu ziwe kwake.

Mtume alikufa na miaka 63 huku akiwa ni mtu muungwana zaidi kuliko mzee mwinyi.

Kuishi maisha marefu hakuambatani na uislamu na wala hakuambatani na uungwana.

Unaweza kuwa mtu mshenzi na ukaishi maisha marefu,naomba usihusianishe baina ya maisha marefu na uislamu au baina ya maisha marefu na uungwana,havina uhusiano.

BTW nayaheshimu maoni yako mkuu.
 
Back
Top Bottom