Miaka 97 ya Mzee Mwinyi na amani ya moyoni pasipo nongwa na visasi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Rais Mstaafu wa awamu ya pili leo anatimiza miaka 97, ni mingi kwa kuiandika na kuihisi kichwani ukifanya tafakari ya kina. Ni miongo tisa na miaka saba. Amekula magunia kwa magunia ya chumvi. Ni umri mkubwa sana kuendelea kuwepo hai, akiwaona wajukuu na watoto zao. Mzee Mwinyi kwa sisi tuliokuwepo duniani wakati anaingia na kuondoka ikulu ni heshima na baraka kumuona akiwa hai miaka 27 baada ya kuondoka Ikulu.

Wengi watajiuliza ameweza vipi kuishi miaka mingi namna hii. Wapo watakaosema hana makuu kwa maana ya kutoweka visasi moyoni, wapo watakaosema hanywi pombe akiwa ni muumini mzuri wa dini ya kiislam. Na wapo watakaokwenda mbali zaidi kwa kusema amekuwa akijitunza na siku zote akishiriki matembezi ya hiari na yeye mwenyewe kupenda kutembea. Na anayependa kutembea mazoezi ya asubuhi au kukimbia taratibu (jogging) anakwepa maradhi mengi yakiwepo yale ya moyo yenye kuua haraka na pasipo kutarajiwa.

Mzee Mwinyi ameendelea kuwepo wakati wazee wenzake karibu wote wa miaka ile ya awamu ya kwanza na ya pili wakiwa tayari wameshazikwa. Siku ya msiba wa hayati John Magufuli akasoma pasipo miwani!, na akatembea kwenda na kurudi kwenye kiti chake pasipo msaada wa kushikiliwa na mtu yoyote.

Ni kweli wote tunapita juu ya uso wa dunia, lakini kupita kwa baadhi yetu ni kule kwenye baraka. Unaweza kujiuliza inakuwaje Mzee huyu anazidi kusherehekea siku za kuzaliwa kila mwaka wakati wanasiasa vijana tu wakiaga dunia. Vijana waliozaliwa akiwa tayari ni mwanasiasa wanakufa na kumuacha yeye akiendelea kuishi kwa upole bila ya makuu pale kwake mbele kidogo ya Msasani kwa Mwalimu Nyerere.

Hakuwa na makuu, hakutunza hasira wala visasi. Hakutaka kuibadili dunia (To change the world), hakuamini kuwa kila tatizo anaweza yeye kama yeye akalitatua na hivyo kuumiza walio wengi katika mchakato wa utatuzi wa hilo tatizo. Hata baada ya kukejeliwa na Mwalimu Nyerere pale Kilimanjaro Hotel Simba Grill mwezi March mwaka 1995 aliendelea kuwa mkimya mpaka ilipofika siku akaamua kujibu mapigo.

Na baada ya hapo hakutaka kujikweza au kupandisha mabega, ni kama alisamehe na kuendelea kuwa huru moyoni. Hiyo ni sifa anayotakiwa kuwa nayo kiongozi mkuu wa Taifa. Uwezo wa kunyenyekea kwa kuyaona ni madogo tu baadhi ya mambo yanakukwaza na kukukera ukiwa ofisini. Ni mtihani mgumu sana kwa viongozi wenye madaraka makubwa kwa mujibu wa katiba yetu kuweza kujishusha huku wakiwa na vyombo vyote wanavyoweza kuvitumia katika kumuangamiza mtu anayewakera.

Miaka 27 ya kuishi kama mstaafu ni mingi, wengi wakijitahidi sana wataishi miaka mitano au kumi na kuaga dunia. Amewaona wasaidizi wake watatu wakiingia ikulu na kuondoka akiendelea kula raha pale nyumbani kwake. Huyu ni mwanasiasa ambaye maisha yake ni zaidi ya kitabu alichokizindua mwaka jana. Kwamba ukiwa hai huhitaji kujijazia makorokoro mengi kichwani kwako, yataishia kukuumiza na kukumaliza siku usiyoitarajia.

Pia ni somo la ucha Mungu. Kwamba ukimtegemea Mungu siku zote hataweza kukuacha ukatetereka na kuteseka kiafya. Miaka 97 ni zaidi ya ile miaka 70 ya kwenye Biblia kwa miaka 27. Siku zote jione wa kawaida na jione hufai kitu ukiwa umepiga magoti kanisani au msikitini. Ukiwa mdogo utajifunza kujiona sehemu ya wakosaji hata kama bajeti yako ya ulinzi ni mabilioni ya shilingi kwa siku, hata kama unalindwa na mitambo imara na wanajeshi wanaotumia zana za kisasa.

Na ni hapa marais wastaafu waislam wanapokuwa ni waalimu wa uungwana unaoambatana na maisha marefu. Hawaoni sababu ya kumuonea mtu au watu. Hawaoni sababu ya kuwafanya watu wakajiona ni kwanini wamekuja duniani kupata mateso yote haya!. Wanaweza kuitwa dhaifu kwa kuwa ni watu walio 'too liberal', wakiachia uhuru mwingi wa kuongea na kuandika, lakini hiyo ni sehemu muhimu wa utoaji wa haki ambao umeandikwa katika vitabu vitakatifu. Hivyo kuona marais wastaafu wa kiislam wanaendelea kuzeeka huku nyuso zao zikiwa na tabasamu la kirafiki ni bahati inayokwenda pamoja na kuwa sababu ya tulio wengi kujifunza mambo fulani ya kimaisha.

Kheri ya kuzaliwa Mzee Ali Hassan Mwinyi.
 
Nikiri kwamba sijaisoma makala yote ! Lakini Ali Hassan Mwinyi ndio anakula capacity charges za IPTL ! Hana usafi wowote ule babu yule!!

Ni kiri kwamba sijaisoma makala yote ! Lakini Ali Hassan Mwinyi ndio anakula capacity charges za IPTL ! Hana usafi wowote ule babu yule!!
 
Mkuu Asante kwa andiko!
LAKINI
Ili uwe hivyo ulivyo andika inategemea malezi na makuzi uliyokulia!
Vijana wengi kama kina JPM walikulia shida na suluba za utotoni wakiwa wakubwa ile Hali haiwaachi salama kabisa kiakili na kisaikolojia na jpm anawakilisha kundi kubwa la watoto na vijana wengi wa kisasa hapa NCHINI makuzi na malezi DUNI full stress KILA kukicha mtu Huyo akipewa madaraka tu utaziona nyufa nyingi Sana!!malezi ya Mwinyi junior na Ridhiwan na baadh yao wanaweza kuyaishi hayo lakini sio kwa WENGINE kama Bashite na wengi Sana!
 
Mkuu Asante kwa andiko!
LAKINI
Ili uwe hivyo ulivyo andika inategemea malezi na makuzi uliyokulia!
Vijana wengi kama kina jpm walikulia shida na suluba za utotoni wakiwa wakubwa ile Hali haiwaachi salama kabisa kiakili na kisaikolojia na jpm anawakilisha kundi kubwa la watoto na vijana wengi wa kisasa hapa NCHINI makuzi na malezi DUNI full stress KILA kukicha mtu Huyo akipewa madaraka tu utaziona nyufa nyingi Sana!!malezi ya Mwinyi junior na ridhiwani na baadh yao wanaweza kuyaishi hayo lakini sio kwa WENGINE kama Bashite na wengi Sana!
Ukiishi ukiwa unafikiria kuumiza wengine mchana kweupe maana yake na wewe uliumizwa sana utotoni. Kule kuumizwa hakuishi kuwa ni tukio la kivitendo tu, bali kunaingia ndani kabisa ya ubongo wako.
 
Ukiishi ukiwa unafikiria kuumiza wengine mchana kweupe maana yake na wewe uliumizwa sana utotoni. Kule kuumizwa hakuishi kuwa ni tukio la kivitendo tu, bali kunaingia ndani kabisa ya ubongo wako.
Nimekuwa MTUMISHI wa umma kwa muda Sasa hasa nikitumika kufundisha vijana wa umri wa miaka 17 Hadi 20 plus!!

Kuna kundi la vijana WENGI hawana uhakika wa milo mitatu WENGINE ni vibarua tu wa ujira mdogo Sana! Ukianza ku dig deeper Maisha yao utaogopa aisee!! Tumeandaa Taifa la sadist Sana kiasi KWAMBA huko mbeleni kupata magaidi kwenye makundi ya kigaidi Duniani ni kugusa tu!!!
 
Nimekuwa MTUMISHI wa umma kwa muda Sasa hasa nikitumika kufundisha vijana wa umri wa miaka 17 Hadi 20 plus !!kuna kundi la vijana WENGI hawana uhakika wa milo mitatu WENGINE ni vibarua tu wa ujira mdogo Sana !ukianza ku dig deeper Maisha yao utaogopa aisee!!Tumeandaa Taifa la sadist Sana kiasi KWAMBA huko mbeleni kupata magaidi kwenye makundi ya kigaidi Duniani ni kugusa tu!!!
Panya Road.
 
Alijitahidi chini ya Nyerere. Alipochukua nchi kila kitu alisikiliza Mabeberu, IMF, World Bank.

Aliuza kila kitu, kuviweka vyote sekta binafsi. Walipewa kama bure sekta zote muhimu Mafisadi wote. Matajiri wa sasa. Madhara yake tunapambana nayo hadi leo.

Mrema alipambana akamshinda kwenye uchaguzi. Nyerere alimuunga mkono Mrema kugombea, kui -challenge CCM.

Sababu kubwa ni uhuni kama huu unaondeleo. Unahitaji watu kama JPM, Mrema, Nyerere watu kama hao kuutokomeza.
 
Alijitahidi chini ya Nyerere. Alipochukua nchi kila kitu alisikiliza Mabeberu, IMF, World Bank.

Aliuza kila kitu, kuviweka vyote sekta binafsi. Walipewa kama bure sekta zote muhimu Mafisadi wote. Matajiri wa sasa. Madhara yake tunapambana nayo hadi leo.
Aliachiwa nchi maskini sana na Nyerere. Tulikuwa tumetoka vitani mwaka 1978 madhara yake yakiwa dhahiri kwa kila sekta.

Ndio miaka ya mwanzoni ile, tofauti na hawa kina Samia na hayati JPM waliokuta kuna wasomi wa kila aina.
 
Back
Top Bottom