Miaka 63 baba mdogo hajawahi kurudi nyumbani

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,682
3,065
Maisha haya wamejaa mambo mengi sana hasa ya utafutaji.

Je, umeshawahi kupotezana na ndugu yako wa tumbo moja, binamu yako, Baba Mkubwa au Baba Mdogo, Shangazi, Mama au Baba, Bibi au Babu, Mpwa, rafiki yako au hata jirani yako, Baba Mkwe au Mama Mkwe unawasikia sikia tu wapo mahali fulani lakini kutokana na maisha yetu haya kitanzania umeshindwa kwenda kumtafuta huko mikoani alikokimbilia.

Binafsi baba yetu huwa anatuambia anaye Kaka yake mkubwa ambae aliondoka nyumbani toka mwaka 1957 hadi sasa hajawahi kurudi ila ana watoto kama watano nao aliwaacha wakiwa wadogo. Kati yao watatu wapo Uingereza na wenyewe waliondoka mwaka 1983 na hawajai kurudi tunasikia tu story mmoja yupo Kigoma na mmoja tunamsikiaga tu TBC Taifa ila huyo wa Kigoma ndo huwa anatutembelea.

Sababu za kuondoka nyumbani tunaambiwa ni kutafuta maisha ila tulishafanya kila njia kumtangaza kupata imeshindika tumetumia radio na magazeti hatujwahi kumpata. Mtoto wake huyo anaekaa Kigoma alimsikia Baba yake kuwa yupo Singida akaanza pori kwa pori lakini wapi.

Kuna mtu akamwambia yupo Ruvuma akaanza ardhi kwa ardhi lakini wapi.
Kubwa zaidi aliondoka akiwa hajawahi kupiga hata picha ,huwa tunatamani kumuona huyo dingi lakini imeshindikana.

Hapa ina maana Baba Mdogo wetu huyu hajui hata sura ya ndugu zake, hajawahi kuhudhuria msiba wa Baba yake wala Mama yake.

Wengine huwa tunajisemea bado hai muda mwingine tunajisemea tu huyo alishachukuliwa na mbingu.

Je, una ndugu amewahi kuondoka nyumbani na hajawahi kurudi na kwa nini, sababu za kuondoka nyumbani ni nini?

Njia gani umewahi kutumia ili kumpata?

Je, ni kweli kuwa kuna dawa za kuwarudisha watu waliopotea au kuondoka nyumbani?

Unajisikiaje kusikia ndugu yako kukimbia nyumbani

Je, kuwa mlowezi ni laana?

Je, tutumie chanjo kama iliyompata Osama kwa kutafuta vinasaba?
 
Inauma Sana. Hata sisi shangazi yetu alijifungua mwaka 1963! Naskia akawa anatoka kinyesi. Jamii ikamtenga, akaona isiwe kesi. Ndo hii sasa tunaita "fistula!

Tunajiulizaga sijui alipona au alikufa! Aliondoka na mwanaye😭😭
 
Inaonekana kupotea katika familia ya huyo mzee ni kitu cha kawaida aisee..

Babu yangu mzaa baba aliondoka kijijini akamuacha baba mkubwa na mwaka miaka miwili ..Baba angu ndiyo Kwanza mimba ya miezi mnne..alikuja kurudi baba mkubwa ameshamaliza chuo ameanza kazi Baba ndiyo kaja mjini kutafuta maisha.
 
Wazee wetu hawa nao wanazinguaga sometimes. Kaka yangu wa nyumba kubwa alikwaruzana na baba mwaka 1970 akaamua kuondoka na hajawahi kurudi hadi leo

huyo bro ndie tunachangia jina. Kuna wakati na mm huwa nashikwa na roho ya kuondoka home pasipo kujua nielekee wapi

Mara zote nimekuwa nikimueleza mama hii hali, kwa kweli inamshtua na ananiombea sana sana

Haya mambo yanatembea na damu aisee
 
Katika familia kuna siri nyingi sana ambazo unaweza usizijue na ukadhani aliyeondoka ni mjinga na hajielewi. Familia nyingi duniani ni za kijinga na kipuuzi sana, zimejaa chuki, khusda, mauaji ya kichawi, kuharibiana nyota n.k. wengi huondoka na wasirudi tena na haijaanzia leo ni tangu kuja kwa mwanadamu.

Jambo pekee ni kumuamini Mungu pekee na sio hao wazazi, ndugu au rafiki kwani nao hao ni binadamu na wanayo mapungufu yao kibao.

Binafsi naishi Mkoa tofauti na sifikirii si tu kurudi bali hata kupata Mke kutoka eneo hilo maana hilo eneo kwangu ni hatari, kwasasa narudi kwakuwa mmoja wa walionizaa yupo hai na si vinginevyo.

Binadamu ukiwaweka sana kichwani mambo yako hayaendi, utalost, na mbaya zaidi ukisimamia future yao na yako mtalost nyote maana kuna wengine ni masikio ya kufa na umasikini.

Kijana amka na upambane na uache imani kuwa zipo dawa utafanya kumrudisha ndugu aliyepotea home muwe nae, zaidi mutamsema kuwa kala maisha na hakuwajali.

Jitahidini mfanye yenu na yake muachieni Mungu kwani uliyeandika huu uzi hauwezi kujua hao unaoita nduguzo ulionao hapo home walimfanyia jambo gani huyo Mzee.. maybe walitaka kumuua, kumuweka msukule, kumharibia kwa namna yoyote ile, jitahidi uwafahamu binadamu, itakusaidia sana pale watakapokufanyia mambo ya hovyo.

USIMWAMINI HUYO ULIYEKAA NAYE KARIBU YAWEZEKANA ANAKUFICHA UKWELI WA HILI ULILOLIANDIKA HAPA, SIKU UKIJUA UKWELI UTAMCHUKIA NA KUMSIFU SHUJAA ALIEKIMBIA TANGU 1957
 
Back
Top Bottom