Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,495
- 113,592
Wanabodi,
Makala ya Jumapili ya leo.
Juzi, Ijumaa, Tanzania tumeadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania, na kiukweli tumefanikiwa sana katika mambo mengi ya kisisasa, kiuchumi na kijamii, ila pia lazima tukubali, hapa tulipo, sipo mahali tungepaswa tuwe, tulipaswa kuwa mbali zaidi ya hapa tulipo!, hivyo “Kwa Maslahi ya Taifa” ya leo, inatafakari kwa juu juu, tulipaswa kuwa wapi na kujiuliza, jee tunakwama wapi?.
Tulipopata uhuru ile 1961, tulikuwa tunakabiliwa na maadui wakuu watatu wa taifa, hivyo tukatangaza vita dhidi ya adui ujinga, umasikini na maradhi. Leo miaka 61 ya uhuru, sio tuu maadui hao wangalipo, bali tumeongeza maadui wengine wawili, tumeongeza adui rushwa na ufisadi ambao hawakuwepo wakati tunapata uhuru.
Adui Ujinga.
Wakati tunapata uhuru, nchi yetu ilikuwa na majimbo, elimu ilikuwa ni ya kulipia, hivyo ni watoto wa kutoka majimbo yenye mazao ya biashara, yakiongozwa na kahawa, hivyo watu wa Bukoba, Kilimajaro, Arusha na Mbeya, ndio watoto wao walisoma kwasababu wazazi wao waliweza kulipa karo ya shule. Jimbo la Nyanza, lenye mikoa ya kanda ya ziwa, wao walikuwa na Pamba, Tanga wakasomeshwa na Katani. Mikoa isiyokuwa na mazao ya biashara kama Singida, Dodoma, Mikoa ya Kusini na Pwani, wao waliokolewa na kusomeshwa na Waseminari.
Hivyo makabila kama Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa wengi kupata fursa za kujiendeleza kielimu na kuonekana kama makabila haya wana akili sana, kutokana na uwezo wa kulipiwa karo.
Rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kulijua hili, akatangaza elimu bure, kuanzia darasa la kwanza, hadi chuo kikuu, hii ikafungua fursa za elimu kwa Watanzania wote, na tuliendelea kufanya mitihani inayotungwa Cambridge, Uingereza. Hata baada ya kuanza elimu bure, bado waliopasi wengi mitihani hiyo, bado walikuwa ni watoto wa makabila yale yale.
Tukaachana na mitihani ya wazungu, tukaanzisha Baraza letu la mitihani, tukatunga wenyewe mitihani rafiki, lakini bado waliopasi wengi ni kutoka makabila yale yale!. Ili watu wa makabila yote wapate fursa sawa za kujiendeleza, serikali ya Nyerere ikaamua kuweka viwango tofauti tofauti vya ufaulu kwa baadhi ya mikoa, na kwa mikoa mingine viwango vikashushwa mpaka chini ya alama 50% ili kila Mtanzania aweze kuingia sekondari. Hii ikasaidia saidia watoto wa makabila yote kuingia sekondari.
Kwa yale makabila ya hali ya chini sana kama Wahadzabe na Wataturu, hawa hawakujua shule, hawaongee lugha ya Kiswahili na wanaishi maporini, serikali iliwakamata kwa nguvu watoto wa familia hizo, na kuwapeleka kwa nguvu shule za bweni na kusomeshwa chini ya ulinzi.
Japo wote hawakufaulu hata kiwango cha chini kabisa, bado serikali iliwaingiza sekondari kwa nguvu kwenye shule za bweni, mwanzo ilianza na Ilburu, wenzao wakawa wanawaona na kuwatorosha wote, ndipo serikali ikawapeleka Shule ya Sekondari ya Pugu, hapo walisoma mpaka kidato cha 4, japo wote hawakufaulu, lakini angalau walijua kusoma, kuandika na ustaarabu wa kuvaa nguo.
Serikali ikawarudisha kujiunga na jamaa zao, kwa kuwapa na zawadi za nguo nyingi za kuwavisha jamii nzima, wakawaacha kijijini kwao, baada ya mwezi, wakaenda kuwatembelea kukagua maendeleo yao, walishangaa, sio tuu zile nguo walizikuta pale pale walipowaacha, bali hata nguo za wale waliosomeshwa na kustaarabika, nao walizivua pale pale na kuziacha pale pale, na kuvaa mavazi yao ya asili!.
Juhudi za Awamu ya kwanza kupambana na adui ujinga ziliendelea kwa kuanzisha elimu ya watu wazi, kisomo cha ngumbaru, na kuibadili mitaala ya elimu kuwa na elimu ya kujitegemea na kuanzisha vyuo vya ufundi nchi nzima. Elimu ya mkoloni ililenga kupata makarani, baada ya uhuru tukaanzisha elimu ni kazi, elimu ya kujitegemea, ili lengo la kuelimika sio tuu ili kuajiriwa bali kujiajiri.
Kuna kipindi, nchi ya Tanzania ndio ilikuwa nchi kiongozi barani Afrika kwa literacy level ya watu wanaojua kusoma na kuandika. Hiki kiwango kwa sasa kimeshuka, sijui tunakwama wapi?
Kwa sasa karibu kila kata ina shule ya sekondari, kila mkoa kuna vyuo vya ufundi stadi. Tulipopata uhuru, tulikuwa na chuo kikuu kimoja tuu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa jina maarufu UDSM, na fani ya kwanza ni sheria, sasa tuna vyuo vikuu vingi na fani nyingi, tunatoa wahitimu wengi, tuna maprofesa na madaktari wa Ph.D wa kutosha, kutoka vyuo vikuu vya kuheshimika na kueleweka hadi vyuo vikuu vya mtandaoni, ambayo vinatoa Ph.D hata kwa darasa la saba kama Ph.D ya Mhe. Joseph Kasheku Msukuma.
Na majuzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kimemtunuku Rais Samia, shahada ya heshima ya udaktari wa Falsafa, iitwayo Honoria Causa, hivyo Rais Samia sasa ni Dr. Samia Suluhu Hassan, japo kikawaida madakitari wa Honoria Causa, hawapaswi kutumia jina la Dr, lakini kwa Tanzania, jina hilo limetumika kwa Dr. Jakaya Kikwete na Dr. Reginald Mengi, hivyo hakuna ubaya jina hilo likitumiwa na Rais Samia, kuwa sasa atambuliwe rasmi kama Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, na nashauri lile jina la Mama Samia, sasa life, libaki ofisini kwake, nyumani kwenye familia yake na kwa watu wake wa karibu. Nami nijiunge na Watanzania wenzagu kumpongeza Rais Samia kutunukiwa Ph.D ya heshima, hongera sana Rais wetu Samia kutunukiwa udakitari wa falfasa, ni heshima kubwa kwako na kwa taifa kwa ujumla. Swali hawa ma Ph.D tulionao wa kumwaga, jee wanalisaidiaje taifa letu kusonga mbele?. tunakwama wapi?
Naomba kwa leo niishie hapa, wiki ijayo nitaangazia miaka 61 ya uhuru kwenye mapambano dhidi ya adui umasikini, kiukweli kabisa Watanzania wengi bado ni masikini, jee tunakwama wapi?
Nawatakia heri ya Uhuru na Jamhuri.
Paskali