Miaka 60 ya uhuru bado maji shida. Huku ni kukosa maono

Egbeth

Member
Jan 15, 2018
38
39
Najua serikali yetu imefanya mengi sana ,Pia nimshukuru Mungu kuwa na viongozi ambao toka uhuru wamelinda amani ya nchi yetu na kutetea umoja na mshikamano wetu.

Kiukweli, zipo nyanja tumepiga hatua kwakiasi na zipo nyanja ambazo bado sana.

Swala la maji:Hasa kwa mkoa au jiji linalochangia asilimia zaidi ya 50 kwenye uchumi wetu ,ni jambo lenye kuleta maumivi ,mfadhaiko na tafakari ngumu kuwa,
Viongozi hawana maono?
Je, hakuna mipango ya muda mrefu na muda mfupi?
Je, hakuna njia mbadala?

Toka uhuru mpaka leo hii tunaona kabisa jinsi ongezeko la watu hasa mijini linavyoongezeka kwa kasi?
Watu wa sera na mipango mpo wapi?

Miaka 60 ,ya uhuru chanzo cha maji kikuu ninkimoja tuu ,mto ruvu? Hapa sisemi
Ila uzembe na kutowajibika upo sana kwa viongozi wetu. Lazima mkubali kulaumiwa kwa hapa, chama cha mapinduzi pamoja na serikali yake ni aibu kukaa madarakani muda wote huo nakushindwa kumaliza tatizo la maji hasa kwa mji wa Dar es salaam, kwa sababu inawezekana.

USHAURI.

UJENGWE MTAMBO WA MAJI MKUBWA BWAWA LA NYERERE

Najua itakuwa nje ya mpango ila nadhani ,kama tutaweza zalisha megawati 2000,basi hapo hapo ujengwe mtambo wa maji wa zaidi ya ujazo wa lita bilioni 20 kwaajili ya miaka 50 ijayo hii tutaweza sadia kusambaza majia kuanzia Dar es salaam ,pwani na hata lindi na morogoro.

MFUMO WA UVUNAJI WA MAJI YA MVUA
Naamini maji ya mji wote wa dar es salaam yanaweza kuvunwa ba kuhifadhiwa pale tutapo waelimisha wanachi jiji hili .(Bati kwa bati ,nyumba kwa nyumba ,hii itasadia kupata maji toshelevu kwaajili ya matumizi mbali mbali.

KUBADILI MAJI YA BAHARI
Hii natumaini ishajulikana

BWAWA LA MTO WAMI
Serikali iamue kujenga bwawa mto wami kwaajili ya matumizi ya maji kwa mji wa chalinze ambao mpaka kufikia 2060 unaweza kuwa na idadi kubwa ya watu ,Mfumo wa maji huo uunganishwe na mfumo wa dawasa.

N.B
Nashauri kuwe na munganisho wa mifumo wa maji nchi kama ilivyo na umeme ili ikitokea chanzo kimoja kimefeli kingine kisadie ,mfano Bomba la maji linalotoa ziwa victoria lifike mpaka dodoma ,liunganishwe na morogoro, maji ya morogoro pia yaunganishwe na iringa ,na pwani na mpaka dar es salaam ,kazi otakuwa tuu kuwa na sehemu za kuongeza presha ya maji ili ikitokea mfumo mmoja umekwama tunafungulia mwingine .

Naomba kuwasilisha wazo. Ila viongozi muwe na mipango ya mda mrefu .maji ,umeme ,afya na elimu
 
Unategemea nini kama viongozi wako ili wajione kwamba wao wanaongoza ni lazima watembelee 'Maviete'?

Unategemea nini kutoka kwa viongozi ambao kazi yao kubwa ni kutengenezeana vyeo ili wasiachane kwenye ulaji?

Miaka 60 ya uhuru Nchi ina viongozi wengi kuliko maendeleo.
Utitiri wa viongozi ambao kazi zao zinaingiliana kwa kiasi kikubwa, ila ufanisi ni sifuri.
 
Mradi wa mkubwa wa maji ya bahari usambaze maji mikoa kama Dar, pwani, morogoro, lindi, mtwara, Dodoma na singida hapo kutakua na scheme kubwa za umwagiliaji za mazao hasa ya chakula na mbogamboga, pili mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Tanganyika usambaze maji kigoma, Rukwa, katavi namba tatu mradi wa maji mkubwa Ziwa nyasa usambaze maji Ruvuma, njombe, mbeya na iringa, hoja ya nne ni mradi mkubwa wa maji kaskazini yaani taping point iwe bahari upande wa Tanga hapo mradi usambaze maji Tanga, Arusha, kilimanjaro na manyara

Sehemu zote mradi utakapopita kuhimizwe utunzaji wa mazingira na kilimo cha mazao kulingana na kanda husika ili tuachane na kilimo cha kutegemea mvua, maana kama tungekua mavuno yetu yako miezi ambayo ni kuanzia mwezi wa sita hadi wa kumi na moja mnaingiza fedha nyingi kwani uhitaji unakua mkubwa sana sehemu nyingi,
 
images - 2022-10-27T122131.302.jpeg
images.jpg

Shithole country
 
Najua serikali yetu imefanya mengi sana ,Pia nimshukuru Mungu kuwa na viongozi ambao toka uhuru wamelinda amani ya nchi yetu na kutetea umoja na mshikamano wetu.

Kiukweli, zipo nyanja tumepiga hatua kwakiasi na zipo nyanja ambazo bado sana.

Swala la maji:Hasa kwa mkoa au jiji linalochangia asilimia zaidi ya 50 kwenye uchumi wetu ,ni jambo lenye kuleta maumivi ,mfadhaiko na tafakari ngumu kuwa,
Viongozi hawana maono?
Je, hakuna mipango ya muda mrefu na muda mfupi?
Je, hakuna njia mbadala?

Toka uhuru mpaka leo hii tunaona kabisa jinsi ongezeko la watu hasa mijini linavyoongezeka kwa kasi?
Watu wa sera na mipango mpo wapi?

Miaka 60 ,ya uhuru chanzo cha maji kikuu ninkimoja tuu ,mto ruvu? Hapa sisemi
Ila uzembe na kutowajibika upo sana kwa viongozi wetu. Lazima mkubali kulaumiwa kwa hapa, chama cha mapinduzi pamoja na serikali yake ni aibu kukaa madarakani muda wote huo nakushindwa kumaliza tatizo la maji hasa kwa mji wa Dar es salaam, kwa sababu inawezekana.

USHAURI.

UJENGWE MTAMBO WA MAJI MKUBWA BWAWA LA NYERERE

Najua itakuwa nje ya mpango ila nadhani ,kama tutaweza zalisha megawati 2000,basi hapo hapo ujengwe mtambo wa maji wa zaidi ya ujazo wa lita bilioni 20 kwaajili ya miaka 50 ijayo hii tutaweza sadia kusambaza majia kuanzia Dar es salaam ,pwani na hata lindi na morogoro.

MFUMO WA UVUNAJI WA MAJI YA MVUA
Naamini maji ya mji wote wa dar es salaam yanaweza kuvunwa ba kuhifadhiwa pale tutapo waelimisha wanachi jiji hili .(Bati kwa bati ,nyumba kwa nyumba ,hii itasadia kupata maji toshelevu kwaajili ya matumizi mbali mbali.

KUBADILI MAJI YA BAHARI
Hii natumaini ishajulikana

BWAWA LA MTO WAMI
Serikali iamue kujenga bwawa mto wami kwaajili ya matumizi ya maji kwa mji wa chalinze ambao mpaka kufikia 2060 unaweza kuwa na idadi kubwa ya watu ,Mfumo wa maji huo uunganishwe na mfumo wa dawasa.

N.B
Nashauri kuwe na munganisho wa mifumo wa maji nchi kama ilivyo na umeme ili ikitokea chanzo kimoja kimefeli kingine kisadie ,mfano Bomba la maji linalotoa ziwa victoria lifike mpaka dodoma ,liunganishwe na morogoro, maji ya morogoro pia yaunganishwe na iringa ,na pwani na mpaka dar es salaam ,kazi otakuwa tuu kuwa na sehemu za kuongeza presha ya maji ili ikitokea mfumo mmoja umekwama tunafungulia mwingine .

Naomba kuwasilisha wazo. Ila viongozi muwe na mipango ya mda mrefu .maji ,umeme ,afya na elimu
Waziri anazidi kuoa tayari kabweteka kwa sifa, kazi iliyomfanya azidi kuoa kaisahau.
 
Kwenye mada humu Jf kuhusu hoteli za nyota tano nilisema moja ya vigezo vya 5* hotel ni lazima nchi husika iwe na mfumo wa maji safi ya kunywa NCHI NZIMA.

Nikiri pia kwamba kipindi cha JPM tatizo la maji Dar lilipungua sana.
 
Back
Top Bottom