Wapenzi wa Jf. Jana tarehe 20 /10/11 nilikuwa naangalia kipindi cha malumbano ya hoja kinachorushwa na kituo cha ITV . Hoja ilikuwa "Utaratibu wa ukusanyaji kodi nchini, Je unakidhi haja katika kuleta maendeleo nchini? Jibu langu mimi ni kuwa haukidhi kwa sababu mifumo takribani yote ya ukusunyaji kodi imetawaliwa na Viongozi wachache ingawa sio wote wanaopenda rushwa, ambayo baadaye ikawa takrima na pengine siku hizi inaitwa 10% hali hii pengine ndio imepelekea Tanzania yetu kuwa na watu wanaosifika kwa ufisadi, Mikataba mibovu ilinayopelekea Tanzania kuingia gharama za kulipa mabilioni ya fedha kwa kushitakiwa mifano tunaijua mwenye macho haambiwi Tazama na mengineyo mengi mtajazia.
Tunasherehekea Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kauli mbiu ya TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE ( MIAKA 50 YA UHURU) katika kauli mbiu hii nilijiwa na mawazo ambayo pengine ndio yalinisukuma kushea nanyi ambayo kwangu ni "side effect" ya miaka hamsini kisha nikajiona kama niko katika nchi ya kusadikika au naota ndoto za Kimweri. Kisha nikajiuliza je tunafurahi moja kwa moja au inatubidi tufurahi na kusikitika? Nikajua tunachofurahia ni AMANI ambayo kwa sasa naona kama "Tembo kaanza kuitia Maji" .
Nasema Tembo kaanza kuitia maji kwa sababu wengine wanatumia Amani yetu na kuiona Tanzania ni shamba la bibi, watafanya watakavyo wataiba watakavyo na hakuna atakaye sema maana hatua hazichukuliwi kwa kukosekana au ushahidi wa kutosha au hakuna kifungu kinachoweza kumhukumu huyo mtu au ndiyo hiyo mikataba mibovu kiasi kwamba watu imekuwa ni ukitaka kula kweli lazima uliwe, ukisema pengine utaonekana ni mvunjifu wa amani. Kwa hiyo Watanzania wengi wamekuwa kama wanasemea uvunguni hakuna anayewasikia hatua ni za mwendo wa konokono pengine tutafika tuendako miaka mia ijayo; maana hamsini ndio hii tuanshereheke. Nikianza na
TUMETHUBUTU:
Katika miaka hamsini tumethubutu kweli kuua shirika letu la ndege (ATCL) na kuzidi kuinua uchumi wa nchi za wenzetu kwa kutuma vifurushi na kupanda ndege zao wakati Rwanda kwa kipindi cha miaka 17 toka mauaji ya Kimbari wamethubutu kuwa na Rwandair ambayo kwa sasa inazidi kukita mizizi. Tumethubutu; pia kuua Reli ya kati, Tazara ikiwa inajikongoja, viwanda vya nguo kama mutex, mwatex, sunguratex, urafiki, kiwanda cha matairi, general tyre, mashirika ya usagaji National Milling, usafirishaji MV Victoria zinayumbayumba, MV bukoba imezikwa, UDA ndiyo hiyo hatusemi, huko liganga ndio mgogoro yaani hata sijui. Nilikuwa nafikiri biashara lazima izae biashara kama sio kupanua lakini sisi biashara ni kuua uchumi na visingizio kibao. Hivi nauli wanazotoa abria huwa zinakwenda wapi? Maana huwezi ukakuta behewa jipya angalau moja limeongezeka kwenye treni wakati huo huo mishara ya wafanyakazi serikali inalipa sielewi.
TUMEWEZA:
Tumeweza kuifanya nchi kuwa na matatizo ya umeme mpaka tulidiriki kuleta ‘management' kutoka Afrika ya kusini kuongoza shirika la umeme hivi uliwaka maana wazawa walionekana ndio chanzo cha matatizo pengine ni sababu ya watu wenye profession zao kuamua wote kuingia kwenye siasa ambako ndiko wanaona kuna ulaji na kuacha kutumia professional zao kuboresha na kuinua uchumi. Matokeo yake bado tunaendelea kulia na tanesco, bandari, madini ambayo pengine miaka mia ijao tutakuwa tumeachiwa mashimo tu. N.k. Tumeweza kuzipoteza biadhaa ambazo zamani nilikuwa naziona siku hizi sizioni kama mafuta ya Tanbond, sabuni za komoa, kodrai, n.k ambazo kwa kweli zilikuwa na ubora siku hizi tumebaki kushabikia vya wenzetu sanasana ‘made in china' Hivi hawa wenzetu walikuwa na wawekezaji kutoka nje na kama ndio mikataba feki haikuwepo.
Tumeweza kuporomosha kiwango cha elimu hata kufikia wanafunzi kupenda kufaulu bila kujisomea na kufanya kazi ya kuiba mitihani matokeo yake ufahamu hakuna, uelewa mdogo, kiasi kwamba hata wakienda kwenda mashindano kama yale ya Zain challenge wanatoka kappa, sasa hivi kuna mapya "Guinese sport special'" yanahusu mambo ya michezo bado nimeshuhudia Wabongo wakiambulia 'Nil' hivi kumbe ni ushabiki tu ufahamu hakuna hii siyo kuonyesha Watanzania ni mbumbumbu hasha ila maneno mengi vitendo kidogo na sio watu wa kujisomea kuongeza maarifa. Matokeo yake tunapata wataalamu wengi wa mgongo wa chupa ama amefika hapo kwa kununua pepa n.k uchambuzi mdogo kweli tutaepuka kuingizwa' king' kwenye mikataba ambayo ndiyo inabeba maslahi ya nchi?
TUNASONGA MBELE .
Pengine ingekuwa tusonge mbele kwa kujirekebisha mapungufu yetu maana yake tuamke, tuwe na uzalendo na tufanye kazi kwa maana nyingine tuwe na viongozi bora na tusiiachie serikali pekee, kila mmoja awajibike kwa nafasi yake. Tukilalamika bila kuchukua hatua maana yake ndio twasonga mbele na makapi yetu.. Sasa hivi najua tuna mjadala wa katiba ingawa itabidi pia niishukuru katiba yetu pamoja na mapungufu yake lakini imewezesha watu kuachiana madaraka kwa amani na pengine kujivunia amani tuliyonayo mapaka leo maana kwa wenzetu twayaona. Pengine mazuri niyaonayo ni kuingia kwenye mfumo wa Teknolojia ya kisasa ‘digital' miundomibiu ya barabara lakini bado ujenzi usiongitia miundo mbinu! shule nyingi lakini bado hakuna walimu wa kutosha na wenye sifa, Hosipitali nyingi lakini gharama za matibabu hazibebeki, maji sisemi, umeme janga la Taifa, njaa ndio hiyo, bila kuusahau Uwanja wa Taifa tunaojivunia na inabidi tuwe wazalendo kuutunza je ni haya tu ndio tunatumia mabilioni kusherekea miaka hamsini ya uhuru au kuna mengine siyajui!!!!!!
Je wewe yako ni yapi yanayokufurahisha na kukuchukiza na ungependa mabadiliko kwa miaka hamsini ijayo?