Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru imetolewa leo ambayo ni 'Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga mbele'
Je iko relevant na Tanzania ya leo miaka 50 baada ya Uhuru?
Kidumu chama cha mapinduzi na wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Kikwete unadhihaki wapiga kura wako, hebu angalia huyo mzee na kofia yako!!!
![]()
mkuu nadhani tunaoibiwa ni watanganyika zaidi kwani tumeibiwa na nchi yetu nzuri tukabaki na ufisadi wa tanzania!kweli wamethubutu na wameweza kuwanyonya watanzania.
Nikisikia kauli hiyo huwa napata turmoil na hatimeye PUKE!
Hoja yako itakuwa miaka 50 ya MUUNGANO na sio UHURU..Kifupi sikukuu hii ni ya Watanganyika nadhani umefika mwanzo wa kuitambua Tanganyika kwa madai ya Watanganyika..Hizi kamba za kutokuwa na nchi inaitwa Tanganyika, wakati Zanzibar wameitambua yao kuwa ni nchi, nadhani imefika wakati na sisi wananchi wa bara tukatae na kusema Tanganyika ipo na hai...Karibuni ktk kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika na Wazanzibar watatuunga mkono, nasi tutasherehekea nao siku ya MAPINDUZI ikifika miaka 50...Naona kuna upotovu kwenye hili, ninavyotambua na kuamini Tarehe 9 Desemba ni uhuru wa Tanganyika na sio Tanzania kama tuna taka Tanznaia ni tarehe 26/4/2014. Maoni yangu siku hiyo tuwe na bendera ya Tanganyika tu wananchi wabebe bendera hiyo, pili Wazanzibari wasijihusishe sana na siku hiyo HAIWAHUSU zaidi ya kupumzika tu, Kama wabara watakavyopumzika 12/1/2014 wakati wa miaka 50 yao.
Naomba haya yawekwe SAWA vinginevyo naigomea siku hiyo RASMI. Naomba mniunge mkono tusikubali kuburuzwa hivyo.
- Wamethubutu - Kuiba rasilimali za Watanzania Wanyonge
- Wameweza - Kuiba rasilimali za Watanzania wanyonge kwa miaka 50 sasa
- Wanasonga mbele - Kuendelea kuiba rasilimali ya Watanzania wanyonge kwa miaka mingine 50 ijayo
Ni kauli mbiu nzuri kabisa.Tumethubutu kujitawala na tumeweza. Tumeweza kupunguza umasikini kwa hali ya juu sana na hili nalo tumeweza ingawa jitihada bado zinafanyika maana kutokomeza umasikini ni mchakato na mwisho tunasongambele katika kujiletea maendeleo na hili tumeliona chini ya serikali ya Rais Kikwete kwa kuwekeza sana katika elimu mfano Chuo Kikuu Cha Dodoma, na katika kilimo kwani ni hivi karibuni benki ya wakulima inaanzishwa ukiachilia mbali benki ya wanawake ambayo imekwisha anza kazi.
Hakika tunasonga mbele.