Miaka 50: Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele...

Miaka 50: Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele...

ndg wana jf tuwe wakweli, hizi sherehe zinatufumbua macho wengi, na hasa pale tunaposomewa mafanikio, ila upande wa pili ndo nimegundua kama kumbe ndani ya taifa la tz kuna watoto wa wazazi na watoto wa kambo kulingana na keki ya taifa inavyogawanywa, mfano; rukwa ni miongoni mwa mikoa mama ktk kuzalisha nafaka, lakini hadi leo bado barabara ya rami kwao ni ndoto, umeme ndo usiseme, elimu ikochini ni mwisho, afya du! maji machafu ndo kwao na kila indiketa ya umasikini, ingekuwa heri basi nao waangaliwe kama watz wengine kwani wote wanalipa kodi sawa.
 
Ni awamu ya 4 yenye maneno matamu na ya kutoa matumaini makubwa kwa watanzania, maneno haya yanaendana na hali halisi ya maendeleo ya nchi yetu baada ya miaka 50 tangu tupate uhuru?. Wakuu naomba michango ya yaliyoahidiwa na kutekeleza kwa watanzania. Ajira kwa vijana sizioni, maisha bora kwa kila mtanzania siyaoni, uchumi unaporomoka, shilingi inazidi kupoteza thamani, sukari juu, vifaa vya ujenzi juu, bado kuna majengo ya shule yahana madawati, walimu na vitabu.
 
eti wadau ni sahihi kwa Tanzania kusherekea miaka 50 ya uhuru ili hali tuna matatizo lukuki kama wanafunzi wanajiunga na vyuo vikuu kukosa mikopo,mfumuko wa bei ukosefu wa uongozi bora umasikin ulikithiri?
 
usichanganye baida ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika na Tanzania...............Tanzania sasa ndio inatimisha miaka 47 ya muungano
 
Wanajamvini nimejaribu kupita hapa na pale Mnazi mmoja naona watu wameweka maturubai kwa ajili ya kuonyesha sijui nini kilichofanyika katika hiyo miaka hamsini? Najua kabisa kuna hela zitakuwa zinatumika kuandaa vile vitu kuwalipa watu inakuwaje tunasema Serikali yetu haina hela wakati vitu kama hivi vifanywa kwa kupokezana wizara kwa wizara kila mwezi sijiu kila wiki! Hivi hii nchi ikoje jamani? Watu wanamatatizo ya huduma za kijamii Serikali yenyewe imefumba macho haioni.
 
Nina ndugu yangu ambae anafanya ukalimani wa lugha ya kichina Kwa wachina ambao wamekuja rasmi kufundisha halaiki ya watot laki sita wa shule za msingi za dar kwa ajili ya sherehe za miaka 50 ya uhuru. Kwa siku mwanafunzi 1 analipwa 3000, mkalimani 1 analipwa sh. 60,000 Kwa siku. Chakula na maji analeta bakhressa kila siku na analipwa. Usafiri wa kuwaleta na kuwarudisha watoto nk. Hapo sijajua wachina wanalipwa ngapi (wako 20) walimu nao wanalipwa ngapi sijajua. Hizo ni baadhi tu ya gharama na najua ziko nyingi sana. Hivi ni sawa kutumia mamilioni yote hayo kwa ajili ya sherehe ya siku moja kama si masaa kadhaa?
 
Hii nchi ukiishi kwa kuifikiria na kuifuatilia serikali unaweza kufa kwa msongo wa mawazo bure, ni bora hata tusiwe na serikali kama kule Somalia ingawa sisi tunaona wanaserikali lakini ukiwauliza wao watakujibu kuwa hawana serikali
 
badala ya kuleta unafuu kwa wanainchi ndio kwanza wanapandisha gharama za matumizi ya umeme kwa asilimia mia na hamsini
 
“Wanasiasa wabovu hupelekwa Washington na watu wazuri wasiopiga kura”ni maneno ya William Simon aliyewahi kuwa waziri wa fedha wa Marekani. Nimeamua kuiweka hii nukuu kwa sababu inatafsiri hali halisi ya jinsi mambo yalivyo sasa katika nchi yetu, miaka 50 baada ya uhuru. Tanzania ya leo imejaa manung’uniko mengi yanayoelekeza lawama kwa viongozi hasa wanasiasa kwa kutowajibika kwa viwango vinavyokidhi matarajio yetu.Mara nyingi tumekuwa sehemu ya lawama zinazotokana na sisi kutotumia fursa zinazojitokeza kuamua mambo mazito ya taifa. Japokuwa kumekuwa na jitihada za kuwafanya watu washiriki kidemokrasia kwenye shughuli mbalimbali kama vile uchaguzi, bado watu wanakuwa wagumu sana kushiriki na baadaye kuishia kulaumu mfumo au viongozi kwa kutokidhi matarajio yao. Nini hasa tatizo?
  1. Ni matarajio yetu kuwa makubwa zaidi kuliko uwezekano?
  2. Uongozi mbovu unatokana na tabia binafsi au ubovu wa jamii husika? kama viongozi/wanasiasa ni zao la jamii, ubove wao unawezaje kutenganishwa na na jamii inayowazalisha?
  3. Kama tatizo ni mfumo; nini kifanyike?kubadilisha watu kunaweza kuleta mabadiliko ya mfumo?
Tunawezaje sisi tunaodhani kwamba viongozi wetu wanakosea kujiondoa kwenye lawama ya sisi kutowajibika kuwaweka watu stahiki kwenye nafasi za uongozi kama anavyosema William?tujadili kama taifa tuna tatizo gani ili tusije tukaanza miaka 50 ijayo na stock ya matatizo ya miaka 50 iliopita?. Tutawezaje kubadili huu mfumo wa kifikra ili miaka 50 ijayo iwe ni ya kushiriki badala ya kusubiri kishirikishwa?
 
[h=1][/h]Written by amini // 28/11/2011 // Habari // 1 Comment

Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania

Padri Privatus Karugend
TUNAPOSHEREHEKEA miaka 50 ya uhuru wetu ni wakati mzuri wa kuwakumbuka mashujaa waliopigania uhuru wa taifa letu na ni muhimu pia kuwakumbuka wale wote waliochangia maendeleo ya taifa letu mara baada ya uhuru hadi leo hii.
Kumekuwepo na michango mingi ya watu binafsi, mashirika ya dini na mashirika yasiyokuwa kiserikali. Wote hao wamekuwa wakichangia kuijenga Tanzania yetu.
Historia hii ya miaka 50 ya uhuru wetu ni mradi wa pamoja uliotekelezwa na Watanzania wote na utaendelea kutekelezwa na wananchi wote miaka mingine hamsini na kuendelea.
Ingawa uhuru wetu ni mradi wa pamoja ni vema kutambua mchango wa makundi mbalimbali. Katika makala hii na nyingine zitakazofuata nitajadili mchango wa harakati wa mashirika yanayotetea usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru wetu.
Mashirika haya yamefanya mambo mengi ya kutetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa mwanamke kama tutakavyoshuhudia kwenye makala hizi.
Mfano kusaidia kuiweka sahihi historia ya taifa letu. Tumekuwa tukisikia majina ya wanaume bila kutajwa wanawake katika historia ya kupigania uhuru wa taifa letu lakini kwa kazi iliyofanywa na TGNP (Mtandao wa Jinsia Tanzania) wa kutafsiri katika lugha ya Kiswahili utafiti wa Susan Geiger juu ya Wanawake wa TANU.
TGNP wamehakikisha kitabu hiki kinasambazwa na kusomwa na wengi, kumeleta mwanga mpya wa ukweli wa Wanawake kushiriki kikamilifu katika kupigania uhuru wa taifa letu. Huu ni mchango mkubwa.
Inawezekana hata mtandao huo hawautambui mchango huo maana daima tunaelekeza nguvu zetu kwa mambo makubwa ya dunia hii na kusahau maisha ya siku kwa siku yanayotuzunguka. Baada ya uhuru mfumo dume ulishika hatamu, historia ya wanawake waliopigania uhuru ikasahaulika na kufunikwa.
Marehemu Susan Geiger ni msomi mwanaharakati ambaye alifundisha masomo ya Kiafrika na yale ya Jinsia katika Chuo Kikuu cha Minnesota/Twin Cities, huko Marekani kwa muda wa miaka mingi.
Alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa mwalimu wa kujitolea katika miaka ya 1960. Baadaye aliendelea kurudi katika nyakati tofauti katika kipindi chote cha maisha yake.
Kazi yake kubwa ya utafiti ilikuwa juu ya historia ya uchifu wa Wachaga. Utafiti huo ndio uliokuwa chimbuko la kujipatia Shahada ya Udaktari wa Falsafa. Baada ya hapo alifanya utafiti mwingine wa makusanyo ya wanawake wanaharakati wapigania uhuru.
Susan alikuwa mwanaharakati aliyejitolea kwa michango ya hali na mali hadi mwisho wa maisha yake. Alitoa mchango mkubwa kwa wanamtandao wa masuala ya jinsia hapa nchini ili waweze kuendeleza shughuli zao.
Utafiti wake juu ya wanawake wa TANU, uliibua mengi yaliyokuwa yamefunikwa. Mbali na Bibi Titi Mohamed, mwanamke anayetajwa kwa mbali katika harakati za kupigania uhuru wa taifa letu.
Kuna majina ya wanawake wengi waliojulikana kama “Wanawake wa TANU” waliopigana kufa na kupona kulikomboa taifa letu. Kufuatana na ushuhuda wa wanawake wa TANU, ni kwamba chama hiki kilisimikwa na wanawake, kama alivyonukuliwa Bi Mashavu binti Kabonge kutoka Tabora.
“Nikwambie ukweli, wanawake ndio walioleta TANU. Ukweli ni kwamba wanawake ndio waliofanya hivyo. Wanaume wengi waliogopa kufukuzwa kazi.
Waliambiwa na waajiri wao kwamba yeyote atakayejiunga na TANU atafukuzwa mara moja…. Lakini wanawake walikuwa mashabiki wa nguvu wa TANU na wengine waliachika kwa sababu ya shughuli zao za siasa.”
Mashavu binti Kabonge, ni kati ya wanaharakati wanawake wa Dar es Salaam, waliopigana kufa na kupona kuleta uhuru wa taifa letu, lakini hawatajwi wala kukumbukwa.
Hivyo tunaposherehekea miaka hamsini ya uhuru wetu kwa vile TGNP imetusaidia kuyafufua baadhi ya majina ya wapigani uhuru hawa ni bora kuwakumbuka na kuwaenzi.
Pia ni wakati kuendeleza mapambo ya mfumo dume ambao ni hatari kwa mambo mengi hadi kuifuta historia. Ni wazi majina ya wanawake hawa waliopigania uhuru wa taifa letu yamefunikwa na mfumo dume! Hakuna maelezo mengine!
Mbali na Mashavu binti Kabonge, kuna majina mengine mengi ya wanaharakati wanawake wa Dar es Salaam: Tatu Binti Mzee, pamoja na Bibi Titi Mohamed.
Tatu Binti Mzee alikuwa mmoja wa wajumbe wanawake wa kwanza katika chombo muhimu cha maamuzi, yaani, Kamati Kuu ya Chama.
Halima Hamisi, huyu naye ni mpambanaji wa kuleta uhuru, katika utafiti wa Susan, ananukuliwa akisema: “ Tulitembea kwa miguu siku nzima bila chakula.
“Ukichukua chai nyumbani na ukijaliwa kupata karanga, unanunua. Wakati mwingine tuliweza kupata fedha za chakula kutoka ofisi ya TANU, lakini ilibidi wapige hesabu kwa makini….”
Wanawake wengine wa Dar-es-Salaam, walioshiriki harakati za kuleta uhuru na majina yao yamefunikwa na historia ni: Salima Ferouz, Binti Kipara, Mwasaburi Ali, Fatuma Abdallah na wengine wengi ambao watafufuliwa na tafiti nyingine zitakazofanyika kwa kuchochewa na hii ya Susan.
Katika utafiti wa Susan, Salima Ferouz, ananukuliwa akisema: “ Sisi wanawake tulikuwa na nguvu… tuliongoza njia kwa sababu ya uonevu wa watoto wetu na jinsi tulivyowekwa ndani… tulifanya kazi pamoja, tukajiunga na Kitengo cha wanawake na kutumikia TANU, tukichangisha fedha na kuwahamasisha wengine wengi wajiunge..”
Hata mikoani kulikuwa na wanawake walioshiriki harakati za ukombozi wa taifa letu. Kule Kilimanjaro kulikuwa na Halima Selengia Kinabo, Mwamvita Salim, Zainab Hatibu, Morio Kinabo, Violet Njiro, Elizabeth Gupta, Kanasia Tade Mtenga, Natujwa Daniel Mashamba na Lucy Lameck.
Hata kule Mwanza kulikuwa na wanaharakati wanawake waliopigania uhuru wa taifa letu, lakini historia haiwakumbuki tena. Wanawake hao ni: Agnes Sahani, Aziza Lucas, Tunu Nyembo, Halima Ntungi, Mwajuma Msafiri, Pili Juma, Mwamvua Kibonge, Zuhura Mussa na Chausiku Mzee.
Ni wazi wako wanawake wengine wengi walioshiriki harakati za kuleta uhuru wa taifa letu, ni kazi ya Mashirika yanayotetea usawa wa jinsia na ukombozi wa mwanamke kwa kushirikiana na Watanzania wanaopenda kuweka kumbukumbu sahihi kuendeleza utafiti na kuibua majina mengine ya wanaharakati wote walioshiriki kuleta uhuru wa taifa letu.
Tusitake kusherehekea kwa kuimba, kunywa na kucheza bila kuiandika historia sahihi ya taifa letu.
Ni lazima tujiulize tumeteleza wapi? Kama huko nyuma tuliweza kuendesha harambee ya kuchangia harakati za mapambano, shughuli zote zikaendelea bila misaada ya kutoka nje. Mapato yote ya nchi yakiwa mikononi mwa mkoloni.
Inakuwaje sasa wakati tumeshika mapato ya nchi mikononi mwetu, tunaendelea kuomba misaada ya kujenga vyoo na vyandarua? Uwezo wa kujitegemea uliokuwa miongoni mwa wananchi wakati wa kupigania uhuru umekwenda wapi?
Tulipigania uhuru wa kisiasa, ili tupoteze uhuru wa kujitegemea na kujiamulia mambo yetu wenyewe? Ukipokea misaada, ni vigumu kukwepa masharti yake!
Makala hii ni mwanzo mzuri wa kuangalia mchango wa mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayoshughulikia usawa wa jinsia na ukombozi wa mwanamke.
Swali la kujiuliza ni je, kama wanawake walikuwa mstari wa mbele wakati wa kupigania uhuru wetu, ilitokea nini wakawa mstari wa nyuma baada ya uhuru?
Wanawake walichangisha fedha za kuendesha mapambano, walifanya kazi kwa nguvu kupata fedha, walipika maandazi na wengine walifanya kazi za kujidhalilisha ili wapate fedha za kukiendesha Chama cha TANU. Mapambano ya kuleta uhuru hayakutegemea misaada kutoka nje.
Uwezo mkubwa wa kujitegemea ulioongozwa na wanawake ulikwenda wapi baada ya uhuru kufikia hatua ya kutafuta fedha kutoka nje ili kuendesha “ Miradi” ya kuwakomboa wanawake wa taifa letu? Ni lazima kutafakari kwa kina wakati tukisherehekea miaka hamsini ya taifa letu.
 
Tuana sherekea miaka 50,nakujivunia,pia tunamacho yakuona sehemu muhimu za kazi za kijamii na makazi ya watu,
KARIAKOO KARIAKOO,Afya kwa watu mbona haiangaliwi?ukipita kariakoo "MAVI MAVI" KONA ZOTE KUNANUKAAAAA!,inamaana mabwana afya hawafanyi kazi?hakuna Report zinazoandikwa zinazoonyesha hali ilivyo mmbaya ili wahusika wachukue hatua?TUNAKWENDA WPI TANZANIA?TUNKWENDA WAPI JIJI LA DAR ESS ALAAM?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tuana sherekea miaka 50,nakujivunia,pia tunamacho yakuona sehemu muhimu za kazi za kijamii na makazi ya watu,
KARIAKOO KARIAKOO,Afya kwa watu mbona haiangaliwi?ukipita kariakoo "MAVI MAVI" KONA ZOTE KUNANUKAAAAA!,inamaana mabwana afya hawafanyi kazi?hakuna Report zinazoandikwa zinazoonyesha hali ilivyo mmbaya ili wahusika wachukue hatua?TUNAKWENDA WPI TANZANIA?TUNKWENDA WAPI JIJI LA DAR ESS ALAAM?


Hii inasababishwa na hao wanaojiita Viongozi ambao hawana sifa hata moja ya uongozi. Wanaona miji/majiji yetu mingi/mengi ilivyokithiri/yalivyokithiri kwa uchafu lakini hawachukui hatua zozote. Hapa chini kwenye hii link ulifanyika usanii eti "kampeni ya kusafisha majiji/miji" mbali mbali lakini kama kawaida haikuwa na mafanikio yoyote, ufuatiliaji sifuri.

The Vice-President's Office - News and Events - News
 
Tunakwenda kuzimu, wewe ulifikiri tunakwenda wapi?

Kumbe na wewe unajua kuwa CCM inatupeleka kuzimu kwa kasi ya kutisha? Sasa unahsuri tufanyejei tusiendelee na safari hiyo. Tunataka tuwe kama wenzetu wa China na Singapore.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndugu zangu taarifa za uhakika ni kwamba wakuu wa mikoa wanachangisha fedha kutoka kwa wafanya biashara binafsi, makampuni binafsi, viwanda, taasisi za serikali,halmashauri za miji na wilaya, manispaa, taasisi ambazo sio za kiserikali, mabenki ya ndani na ya nje yanayofanya biashara katika mikoa yao, wasafirishaji wa mizigo na abiria nk.list ni ndefu. Fedha hizi zinahitajika kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara katika mikoa husika na pia kugharimia ushiriki wa mikoa katika maadhimisho ya kitaifa ambayo yatafanyika Dar kwenye viwanja vya mwalimu nyerere kilwa road kuanzia 1/12/2011 mpaka 12/12/2011 baada kusema hayo naomba kufahamishwa yafuatayo:-
1. Gharama za maadhimisho haya ziliwekwa kwenye bajeti ya wizara inayoratibu maadhimisho haya?.
2. Kama ndiyo uhalali wa michango hii uko wapi? Au ndiyo yale yale yaliyokemewa na wabunge katika kikao cha juzi yanapelekwa kwa wananchi badala ya taasisi zilizo chini ya wizara husika?.
3. Jee wizara husika imeipatia mikoa fedha? Kama hapana kuna haja gani ya mikoa kufanya hayo maadhimisho? Si yafanyike kitaifa tuu.
4. Jee ni kiasi gani mikoa imeruhusiwa kuchangisha na zitatumika vipi?
5. Baada ya maadhimisho hayo accountability ya fedha hizo itafanyika vipi??????????
 
NImekuta na mshikaji wangu kawapa kama laki 6 ivi,nkamuuliza kwani ungewanyima wangefanya nini akasema iyo ni serikali si wanaweza nitumia TRA apa ukashangaa unadaiwa billioni.
Ni mwendo wa kuomba omba serikali haina ela.
Sasa uombe kwa mambo ya msingi sasa unaomba kwa ajili ya sherehe ivi ni muhimu kiasi icho?
CCM kweli mumepoteza malengo ata mambo ya msingi ya wapiga kura wenu mnayatelekeza mko bize na 50 YEARS OF TANGANYIKA INDEPENDENCE
 
NImekuta na mshikaji wangu kawapa kama laki 6 ivi,nkamuuliza kwani ungewanyima wangefanya nini akasema iyo ni serikali si wanaweza nitumia TRA apa ukashangaa unadaiwa billioni.
Ni mwendo wa kuomba omba serikali haina ela.
Sasa uombe kwa mambo ya msingi sasa unaomba kwa ajili ya sherehe ivi ni muhimu kiasi icho?
CCM kweli mumepoteza malengo ata mambo ya msingi ya wapiga kura wenu mnayatelekeza mko bize na 50 YEARS OF TANGANYIKA INDEPENDENCE

Kwa taarifa yako zoezi hili la kuchangisha linaangaliwa kwa karibu sana na kamati ya ulinzi na usalama ya mikoa ole wako uonekane hupendi kuchanga na kushiriki utaangaliwa kwa karibu sana tena with open eye na kamati hii.
 
Kwani gharama ya maadhimisho ni nini?, wahudhuriaji watapewa pilau na ulabu au?, huu ni wizi mtupu.
 
Kwani gharama ya maadhimisho ni nini?, wahudhuriaji watapewa pilau na ulabu au?, huu ni wizi mtupu.
Ndugu yangu nachotaka kufahamu ni kwa nini serikali haikuomba fedha kwa ajili ya hii shughuli kwa sababu mimi nakerwa sana na hii michango ni juzi tuu walinifuata kwa mchango wa mwenge jana wakaja na mchango wa kujenga madarasa ya sekondari, na leo nimefuatwa nitoe fedha kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru!!!
hivi hizi fedha zinazotokana na vianzo mbali mbali vya mapato ya serikali zinaenda wapi?? hospitali hakuna dawa mahakamani hakuna karatasi, magari ya polisi hayana mafuta. naomba uhalali wa hii michango tafadhalini sana.
 
Back
Top Bottom