Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,627
Wanabodi,
Chadema imetimiza miaka 30.
Tangu ile Chadema inazaliwa miaka 30 iliyopita, imezaliwa na kunikuta mimi tayari niko newsroom kwa zaidi ya miaka 2, hivyo Chadema imezaliwa naiona, inakuwa naiona, ilipofika peak naiona, na sasa imeanza kusinyaa naiona, na ikiendelea hivi kwa mwendo huu, naiona kule inakoelekea, hivyo hili ni bandiko la ushauri, ili isifike huko ninakokuona mimi.
Hili ni bandiko la SWOT Analysis, na PEST Analysis, ya Miaka 30 ya Chadema huku nikiwashauri wa imarisheni strengths zao, na kushughughulikia weakness zao, na kama ikibidi to start afresh, Chadema is start a fresh!.
Mtu Asiye Chadema, Anaishauri Chadema Kama Nani?
Japo chama cha siasa ni mali ya wanachama, vyama vya siasa nchini Tanzania, vyenye wabunge na madiwani, ambavyo vinapokea ruzuku ya serikali, sio private parties za wanachama tuu, ni public parties za umma, paid by taxpayers money, ndio maana hesabu zake zinakaguliwa na CAG, hivyo sisi as public, mimi nikiwemo, we have all the rights to ask, know or make comments kuhusu all it's affairs, public as well as private.
Declaration of interest.
Mimi ni kada wa chama cha Mapinduzi, ila chama cha Mapinduzi kina makada wengi na wa aina nyingi na makundi mengi, kada mimi ni type mpya ya makada wa CCM, tunaitwa CCM Contemporary, tunaoamini katika kutenda haki bin haki, CCM ikishinda uchaguzi, ishinde kwa haki, katika uchaguzi huru na wa haki, huku tukiamini bila upinzani imara, hakuna CCM imara.
Kiukweli kabisa Tanzania, hatuna upinzani imara, hivyo
huu ni ushauri wa bure, kwa Chadema, wa tathmini yangu ya Chadema ilipotoka, ilipo na inapokwenda, na Chadema mko huru kuusoma au kutousoma, kuuelewa au kutoelewa, kuufuata au kutoufuata, au hata kuupuuzia, mimi nitakuwa nimetimiza wajibu wangu.
Ushauri huu nauweka kwenye points format huku nikionyesha nilishauri nini na nini kikatokea.
Highlights
Intro SWOT ni nini na PEST ni nini?.
SWOT na PEST za kazi gani, au za nini?.
Historia ya Chadema
Chadema ile iliyokusudiwa
Mapito ya Chadema
Uimara wa Chadema
Udhaifu wa Chadema
Makosa ya Chadema
Matokeo ya makosa ya Chadema
Chadema ya Sasa
Chadema ilipo
Chadema inapokwenda
A Way Forward.
Hitimisho.
Intro SWOT ni nini na PEST ni nini?.
SWOT ni neno la Kiingereza ambalo ni kifupi cha Strengths, Weaknesses, Opportunities, and Threats, ambapo hapa unachambua uimara, changamoto, fursa na hatari au tishio kwa Chadema.
PEST Analysis ni kifupi cha Political, Economic, Social and Technological.
SWOT na PEST ya Chadema ni za Nini?
SWOT analysis ni kupima utendaji wa Chadema kama chama cha siasa katika kutimiza malengo yake. PEST analysis inapima trends na kuonyesha mialekeo ya Chadema kwenye the game of politics. A SWOT analysis ni subjective assessment wakati PEST analysis ni objective.
Historia ya Chadema
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kiliomba rasmi usajili Tarehe 28/05/1992 na kupewa usajili wa muda, Tarehe 2 July 1992, kikafanya Mkutano wake Mkuu wa kwanza wa kuiasisi Chadema, Ukumbi wa Msimbazi
uliohudhuriwa na waasisi 89, ambao mimi nilihudhuria nikiwa ripota wa RTD.
Hawa ndio Wanachama Waasisi wa Chadema
Kati ya wanachama hawa waasisi wa Chadema, sijui ni wangapi bado wako Chadema mpaka sasa zaidi ya Freeman Mbowe.
Tarehe 21, mwezi January, mwaka 1993 ndipo Chadema kikasajiliwa rasmi kwa usajili wa kudumu na Msajili wa kwanza wa Vyama vya Siasa, Balozi Jaji Mst. George Liundi kikiwa ni chama nambari 3 baada ya CCM Numbari 1, na CUF Nambari 2
Hivyo usikute japo mimi sio Chadema, kama jina lako halipo kwenye majina hayo, ujue mimi naijua Chadema kuliko wengi wa Chadema wenyewe kwasababu nilikuwepo hapo siku hiyo!.
Kufahamiana na Viongozi Wakuu wa Chadema.
Edwin Mtei ni baba mzazi wa Class mate wangu kwa miaka 7, enzi za Primary, 1975-1981 ikiwemo kufika kwake kote kote Dar na Arusha-, hivyo kuna uwezekano kuna watu humu wanadhani wana,fahamu sana muasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei, kumbe wamemfahamia Chadema, mimi nimemfahamu toka akiwa Gavana, sambamba na Bob Makani.
Freeman Mbowe tumefahamiana kitambo, toka akiwa DJ, Mimi na Uncle J Nyaisanga ndio tumekuwa ma MC wa kwanza wa Club Billicanas ile inafunguliwa 1993, 1995, nimeendeshea kipindi cha Kiti Moto kutokea Bills, na nilipoa ile 1995, vikao vyangu vya harusi vimefanyikia Bills, nilipewa ukumbi bure na Freeman mwenyewe in person.
Nawaomba sasa sana sana kwa sasa, jiuzuie kadri uwezavyo msichangie chochote kwanza kwenye uzi huu hadi nondo zitakapo anza kushuka.
Natanguliza shukrani
Karibuni.
Paskali