Miaka 3 tangu kufariki kwa CPWAA, unamkumbuka kwa wimbo gani?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1705482323361.jpeg

Leo Januari 17, 2024 imetimia miaka 3 tangu kutokea kwa kifo cha Rapa Ilunga Khalifa maarufu kama CP aka Crazy Power a.k.a CPWAA au Mfalme wa Bongo Crunk aliyefariki Januari 17, 2021

Wakati wa uhai wake, CPWAA alifanya vizuri na ngoma nyingi zikiwemo 6 In The Morning, Problem, Pwaa na Action. Pia, alikuwa mmoja kati ya Wasanii waliounda kundi la Park Lane akiwa na Suma Lee ambaye kwasasa ameachana na Muziki

Unamkumbuka kwa ngoma gani mkali huyu wa Bongo Flava?

Soma TANZIA - Msanii Ilunga Khalifa maarufu 'C Pwaa' afariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili
 
Kwanza nilianza kumuelewa kwenye Nafasi nyingine akiwa na wenzie Parklane.
Pili Problems, ulikuwa na kichupa kikali sana enzi hizo niko sekondari full kuiga ya mule, lol
Tatu Action, sihitaji kusema zaidi...

Jamaa alikuwa mnyama, RIP!
Problem ulikua sekondari!!..we mchumba zuchu tu kumbe!?.. problem nimemaliza chuo kitambo,maisha yananionesha kwamba elimu si lolote,msoto wa maana
 
Problem dude la maana,nna wanangu walikua wanadai kile kidada cheupe kwenye problem kilimtaka mwamba aagize na mafuta wakayatumie kudinyana..nilikua nakiangalia sana
 
View attachment 2874344
Leo Januari 17, 2024 imetimia miaka 3 tangu kutokea kwa kifo cha Rapa Ilunga Khalifa maarufu kama CP aka Crazy Power a.k.a CPWAA au Mfalme wa Bongo Crunk aliyefariki Januari 17, 2021

Wakati wa uhai wake, CPWAA alifanya vizuri na ngoma nyingi zikiwemo 6 In The Morning, Problem, Pwaa na Action. Pia, alikuwa mmoja kati ya Wasanii waliounda kundi la Park Lane akiwa na Suma Lee ambaye kwasasa ameachana na Muziki

Unamkumbuka kwa ngoma gani mkali huyu wa Bongo Flava?

Soma TANZIA - Msanii Ilunga Khalifa maarufu 'C Pwaa' afariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili

Namkumbuka sana mshikaji enzi zile akishiriki mashindano ya rap mkoa wa mbeya pale jengo la nssf.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom