Miaka 10 ya kifo cha Albert Mangwair, unamkumbuka kwa ngoma gani mkali huyu?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1685286272687.png
Leo Mei 28, 2023 imetimia miaka 10 tangu kutokea kifo cha ghafla cha Nyota wa Hip Hop, Bongo Flava na Mkali wa "Freestyle" kutoka East Zoo Dom, Mangwair au Ngwair au Cowbama

Wakati wa uhai wake, alijizolea sifa ikiwemo kuwa na uwezo kuingia studio na kurekodi 'Ngoma' bila kuandika (Freestyle) na bado wimbo ukawa mkali na unaoeleweka, ikiwa ni tofauti na 'Freestylers' wengi ambao huishia kuweka Vina' bila kuwa na maana

Ngwair alifanikiwa kuachia Albamu 2, (A.K.A MIMI - 2004 na NGE 1982 ya mwaka 2009), alitamba na vibao kama Ghetto Langu, Mikasi, Sikiliza, CNN, Nipeni Deal n.k. Alifariki dunia Mei 28, 2013 akiwa Nchini Afrika Kusini

Unamkumbuka kwa wimbo gani mkali huyu??
 
Albert Mangwair hajawahi kuwa na Ngoma mbovu....hata zile alizokuwa anaimba Kwa ajili ya chama chake Cha siasa Bado zilikua kali... Apumzike mahala pema fundi huyu...
 
Leo Mei 28, 2023 imetimia miaka 10 tangu kutokea kifo cha ghafla cha Nyota wa Hip Hop, Bongo Flava na Mkali wa "Freestyle" kutoka East Zoo Dom, Mangwair au Ngwair au Cowbama

Wakati wa uhai wake, alijizolea sifa ikiwemo kuwa na uwezo kuingia studio na kurekodi 'Ngoma' bila kuandika (Freestyle) na bado wimbo ukawa mkali na unaoeleweka, ikiwa ni tofauti na 'Freestylers' wengi ambao huishia kuweka Vina' bila kuwa na maana

Ngwair alifanikiwa kuachia Albamu 2, (A.K.A MIMI - 2004 na NGE 1982 ya mwaka 2009), alitamba na vibao kama Ghetto Langu, Mikasi, Sikiliza, CNN, Nipeni Deal n.k. Alifariki dunia Mei 28, 2013 akiwa Nchini Afrika Kusini

Unamkumbuka kwa wimbo gani mkali huyu??

Kimya kimya akiwa na j, aise hii ngoma from beat,lyrisc ,michano ni
 
Sijui kwa nn sikuwahi kumpa attention akiwa hai, ila kadiri ninavyosoma stories zake nazidi kukubali kazi zake .
Kwa wanaomjua huyu jamaa ilikuwaje akaingia kwenye madawa kirahisi hivo
 
Hakuwa na maajabu yoyote ni msanii kama wasanii wengine tu.

HUJAFA HUJASIFIWA
 
Mangwair alikuwa ni zaidi ya kipaji. Kuna muda ukiwa unamjua mtu ndiyo unajua thamani yake. Rest easy well Albert 🖤
 
Back
Top Bottom