Tutayamaliza yote kumhusu Albert Mangwair au tutayataja machache na kuyasahau mengi?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
TUTAYAMALIZA YOTE KUMHUSU AU TUTAYATAJA MACHACHE NA KUYASAHAU MENGI?

1. Kutokana na wimbo wake wa GHETTO LANGU, vijana wakaziita nyumba au vyumba walivyopanga kwa jina la NGWEA. Ilikuwa kawaida na (wengine wamekuwa wakiendelea kusema) "nipo ngwea" wakimaanisha wapo ghetto. Albert ameacha alama isiyofutika.

2. Mitindo huru (ISIYOANDIKWA) imekuwa kipengele kinachowawia ugumu rappers na MCs wengi lakini Ngwea anaingia katika orodha ya vichwa vichache vilivyofanya freestyles kama mchezo wa kutafuna jojo.
Heshima kubwa ilikuwa kwa;
Hashim Dogo
Ndipo akaibuka
Albert
Kisha akaja Rashid Abdallah Makwilo " Chid Benz"

Kikaibuka kizazi kipya chenye majina kama Nikki Mbishi, Godzilla, Mkristo, Haidary Scoda, Rota, Cado Kitengo na wengineo wanaoibukia na wale walioko chimbo.

Kuna video clip ambayo anafanya live show na Fid Q jukwaani, Fid kapiga vesi yake lakini Ngwea kafanya freestyle mwanzo mwisho.

Vipi ile freestyle yake ya mwishoni kabisa aliyoifanya pale Mawingu walipoenda kutambulisha BALL PLAYER YA IZZO ile " ya COCA-COLA NA KOROSHO"

3. Albamu yake ya AKA MIMI inatajwa na wengi kuwa MIONGONI MWA ALBUMZ BORA KABISA ZA RAP BONGO lakini ukiitegea sikio NGE 1982 UTAONA KWAMBA USIPOIJUMUISHA KWENYE ORODHA YA ALBUMS BORA UNAMKOSEA HESHIMA NGWEA.

4. GHETTO LANGU ni wimbo unaoelezea nyumba ya fahari yenye kila kitu kwa kijana 'anayekwenda na wakati'. Nimesikia na kusikiliza nyimbo nyingi zenye maudhui ya namna hii lakini hakuna unaoukaribia wimbo huu hata kwa mbali.

5. NITAJIE MSANII ALIYEIIMBA STAREHE KWA UBUNIFU NA KIWANGO CHA JUU KUMZIDI NGWEA!
NGWEA ALIIJUA STAREHE.
TZ HUSTLER, WEEKEND, CNN, MIDA MIBOVU, MIKASI ni ngoma kali mpaka kesho.

6. Rapa gani aliweza kuimba kwa sauti TOFAUTI na KWA UBORA KUMZIDI NGWEA? anza na vesi ya pili kwenye GHETTO LANGU, njoo kwenye vesi ya pili ya CNN, ondoka hapo, icheze WEEKEND halafu hesabu humo ametumia zaidi ya sauti ngapi, hama hapo, sikiliza ACTION ya CP halafu urudi hapa, uniambie kama una jibu tofauti.

7. Alipoandika kuhusu mada tofauti na starehe, bado alikaza sana mistari;
NAOMBA NISAMEHE
MASKINI WENZANGU
AHADI ZA BOSS
ZAWADI
AKA MIMI
MSELA
BILA MUZIKI FT BUSHOKE

8. Kazi zake zilizorudiwa na wasanii wengine.
DAKIKA MOJA - FA/AY FT HARD MAD
GHETTO LANGU - MSWAKI
WAKATI NDO HUU - NIKKI MBISHI
MADEMU WANGU - P THE MC
NB; Yule DULLA MAKABILA na wimbo uliompa umaarufu wa KABILA LAKE, una tofauti gani na MADEMU WANGU ya Ngwea?? Au nd'o NO IDEA IS ORIGINAL??

9. Nyimbo zilizotoka wakati anakaribia kukumbwa na mauti na baada ya kifo chake;
BABY - QUICK ROCKER.
BILA WEWE -JORDAN
LOOKIE LOOKIE - BLACK RHYNO
BALL PLAYER - IZZO B

10. Uwezo mkubwa wa kurap kwa Kiingereza na Kiswahili. Kwenye Kiswahili, ushahidi upo wazi, vipi kwenye ung'eng'e alioupiga kwenye ngoma kama;
STREET - NCHA KALI
WE MAKE IT ALRIGHT - ZIZZOU ARTISTS
SHE PERFORMS FT TID
MAMA MIA - Q CHILLA

11. MTU PEKEE DUNIANI ALIYEMFUTISHA VESI FID Q NA BADO ALIPOANDIKA VESI MPYA AKAENDA OFF- TOPIC.

13. Unakumbuka ile 'cheza yake' kwenye video ya HAPO VIPI ya PROF JAY? Baada ya kutubamba, Chid Benz akaona usin'tanie akaihamishia kwake.
14. MTU PEKEE ALIYEAGWA KWA WIMBO NA GEEZ MABOVU NA LANGA NA WAO WAKAMFUATA.

15. MTU PEKEE AMBAYE ALIPOFARIKI, LADY JAY DEE NA MWANA FA WAKAAHIRISHA MAONESHO YAO.

16. MTU PEKEE ALIYECHUKUA IDEA YA MSANII MWENZAKE NA KUMSHIRIKISHA HALAFU REMIX IKAWA KALI KULIKO ORIGINAL IDEA.

NDIYO, NAONGELEA MIKASI, AMBAYO ILIKUWA IDEA YA TAIKUN ALLY " MCHIZI MOX" HALAFU MWANA AKAENDA KWA MAJANI NA VICHWA KADHAA, MOX AKIWEMO, GOMA LIKATOKA LA MOTO, MOX AKAONA 'AH! HII SIKUBALI'

17. MTU PEKEE AMBAYE CP NA MARCO CHALI WALICHUKUA SAMPLES ZA NGOMA YAKE YA MIKASI NA ALIPOSHIRIKISHWA ILI KUONDOA SINTOFAHAMU, AKAINGIZA VOKO BILA SHIDA NA NGOMA IKAWA KUBWA.

18. Sikiliza NO BEEF ft TID inakupa vitu viwili kwa mara moja. NGWEA HAKUWA NA BEEF NA MTU lakini pia aliwahi kuulizwa kuwa alidhani anastahili kuitwa MFALME, alijibu, " HATA NIITWE VYOVYOTE LAKINI IKIMAANISHA MIMI NI BORA, IT'S OK"

19. NOORAH alifahamika zaidi kama BABA STYLES, Ngwea pia aliheshimika kwa styles lakini wawili hawa hawakutupa ngoma kali wakiwa wawili. Pengine waliamini kuwa muda bado upo. Walitukosea sana. Nakumbuka walifanya CHAMBERVMENT kwa HERMY B lakini pia walifanya DAKIKA MOJA na zile ngoma za CHAMBER SQUAD ikiwamo BWII.

20. Miongoni mwa vichwa vilivyoitengeneza himaya kubwa ya BONGO RECORDS, ambayo Dizasta anasema NI MKUBWA KULIKO THIS WHOLE LABEL kisa kukosa adabu kwa mtoto Cosmas.

Nimeandika mambo 20 lakini bado naona kuna mengi yamebaki. Nisaidie kuyaongezea yale ambayo hayajaguswa na kalamu yangu.
NGWAIR IS TO LIVE FOREVER!!!
CHAMBER SQUAD
EAST ZOO
WE STILL RESPECT AND LIVE YOUR LEGACY, KING!!!
Luah
MWANDISHI WA AINA YAKE.
330336393_709705624276039_793943057665578224_n.jpg

331553504_234625952328307_7135529246442365783_n.jpg
 
Dogo alikuwa anaweza sana ila ila kosa watu sahihi kwenye maisha yake ya kawaida hii nyimbo yake huwa haipotezi ladha kwenye maskio na hisia zangu. Hapa alishirikishwa tu na Mchuzi mox lakini aliudominate
 

Attachments

  • Mchizi Mox-Demu Wangu ft Ngwair.mp3
    4.8 MB
Ana album pekee niliotoa ela yangu nikanunua na kuifadhi kanda adi ilipoibiwa miaka mitatu mbele..katika kila playlist yangu haiwezi kukosa nyimbo yake..katika simu yangu nna nyimbo zake zote adi sasa..kwangu bado anaishi kijana wangu ngwear
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom