Mhitimu, Serikali ifanye nini ili uweze kujiajiri?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Hii ishu imesemwa sana lakini naomba nirudie. Serikali yetu imeajiri watu kama laki tano tu usipojumlisha wanajeshi na polisi. Sehemu kubwa ya hao, kama asilimia 50 ni waalimu.

Ukiangalia hapo hata serikali ikisema iajiri watu kadri inavyoweza haitaweza kutatua tatizo la ajira.

Serikali inatakiwa kuweka mazingira mazuri ya kujiajiri.

Mhitimu na kijana usiye na ajira, serikali ifanye nini ili uweze kujiajiri?
 
Iondoe utitiri wa kodi

itoe vipaumbele kwa biashara zinazoanza

ifute au kusamehe madeni ya zamani

itengeneze mazingira mazuri ya masoko

Itoe mwanga mzuri na nafasi kwa wadau wanaotoa mikopo

Itoe sapoti kama maeneo ya kulima, kufuga, mabwawa na supportive education kwa vijana walikwisha anza miradi midogo midogo buree
 
Tumechoka kuwanyenyekea hao serilikari daily wafanye nini wafanye nini.

Be Selfish
 
Swali uliza kwanza mhitimu yeyote unayemjua kama kichwani kwake ana hata wazo la kujiajiri ajiajiri kwenye nini? wengi weupe tu kichwani hamna kitu nimefanya utafiti binafsi hwengi hawana wazo hata moja labda tuombe wazazi waulize watoto wao kuwa kama nikitafuta mtaji mwanangu waweza kupenda kujiajiri kwenye kipi? Nakuhakishia wazazi wengi wakiuliza watoto hili swali watashangaa mtoto hana alijualo ni mweupe kabisa kichwani.

Nawasihi wazazi jaribuni kuuliza wanenu hilo swali hata sasa hivi tumeni meseji au wapigieni simu ghafla kuwauliza mtashangaa wenyewe kuwa mna mitoto isiyojielewa mkifa leo itaishia pabaya.
 
Back
Top Bottom