Mheshimiwa Zitto, kwa hili umekosea

Mheshimiwa Zitto, kwa hili umekosea

Uchumi umedoda na ndo kiama kwa Taifa, ninavyofahamu mie jinsi tulivyo naomba Mungu tu mvua zinyeshe wakulima mama/bibi zetu wajipatie mazao ya kutosha njaa isiwamalize.

Na bahati mbaya balaa hili linaukumba Tanzania wakati nchi nyingi wanaotupa msaada nao wapo ktk hali ngumu. Soln, ni kuipindua utawala, tupilia mbali uongozi wote na wabunge waliopo. Ije serikali mpya kabisa na wala sio kutoka vyama vilivyopo. 2015 mbali sana.

Wafanyakazi wagome kwenda makazini, wasiandamane bali wagome tu kwenda makazini. Hii ndo soln ya kureform uchumi.
MkamaP u speak my language.
 
Kama tunataka kusambaza umeme vijijini,itabidi TANESCO iwe overhauled na ioperate at a break even point to minimize costs kwa wanavijiji,sidhani kama hii ni recipe nzuri kwa private investors,otherwise tanesco ingeshakuwa na private captal kubwa tu!

U r quite right..but on overhauling part it might not be the soln as we have REA every TANESCO customer contributes 3%....but if TANESCO has to operate profitably then govt has to subsidize loss making areas...areas which are thermal fired plants where cost of production is higher than returns
 
Vua hayo magamba kwanza ndio nichangie upuuzi wako.......
wakatio great thinkers wanaspojadili hoja ya maana na kumvuta hadi muwakilishi wetu zito kuja kufanya masahihisho.. basi kama huna cha kuchangia bora ungebaki msomaji tu!! kuliko huu upuuzi ulioandika
 
Ujue waheshimiwa wanajamvi, kuna wakati huwa napata taabu sana nikifikiri, hivi wanasiasa wa Tanzania huwa hakuna kitu mwisho wa siku kinawaunganisha? kuna mambo mengi sana yanatokea hapa nchini yanayohitaji "attention" ya kila mmoja wetu bila kujali itikadi za siasa lakini kila kitu ni kambi tu za siasa, tunayaona haya hasa bungeni, ifike mahali tuwe kitaifa zaidi, tuwasaidie watanzania,wananchi wamechoshwa na malumbano wanahitaji maendeleo.

Vile vile, CHADEMA ndiyo mnayo mambo mengi yanayoleta matumaini makubwa kwa watanzania ila sasa kumbukeni siku moja mtashika dola geukeni pia muwaeleze watanzania nao pia ni sehemu ya tatizo la umasikini wao, watanzania walio wengi ni wavivu, vijana wengi hawafanyi kazi wanapenda short-cut.
 
Lengo ni kufloat tanesco in the near future. Tanesco ni kampuni binafsi inayomilikiwa na serikali kwa asilimia 100. Maana yake ni kwamba tanesco imesajiliwa kupitia cap 212 kama kampuni nyingine yeyote, hivyo kuiorodhosha hisa zake katika soko la hisa ni rahisi zaidi.

Tatizo tanesco bado haijaanza kufanya faida. Sheria ya capital markets inataka kampuni iwe inafanya faida kwa angalau miaka mitatu mfululizo kabla ya kulist DSE.
Tumewapa lengo hilo tanesco, hasara imekuwa ikishuka sana lakini bado hawajaweza kupata faida.
Ni kweli kwamba wingi wa makampuni peke yake hauleti liquidity. Lakini ni hatua mojawapo muhimu kwa kila soko la hisa ie market capitalisation. Wingi wa hisa unasaidia kupata products mbalimbali katika soko na financial engineers wanasaidia kupanua soko. Hivyo ni muhimu sana kuongeza kampuni katika soko.
Kuhusiana na cost-benefit, mtanganyika atakuwa anafahamu kuwa ile dividend badala ya kwenda serikalini sasa itakwenda kwa wananchi moja kwa moja. Pia serikali itaendelea kupata kodi ie corporation tax na witholding tax on dividend. Hivyo ni suala la kuangalia na kusema glasi ipo half full au half empty!
Tukumbuke, listed companies zinakuwa na uwazi zaidi kwa mujibu wa sheria. Sababu kubwa ambayo imesababisha serikali ishindwe kukusanya kodi katika mauzo ya zain to airtel (tshs 470) ni kampuni hiyo kutokuwa listed pamoja na udhaifu wa sheria yetu ya kodi. Pamoja na kwamba kila mteja alinunuliwa kwa takribani dola 227 wakiwemo watanzania, TRA collected zero.
ABSA pia wameuzwa kwa Barclays ikiwemo NBC yetu (mtakumbuka nyerere alitaifisha barclays na kuiita NBC in 1967). Mauzo hayo pia hakuna kodi tuliyokusanya. Listing itaweka mambo mengi wazi, market ita react na itasaidia sana nchi.
Tupeleke umiliki wa uchumi kwa umma kwa kuwawezesha kumiliki baadhi ya makampuni. Tuanze na yale ambayo serikali ina hisa

Zitto sasa nadhani tunaimba wimbo mmoja katika tofauti ala, kuna mambo mawili muhimu ambayo umeyaongelea ambayo nitayachambua kwa undani kabisa.

Kwanza ni swala la cost-benefit ratio, kwamba ni kweli serikali ikiuza share za mashirika hayo mawili Watanzania watakuwa wamiliki ambao technically watakuwa wanapata faida kisha wanatumia faida hiyo kukuza local economy. Vile vile serikali ya Tanzania itajikita zaidi katika ukusanyaji wa kodi (corporate tax and other withholding taxes). However, that statement is only in the well structured capital market. Nadhani loopholes ambazo zipo leo kwenye ukusanyaji wa kodi inabidi kwanza ZIZIBWE. Close all the loopholes includes Tax holidays ambazo hazina mbele wala nyuma, reduce witholding taxes kwa wafanyakazi, tight all the loopholes kwenye VAT and give tax credit kwa kampuni ambazo zina tengeneza product Tanzania. Kwa kufanya hili kwanza tutakuwa tunajipanga kwenda kwenye njia sahihi ya kubinafsisha.

Swala la pili: nikuhusu DSE, ukweli nikwamba Dar Es salaam Stock Market is more of a sysmbol than stock market. Sheria ya uuzaji na umiliki wa share imetungwa bila strong feasibility study, matokeo yake inabana kampuni nyingi kuja kukusanya mitaji. Vigezo vya kufuzu kuuza share in DSE ni total absurd. Hakuna financial tools ambazo zinawezesha liquidity, makampuni yanayo list yana limit financial disclosure, hakuna strong check and balance among makampuni na auditing firms. Hatuna strong commission ambayo imejikita zaidi kwenye kuchunguza makampuni haya kama yana fanya yanafotakiwa kwa washikadau.

Nadhani kabla hatujaingia kwenye bandwagon ya DSE and IMF conditions kwanza tujikite kwenye kuifanya hii DSE iwe stock market ya ukweli na sio propaganda. Tuipe necessary tools ambazo itaisababisha kuingiza more financial tools kwenye market, na watanzania wengi watafaidika. Kuna tools nyingi tuu kama commodities trading ambayo itasaidia sana wakulima wakubwa na wafanya biashara wa chakula. All this needs strong financial market ambayo imepewa more power and smart regulations.

Kuhusu Tanesco, Nadhani kuna mengi inabidi yafanyike kabla hata ya kuwaza kuiuza. Kwanza tuigawe kwenye vipande vitatu, uzalishaji, usambazaji and uuzaji. Baada ya hapo tuvunje vunje kipande cha uuzaji kiwe kinamiliwikiwa na kampuni zaidi ya moja, hizo kampuni zishindane kwenye namba ya wateja kudetermine price. Usambazaji unaweza kupewa atleast zaidi ya kampuni mbili na mwisho uuzalishaji uachiwe kwa serikali ambao sababu ya national interest lazima iwe ndio majority shareholder. Hizi njia tatu ndio zimetumika Australia au USA, nazimefanya kazi. However, it will need more than those three ways kuifanya Tanesco iwe profitable again.

Mwisho, Mh. Zitto kama mnaweza please and please again kalobby kubadilisha sheria za vigezo vya kulist kwenye DSE. Kusema kwamba kampuni lazima ionyeshe faida kwa miaka mitatu ni kuzuia wajasilimali ambao wana product zao kichwani lakini hawana mitaji. Tuwaache wawekezaji wachagua wapi wawakeze. Let us restructure DSE for the best.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mheshimiwa Zitto, kwanza mimi ni mwana CCM, lakini kwanza ni Mtanzania kama wewe kwani mtazamo na msimamo wangu kwanza kabla ya itikadi yoyote ni Tanzania Kwanza, Siasa Baadae! Lakini pili, lazima nikiri kwamba kuingia kwako katika medani za siasa ya nchi yetu kuliamsha sana moyo, udadisi na mvuto wangu juu za siasa za Tanzania. Nina uhakika vijana wengi hawatofautiani nami katika hili. Tangia mwaka 2005, umekuwa tumaini letu vijana wengi bila kujali vyama vyetu vya siasa kwamba – Vijana Tukiamua, Tunaweza!

Inaonyesha unamtazamo mzuri. Kwamba, nawe pia unachungu na nchi yako. Lakini jambo moja tu ndugu yangu. Kuti ulilokalia, siyo jema. Toka huko uliko uungane na Watanzania kudaii haki iliyo pokonywa muda mrefu na kaka zako. Sidhani kama kinondoni wangekuchagua kupitia CCM ungeweza tetea maslahi ya umma vilivyo. Next time ningependa kuona article yako ikinijulisha kuwa nawe pia uko CDM kwa maendeleo thabiti ya nchi. Goodluck!
 
Mkandara,
Nadhani hii si mara ya kwanza tuna bump heads on philosophical point of view.Jammi/umma ni maneno ya kiarabu,ujamaa umetokana na maneno hayo na maana yake ni taifa kuhodhi mali as a big ass family.Nyerere kwenye kitabu cha "The crusade for the liberation" ametafsiri ujamaa kama "Familyhood".
Kwenye interview na Gazeti la "The Courier" Edwin Mtei alisema ujamaa hata siku moja hautaijenga nchi hii,akasema private sector ndio itaijenga nchi hii.
Hivi sasa,GoT inacontrol 12% ya GDP yetu,na USA wana control 34% ya uchumi wao kama ni public sector.Sasa hebu niambie ni nchi gani ya kijamaa zaidi?
With the private sector controlling 88% ya total GDP,watanzania wameona maisha yao yakienda na maji huku uzalishaji wa madini kama ya dhahabu ukiongezeka kwa kasi na kilimo kikipungua kama ndio base ya uchumi wetu na kuwaacha wakulima hoi.
Tukisema sera za IMF zimetusaidia,hapo tutakosea,we have to suffer a lot kama tutataka watoto wetu wanufaike na maliasili yetu.....tusiwachekee wabinafsi hata kidogo!!
CHADEMA'S INPUT:
Kumkemea rais au serikali ipunguze bei ya sukari na vyakula...hii imesababisha serikali kuondoa import tarriffs na kuwanufaisha wafanyabiashara na kuwapunguzia mapato walalahoi.
Kusimamisha uzalishaji wa umeme kwa kampuni ya DOWANS.....hii ilileta upungufu mkubwa wa umeme ambao ulikuwa cheaper than IPTL na ulikuwa more consistent compared to others...matokeo ni faini ya bilioni 94!
Sasa hivi tena,wanataka kuuza shares za parastatals kuziba pengo la mapato,....huu ni uhuni uliokithiri kwani hii itanufaisha wafanyabiashara na si wakulima.
MY POINT?
Mlengo wa kati ambao CDM sasa wanasema ndio falsafa yao,hautuelezi kinagaubaga serikali itapataje fedha za kugharamia elimu,afya na ulinzi.Serikali imetumia kiasi gani?....na je,tukiondoa haya matumizi,tutaimarisha elimu na afya kwa kiasi gani?.....Hivi haya mafuta yanamnufaisha mkulima wa matombo? As compared to Bakhresa?
THATS THE ISSUE AND NOT WHO CAME UP WITH WHAT.
Mkuu shukran sana kwa majibu yako na hakika tunagongana sii kwa nia mbaya bali kuelimishana. Usihofie kuwa nafanya ubishi tu ili mradi kubisha.
Katika maswala haya mkuu wangu ni muhimu kuwa makini sana na tulisemalo kwa sababu unaweza kupotosha watu wengi kwa sababu tu hukuelewa mtazamo wa mtu mwingine, kwa mfano wewe unaposema Ujamaa maana yake ni taifa kuhodhi mali as a big family, mimi sikubaliani nalo zaidi ya kusema kwamba Ujamaa maana yake ni wananchi kuwa ndio wamiliki wa rasilimali zao na tofauti baina ya Ujamaa mmoja kwenda mwingine ni jinsi mnavyotekeleza sera za kufikia malengo haya. Huu ndio Ujamaa ambao nadhani tunatakiwa kuuzungumzia leo kutokana na wakati tulokuwa nao badala ya ule Ujamaa wa Nyerere na Kikumunist ambao ulisema mali zote za taifa ni mali ya wananchi kupitia serikali zao. Na ndio tukaona Utaifishaji wa mashirika ya Umma, ardhi kuwa mali ya Taifa na kadhalika..

Na labda nikukumbushe tu tena kwamba hata Mtei alikuwa Mjamaa wakati wa Nyerere isipokuwa alitofautiana na mwalimu ktk pendekezo lake la kuwatumia IMF kulikomboa Taifa ktk hali mbaya ya kiuchumi na alikuwa na kila haki ya kufanya hivyo akiwa kama waziri wa fedha pamoja na kwamba ilikuwa kinyume cha mtazamo wa mwalimu... Waliotofautiana na mwalimu ktk Ujamaa walikuwa kina Kambona na sii Mtei..

Halafu pia nakuomba ufahamu kwamba sii lazima watu wote wanaopingana na IMF ni Wajamaa kwa sababu tu IMF inasisitiza Ubinafsishaji na wala sii kweli kwamba nchi yeyote inayohodhi mali za Taifa badala ya wananchi ni Wajamaa kwa sababu hadi leo hii zipo mali kibao ambazo serikali ya Marekani, Uingereza, Canada, ambao ndio Mabepari haswa zinahodhiwa na serikali zao isipokuwa kwa mfumo tofauti wa kiutawala. Pia nchi hizi hizi zinaweza kutaifisha mali ya mtu binafsi na kuiweka chini ya serikali wakati wowote inapobidi.

Hivyo basi swala la kutaifisha au kubinafsisha sii swala la kiitikadi na narudia kusema Ujamaa sii lazima iwe Taifa kuhodhi mali zote kwani Liberal ya UK na Canada walibinafsisha mashirika mengi ndani ya utawala wao, China wanafanya hivyo na kwa uhakika zaidi CCM wamefanya hivyo wakati bado wanaamini kiitikadi kuwa mwongozo wao ni siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. La muhimu kwa msomaji ni kuelewa kwamba maana ya Ujamaa na Kujitegemea imebadilika toka ile ya Kimomunist kuja hii ya kulijenga Taifa moja na kwamba mali zote zilizopo nchini ni mali ya wananchi lakini sivyo wanavyofanya badala yake CCM wanabinafsisha mali nyingi za Taifa kwa Wageni na hata kuuza ardhi kwa wageni kiasi kwamba wamepoteza kabisa maana ya Ujamaa..

Na kama umenisoma vizuri hapo juu ndio unapata majibu ya maelezo yako kwa nini serikali ya US inahodhi asilimia 34 hali ya Tanzania inahodhi asilimia 12 tu, sasa nani Mjamaa zaidi nadhani mimi nimeliweka wazi zaidi yako unayeamini kwamba Ujamaa ni serikali kuhodhi mali zote as a big family na hapa US ipo karibu zaidi ya kuhodhi zote kuliko tanzania hivyo unataka kusema US ni wajamaa kuliko TZ..

Turidi ktk swala laetu, kwa nini watu wanashindwa kumwelewa Zitto ni kwa sababu bado wana mawazo ya Ujamaa wa kikomunist, ujamaa wa serikali kuhodhi njia kuu za uchumi na kwamba neno Public linahusiana tu na kuhodhi huko. Lakini kiuchumi na dunia ya leo Public company ni Private company vile vile likiwa sokoni likiuza hisa zake ambazo zinamilikiwa na wananchi sio serikali.

Kuna tafsiri moja nimeipata hapa niiweke..
- A public company or publicly traded company is a company that offers its securities (stock,bonds, etc.) for sale to the general public, typically through a stock exchange, or through market makers operating in over the counter markets. This is not to be confused with a Government-owned corporation which might be mis-described as a Publicly -owned company..

Mkuu huu ndio Ulimwengu tuliokuwepo leo na nakubaliana sana na maelezo yako mengi kuhusu hali halisi ya leo na tunatakiwa tufanye kitu gani. Wala siyapingi mawazo ya Zitto na ndio maana husema Zitto ni mtendaji mzuri sana, kasoma kaelimika na nipo nyuma yake sana ktk mambo mengi isipokuwa Zitto sii mwanasiasa na anapojaribu kutumia taaluma yake kisiasa ndipo hupoteza umaarufu wake. Zitto kama mwanasiasa ataweza tu kujipatia sifa pale anapozitumia siasa kwa faida yake na ya chama zaidi ya kuwataka CCM wafuate mapendekezo yake au kamati yake kwa sababu at the end of the day credits zote zitakuwa za CCM...

sasa angallia wewe mwenyewe tayari umeshindwa kuwapa CDM credits pale walipostahili ktk swala la kupanda kwa bei kwa bidhaa kama sukari, swala la Dowans kwa sababu umepima tu gharama ya manunuzi bila kufahamu kwamba wizi ni wizi tu mtambo wa Dowans ni ushahidi wa Ufisadi ambao hatuwezi kuupokea kwa sababu ni rahisi kuliko IPTL.. Ukienda Kariakoo utauziwa Laptop kwa Tsh, 150,000 haina maana ni hekima kukunua Laptop hizo kuliko halali za dukani ukipuuza hoja zinazohoji uhalai wa mali hiyo...Zaidi ya hapo CDM haijasita hata siku moja kuendelea kuhoji swala la IPTL ingawa serikali imeliweka kando na haitaki kabisa kulizungumzia... Wape kura yako CDM utayaona mengi ambayo hukutegemea..

Hili la kuuza hisa za NBC na airtel ktk soko letu la DSE ni zuri sana lakini sii kwa utawala wa huu CCM kwa sababu itabidi sheria na restriction nyingi sana ziwekwe kuzuia Ufisadi (kama alivyo suggest Mwanakijiji kuhusiana na Tanesco) na hata kuharibu kabisa maana ya wallstreet. Na nitazidi kusema kwamba Tanzania itaweza tu kufanikiwa ikiwa CCM itaondolewa madarakani na watu kama kina Zitto wapate nguvu na mamlaka ya kutekeleza vision zao pasipo vikwazo na mitilinga ya Mafisadi ambao watahakikisha kwa kila hali na mali wanaendelea kushika asilimia 80 ya uchumi wa Tanzania.
 
Nimemuelewa zitto lakini kama walivyoainisha wengi, anahitaji kutolea maelezo zaidi juu ya suala la IPO. Hivyo basi namsubiri atoe ufafanuzi zaidi kwanza.

Kwa sasa ningependa kujibu maswali makuu mawili: Kwanza, kuna mtu aliniuliza natumia vipi nafasi yangu ndani ya CCM kutoa mawazo yangu? Wa pili akaniuliza nina mawazo gani juu ya utatuzi wa hali ya sasa – bei za vyakula na nishati? Kwa swali la kwanza - kama unaulizia katika mazingira ya sera kitaifa, kwa kweli sina nafasi yoyote ndani ya chama zaidi ya kuwa mwanachama tu wa kawaida. Inawezekana ni kweli alichosema Doctor Kitila na wengineo kwamba mawazo kama yangu hayana nafasi ndani ya CCM, lakini ningependa kuamini sivyo kwani vijana kama Nape wamepitia hayo na sasa wanasikilizwa. Vinginevyo, kama nimevyokwisha ainisha, Falsafa yangu ni Tanzania Kwanza, Siasa baadae, CCM sio msingi wa kunipa jukwaa kutoa mawazo yangu. Nikipata nafasi hiyo, sawa, nisipopata, kuna maeneo mengine kama jamii forums, kwenye NGO sector na kadhalika ambako huwa tunakaa na kujadili masuala muhimu kama haya. Vinginevyo nadhani mnakubaliana name kwamba mchango wa dhati hauitaji uwe na cheo CCM. JamiiForums mbona tosha? Pakubwa hapa!

Nirudi kwenye mada. Ningependa kuzungumzia suala la Food and Fuel Prices. Kwanza nadhani ni muhimu sana kuliangalia tatizo hili tokea kwenye shina lake kabla ya kupendekeza ufumbuzi.


  1. Nini Kinatokea hivi sasa?
First of all, commodity price boom ni suala lililopo world wide at present. Pace hii ilianza shika kasi in the late 2007, na iliendana na turmoil in the global financial markets pamoja na sluggish economic growth katika nchi zilizoendelea. According to the IMF, kwa wastani, commodity prices have risen by almost 45% since 2006 (see IMF Commodity Price Index). Tutambue kwamba many commodity prices have reached a record high in real terms, most notable zikiwa ni Oil, Corn, Wheat and Soyabeans. The soar up price was led by major food crops (corn, wheat, edible oil etc) but recently ime spread into other foods, especially rice. Ila muhimu: tutambue kwamba, price levels today are record breaking only in current terms, but in real terms, if you look at the data, the prices remain way below the levels of the late 1970s, ofcourse with the exception of Crude Oil.


  1. Kwanini hili tatizo linatokea?
It is simply a combination of both temporary and permanent factors. We have to be very careful not to treat it as a temporary problem with permanent solutions or permanent problem with temporary solutions bila uchambuzi because tuna mazoea na serikali yetu kutokuwa makini at times. Reasons to why tatizo la bei ya mafuta na vyakula is happening:

  • First of all, we all know kwamba the major reason to why oil prices are skyrocketing is the continuing instability in the Middle East and North Africa. The idea that the region will be unstable for a while plus revolutions replicating in many other areas makes oil producers adopt a speculative mode of production. Typical oligopoly capitalists.
  • High demand for food from emerging economies – hizi nchi zime experience growth of per capita income so their demand and food consumption habits have surged thus depleting global inventories za grain.
  • Biofuel phenomenon – demand and production of these compete with that of food i.e. it’s a substitution phenomenon taking place. At present, there is a surge in demand for corn and rapeseeds oil and it is mentioned that almost 50% of the demand for major food crops in the world are biofuel related. This is very dangerous and we have some investors snooping for biofuel land in Tanzania. Tuwaangalie kwa makini sana. This demand adds pressure on food prices in the context of demand and supply.
  • Of course pia drought plus high costs of food production inputs (fertilizers etc).
  • Financial factors – The appreciation of the US dollar decreases our purchasing power as we are net importers of food (grains). Our purchasing power decreases in the sense that, we get less and less dollars from our shillings; but also our import bill pia includes other important imports, so food imports competes with oil imports etc, thus demand for food remains high relative to supply. Ila tuseme wazi pia kwamba kuna importation ya vitu vingine by the government that are so unnecessary.havina tija kwa maskini.


  1. Implications kutokana na mfumuko huu wa bei ya petrol na chakula
In terms of balance of payments, in a way we have been able to absorb the balance BOP impact – our high earnings from exports of gold and key cash crops (tobacco, tea, coffee, cotton, cashew nuts). However, attention has to be on the terms of trade – TOT is the relative price of our imports to imports; if imports are greater than exports, the TOT are unfavorable because it implies that we have to give up more of our exports for the imports we receive. We currently face this problem i.e. trade deficit.


  1. Why should we be concerned?
For the majority of Tanzanians, food carries the largest share of their consumption. Mfano rahisi – mbeba zege (kama kazi badi zipo because hata hizi zimeanza kuwa haba) makes about T.sh 5,000/day. Akinunua chakula kwa mama ntilie baada ya kushinda na njaa asubuhi, halafu aende gengeni kupitia nyanya na dagaa watoto na mke wale, zaidi ya elf tatu is gone kwa chakula tu in a day. Elfu mbili iliyobakia ndio ya vocha ya simu, nauli ya basi, na hela ya kitumbua kwa watoto wakienda shule kesho. So it is a major concern because food expenditure exceeds other commodities by a very large margin, among the poor, urban poor in particular.
Social implications includes possible riots in urban areas might become inevitable. It wont be surprising to see people walking to work tokea kimara mpaka mjini na kurudi kwani tatizo likizidi, hata madaladala yatakuwa hayashikiki. Tuombee tu mungu ikitokea, basi maskini wasije tafsiriwa kwamba wanagoma. In Indonesia, watu walishagoma kupinga shortage of soyabeans; niger, Uganda, Ethiopia, tayari kumekuwa na riots.


  1. Possible remedies
Remedies depends on the pace of economic growth especially in china and other emerging economies (see the discussion above - about the increases GDP per capita in emerging economies and how this leads to their increased food consumption from developing countries);slowness in growth itasaidia utatuzi kwa kiasi fulani; it should be noted also that it has been projected that the decline in oil prices will be limited in the medium term because oil prices reflects not only the instability in Middle East and North Africa but also costs of oil production which are still very high. There has not been a major innovation in this area to make the production of oil more reasonable in terms of technologies…
So for countries that remain to be oil importers like Tanzania, there is no major remedy in the short and medium term;
On food prices – As we know, weather conditions ni key; also we need to increase production of food crops; we also have to reject investors coming to grab our land for biofuel production, by all means necessary. We have many energy sources (hydro, coal, wind, that) remain to be underutilized. Zitto, Wanasemaje huko serikalini juu ya hili? I heard that 5 years ago, a reputable (globally) company in hydro electricity pdn called energem was ready to invest at stiglers gorge kwa hela yao wenyewe, sio mkopo wala deni kwa serikali but akapigwa stop. Akaulizwa, umeme wa megawatts 2000 utaupeleka wapi, mbona mwingi sana because hatuna that much demand? So akawa turned down. Habari hizi za energem unaweza google. Sasa nasikia wamemruhusu mwekezaji mwingine kwenye the same project ila hana ufanisi kama energem.


  1. Policy Response
We can hardly tell the extent to which the price hike in oil and food prices are a permanent or temporary; as already noted above, we should take care and avoid using short term solutions for long term problems OR using long term solutions for short term problems. However, once determined, temporary prices increases can be mitigated by temporary targeted solutions and vice versa (i.e. permanent) holds. I suggested kwamba: the government should avoid the use of untargeted subsidies to lower domestic food prices (e.g. kutoa hela kiholela kwa jamaa jamaa wanaopataga tender ku import food); also government should avoid subsidizing farmers kiholela as a way to increase food production and supply; also avoidance of the following ni key: direct price controls; financing food production; export bans; if governments don’t avoid haya, it will further raise the world market prices); also improper handling of such it may become a disincentive to farmers; also willl fail to help the poor and will drain our resources, which are already limited.


  1. INSTEAD

Looks like this is a permanent shocks, so may require adjustment of the exchange rates or monetary policy or fiscal policies – wabunge wetu wachumi kama kina Zitto pamoja na wachumi waliopo BOT na Hazina should be lead katika hili.

Finally, I would like to say kwamba we should consider this not just as a threat but pia an opportunity. We should try to encourage expansion of domestic agricultural production by improving infrastructure, distribution and storage systems because Tanzania has a clear comparative advantage in agriculture, by very far, over most SSA countries. The government should use this opportunity to also increase competition in the food sector, come up with a stable and an effective regulatory environment; provide access to credit to farmers and remove trade barriers (free trade iwe encouraged lakini while furthering incentives for production and effective policies to protect wananchi esp waliopo mijini. If done correctly, food productivity and food supply should increase, thus lead to less pressure on food prices.
 
Finally, I would like to say kwamba we should consider this not just as a threat but pia an opportunity. We should try to encourage expansion of domestic agricultural production by improving infrastructure, distribution and storage systems because Tanzania has a clear comparative advantage in agriculture, by very far, over most SSA countries. The government should use this opportunity to also increase competition in the food sector, come up with a stable and an effective regulatory environment; provide access to credit to farmers and remove trade barriers (free trade iwe encouraged lakini while furthering incentives for production and effective policies to protect wananchi esp waliopo mijini. If done correctly, food productivity and food supply should increase, thus lead to less pressure on food prices.

Bado unazungumzia kitu ambacho kiko "out of touch" na sera za chama chako na utekeleza wa sera zenyewe. Nakuambia sasa mimi ni mkulima; potential ya kuzalisha chakula cha kulisha Tanzania na kuuza nje ni kubwa sana. Lakini kuwepo zero attention ya kilimo na kilimo kutumika kama political platform inatuacha baadhi yetu sisi local serious middle level farmers na frustration kuwa utawala tulio nao ni wakimachinga hawana dira.

Hakuna guarantee ya usambazaji wa vyakula isipokuwa kupitia kwa watu wa kati maana yake bei ya mlaji wa mwisho inaongezeka visivyo na mkulima kufaidi bei anayostahili.

Angalia Kilimo kwanza Wachuuzi wameuza power tiller fake machoni pa watawala wetu wakishabikia kwa ajili tu ya kulubuni kura. Nadhani umesikia watu wanataka kushitakiana kwa hili.

Lengo lako linaelekezwa kwa wasomi wa kiwango fulani (yaani ambao siyo kundi la uzalishaji na ukuzaji wa uchumi (production)); hao ndiyo focus ya chama chako CCM matokeo yake unayaona. Sisi wazalishaji(kwenye kilimo) ni watu wa kulubuniwa wakati wa kutafuta kura. Huo ndio ufisadi unaotuumiza zaidi. Nina maanisha kukosekana kwa mtazamo ambao unasaidia uzalishaji toka kwa mwananchi wa kawaida.

As for Zain, NBC sisi tunajua ni pesa zetu wananchi zimezamishwa na wachuuzi tuliowapa madaraka wakatuuza. Zain 40% ya hiza za serikali zinareflect nini kwenye revenue za serikali na mwananchi wa Tanzania? Hilo ni swali najiuliza mkulima sipati jibu. Ila na conclude kuwa undani wake wenye madhara kwangu kama mwananchi mnaujua nyinyi CCM. Siajabu ni mgao wenu.

Kwa kweli sielewi unachosema hapa kwa sababu hujaweza kuniweka on board. Kama Ulikuwa unaelekeza mjadala kwa kundi maalum ni bahati mbaya na sisi wakulima tumo humo. Swala sisi watu wa mashambani ni kundi lenye maslahi katika ujenzi wa uchumi imara; hamjatushirikisha kwenye sera zenu kimatendo.
 
Bado unazungumzia kitu ambacho kiko "out of touch" na sera za chama chako na utekeleza wa sera zenyewe. Nakuambia sasa mimi ni mkulima; potential ya kuzalisha chakula cha kulisha Tanzania na kuuza nje ni kubwa sana. Lakini kuwepo zero attention ya kilimo na kilimo kutumika kama political platform inatuacha baadhi yetu sisi local serious middle level farmers na frustration kuwa utawala tulio nao ni wakimachinga hawana dira.

Hakuna guarantee ya usambazaji wa vyakula isipokuwa kupitia kwa watu wa kati maana yake bei ya mlaji wa mwisho inaongezeka visivyo na mkulima kufaidi bei anayostahili.

Angalia Kilimo kwanza Wachuuzi wameuza power tiller fake machoni pa watawala wetu wakishabikia kwa ajili tu ya kulubuni kura. Nadhani umesikia watu wanataka kushitakiana kwa hili.

Lengo lako linaelekezwa kwa wasomi wa kiwango fulani (yaani ambao siyo kundi la uzalishaji na ukuzaji wa uchumi (production)); hao ndiyo focus ya chama chako CCM matokeo yake unayaona. Sisi wazalishaji(kwenye kilimo) ni watu wa kulubuniwa wakati wa kutafuta kura. Huo ndio ufisadi unaotuumiza zaidi. Nina maanisha kukosekana kwa mtazamo ambao unasaidia uzalishaji toka kwa mwananchi wa kawaida.

As for Zain, NBC sisi tunajua ni pesa zetu wananchi zimezamishwa na wachuuzi tuliowapa madaraka wakatuuza. Zain 40% ya hiza za serikali zinareflect nini kwenye revenue za serikali na mwananchi wa Tanzania? Hilo ni swali najiuliza mkulima sipati jibu. Ila na conclude kuwa undani wake wenye madhara kwangu kama mwananchi mnaujua nyinyi CCM. Siajabu ni mgao wenu.

Kwa kweli sielewi unachosema hapa kwa sababu hujaweza kuniweka on board. Kama Ulikuwa unaelekeza mjadala kwa kundi maalum ni bahati mbaya na sisi wakulima tumo humo. Swala sisi watu wa mashambani ni kundi lenye maslahi katika ujenzi wa uchumi imara; hamjatushirikisha kwenye sera zenu kimatendo.

Mkulima, ni wewe ndio nakupigania, tunapishana lugha tu. Mimi kuvaa rangi ya kijani isiwe kigezo cha moja kwa moja kwamba sikubaliani na hali yako pamoja mtazamo wako.
 
Mkulima, ni wewe ndio nakupigania, tunapishana lugha tu. Mimi kuvaa rangi ya kijani isiwe kigezo cha moja kwa moja kwamba sikubaliani na hali yako pamoja mtazamo wako.

Nashukuru sana sana ila ujue ni mkakati mfu, chama chako sera zake, mikakati yake ni ya kifasadi; mimi mkulima sina huo msingi wa kuchangia kwenye ufisadi. Ila kwa sababu hapa tunajadili ki great thinker, wewe kama wewe una role 1. Kukifahamisha chama chako kuwa kimeacha mwelekeo mzima wa uongozaji wa taifa kisiasa na kiuchumi kwa kukumbatia myopic practice za utawala ambao hauna mfano ila wa kifisadi. 2. Jaribu kujihusisha na watu wa kawaida ili ufahamu hali, mawazo na practice yao ya uchumi utagundua siyo mnayoipursue kama CCM.

Mimi najivunia ukulima hata katika mazingira magumu na matata ya CCM. Na kinaniuma sana mnapokabidhi rasilimali zetu Zain, NBC acha madini kwa kutupuuza kama watoto wasioelewa kitu; ila tunajua msukumo wenu kwenye maamuzi na utendaji wenu ni ufisadi.
 
Mchambuzi,
Mkuu wangu ni vizuri sana ukizungumzia kitu kulingana na mazingira ya Tanzania na sio kuchukua somo zima la uchumi la kuliweka hapa ili mradi kuhalalisha utawala huu mbaya.

Katika swala la mfumko wa bei sioni uhalali wowote wa kuhusiana na global economic crisis kwa sababu nchi za Kiafrika na hasa maskini hatukuwa affected sawa na nchi za magharibi isipokuwa sisi ile recession ilisababisha slowdown ktk ununuzi wa exports zetu kwa sababu demand ya mali zetu ilipungua hivyo kama tumekosa soko ina maana mali yetu ilikuwa inatakiwa ishuke bei badala ya kupanda kama tulivyoshuhudia wakati wote wa utawala wa JK.

Kwa hiyo sidhani kama ni busara kuzungumzia global economics crisis na impact zake mahala ambapo viashirio vya ongezeko la bei ya bidhaa havifanani hasa tukizingatia kwamba hakutudhulika kwa sababu hizo.. Na sikuelewi unaposema hivi:- Ila muhimu: tutambue kwamba, price levels today are record breaking only in current terms, but in real terms, if you look at the data, the prices remain way below the levels of the late 1970s, ofcourse with the exception of Crude Oil.

Hapo nilipo highlight sielewi hizo data unazozungumzia kwamba prices ya vyakula ipo chini ya miaka ya 70's una maana gani?

Mkuu wangu ktk baadhi ya maelezo yako umeorodhesha vitu vingi vilivyosababisha mfumko wa bei ya bidhaa...haya mengi hayakuwepo miaka ya 70's iweje leo useme kwamba bei zipo chini ya miaka ile wakati unajua fika kwamba nchi kama Tanzania haya maswala ya KILIMO KWANZA ndio sababu kubwa ya mfumko wa bei kwa sababu gharama zote za uzalishaji mazao yetu lazima ziwekwe ktk upangaji wa bei mpya za mazao jambo ambalo halikuwepo zamani..Binafsi nilitegemea zaidi kilimo cha kisasa kingekwenda kwa hatua.. tukitumia mbegu zetu za asili na kitakachoongezeka ni umwagiliaji badala ya kusubiri mvua lakini CCM na KILIMO KWANZA mkachagua matumizi ya mbegu za kisasa ili kuongeza mavuno ya mkulima pasipo kupima gharama na athari zake..

Kilimo cha mbegu za kisasa kinategemea sana matumizi ya vifaa ambavyo havipatikani kwa bei rahisi kama jembe la mkono, pia sii rahisi kubadilisha kilimo cha mashamba madogo kubadilika ghafla na kuwa kile cha ma settlers kwa sababu ati huko Ulaya na nchi zilizoendelea ndio zinafanya hivyo..Matrekta, mbolea, mafuta na kadhalika haya yote yanachangia mfumko wa bei ya mazao hasa pale tulipoamua kufanya hivyo ktk mazao ya chakula (food crops).

Leo hi tumepoteza kabisa mbegu zetu za asili ambazo zilikuwa vumilivu ya ukame isipokuwa mvua hazikuwa za kutosha na kilichotakiwa zaidi ni kilimo cha umwagiliaji na tumepandikiza mbegu ambazo zinahitaji mbolea sana na kama usipoweka mbolea hakuna kitakachoota.. Na kibaya zaidi ardhi iliyokwisha tumia mbolea hizi haiwezi kuotesha kitu kingine chochote pasipo matumizi ya mbolea hizi. bado pamoja na uvumilivu wake wa ukame zinahitaji maji sawa kabisa na amount ya maji mbegu zetu za asili zilihitaji sema tofauti ni muda wa kufikia kuvuna mazao haya...

Nikilikuwa dara miezi michache iliyopita nikatazama jinsi tulivyoondoka ktk ufugaji wa ng'ombe wa kiasili kwenda ng'ombe wa kizungu na hakika sikuelewa sababu haswa. Ukienda ktk Mabucha ya nyama utaambia huwa hawauzi zaidi ya nusu ng'ombe kwa siku na wakati mwingine nyama hulala, Na matumzi ya maziwa sio kwamba yameongezeka kiasi kwamba kulikuwepo na shida ya maziwa au demand ilikuwa kubwa kulio supply bali ni ile imani kwamba ng'ombe wa kizungu wana maziwa na nyama nyingi kuliko wa kienyeji wakati huohuo soko kubwa lililopo nchini ni nyama na maziwa ya ngo'mbe wa kiasili.. sasa tunafanya hivi ili tufikie kitu gani haswa kaa sii kufuata matakwa ya wazungu..

Nimeyasema haya siku nyingi sana na kama nakumbuka hata mh.Mwandosya akiwa waziri wa kilimo ( correct me if I'm wrong) awaliwahi kusema Tanzania hatupo tayari kuanzisha kilimo cha kisasa kwa njia ya kutumia mbegu za kisasa lakini tumekuja wasikia kina Kofi Anan wenye kufanya kazi zao kwa interest za nchi za magharibi leo bei hata ya sukari imepanda na tunashindwa kuirudisha chini..

Na nitahitimisha hili la Kilimo kwanza kwa kusema makosa yaliyofanyika yatakuwa na impact kubwa sana kwetu kama ilivyotokea kwa samaki sangara ziwa nyanza (victoria) kiasi kwamba tumepoteza samaki wa asili (wameliwa na sangara) na wachache waliobakia tunashindwa kumudu bebi zake.. halafu sangara nao wanakwisha mwisho wa siku Ziwa Victoria litabakia ziwa lililokufa (dead lake)..

Labda nikuunge mkono zaidi ktk swala la Trade deficit ambapo kwa miaka mingi tumekuwa tunashindwa kulitazma zaidi. Tanzania ya leo imekuwa nchi ya imports zaidi ya exports na kwa bahati mbaya hata Utajiri Mungu alotupa tunaugawa nje kwa Maifsadi.. mfano tazama mkataba wa Barricks, sasa ukichukulia uchumi wa puto utafikiri kwamba Tanzania inafaidika sana na mauzo ya dhahabu lakini ukweli ni kwamba hatupati kitu..Huu ni uchumi hewa ambao Nyerere aliukataa na wala sii jadi yetu kabisa..Wabongo kwa asili wanaamini zaidi into Liquid market na ndio biashara yetu miaka yote..fedha iliyopo mfukoni itanunua mali inayohitajika with minimum loss of value...kuliko biashara ya tombola ambayo huna hakika ya market kesho na ndio maana tunashindwa hata kuweka fedha benki au hata kununua hisa DSE..

Hivi nikuulize wewe uliyeko CCM, tumeshindwa nini kufanya kilimo kwanza kiwe focussed on Cash crops?..Nchi kubwa yenye ardhi ya kilimo isiyokuwa na kipimo kwa nini tusianzishe mashamba mapya ya mazao ambayo yana soko nje, tuanzishe viwanda vinavyosindika mazao hayo kama wajarumani na waingereza walivyoanzisha Pamba, kahawa, katani na kadhalika badala yake tumeingia ukulima wa mahindi, mpunga, miwa na vitu ambavyo kiasili vilihitaji tu maji kutosheleza mahitaji yetu na hasa tukizingatia kwamba sisi tuna wakulima wadogowadogo wenye mashamba madogo ambayo hayakuhitaji mfumo tulochukua?..

To be specific, The high levels of liquidity had not stressed out any major impact on our financial system. In fact, hao wanaoitwa Wajisiriamali wametokana na mfumo huu wa kibiashara zaidi kwani hutengeneza vitu kulingana na soko na kuviauza chapuchapu.. wenyewe wanasema biashara ya kuzungusha..However, local banks zetu zinztoa fedha na wanachukua risk kubwa sana, na pengine naweza kusema impact iliyotokana na global economic crisis ktk banking system imetugharimu tu kwamba hizi bank zetu zina share ownership na Bank za nje kwa hiyo hiyo bank za nje zinapo suffer capital constraints kitu cha kwanza huondoa capital zao ktk benki ndogo kama zetu na hapo ndio unaona kuyumba kwa mikopo na benki zetu lakini bado ukitazama kwa makini hizi benki zetu zinatengeneza fedha (faida) kubwa sana ku operate kwetu kutokana na interest kuwa wanazo charge kwa gharama ndogo sana ya matumizi..

Mkuu, Tanzania is Heaven of business world, ikiwa tutapata utawala bora (viongozi) wenye kutambua jinsi Mungu alivyotujaalia utajiri mkubwa na kinachotakiwa ni matumizi mazuri ya mwongozo, itikadi na sera nzuri kulingana na mazingira yetu..Ufisadi ni haramu na hata siku moja hatuwezi kuendelea kwa kufuata mrengo wowote ikiwa Ufisadi ni sawa na tobo ktk pakacha la mfuko wa Taifa. No matter how fast, careful, energy mtakayoweka hatuwezi kulijaza pakacha linalovuja.. Tuzibe kwanza pakacha na ndio maana namsifia sana Dr.Slaa ktk hili kwani hata kwa kutumia logic hivi kweli unaweza kuijaza ndoo maji ikiwa imetoboka?.. je ni muhimu kuziba tobo kwanza au kutafuta mbinu za kuijaza hiyo ndoo pasipo kuziba hizo tobo..
Watanzania tena wasomi kwa hesabu kubwa wanafikiria zipo mbinu za kuijaza ndoo bila kuziba tobo na ndio haya tunayoyaona kila siku yakiendelea hali nchi inazidi kudidimia ktk umaskini...Still never learned a thang!
 
Mimi nina swali kwenu wataalaum wa uchumi. au yeyote mweny jibu lisilo la kisiasa.

Wekeni siasa na maneno ya wanasia pembeni. Uchumi wa Tanzania unategemea nini.?????

Nauliza swali hili sababu nimesoma

  • nchi kama UK ni finacial econony
  • Nchi kama Ujemarumani na Japan ni manufactiring economy
  • USA nadhani ni mchaganyiko wa Fiance na manufactiring.
  • China inakuja juu sababu ya manufacturing
Je tanzania uti wa mgongo wa uchumi wetu wake ni nini ? Not politics please.

  • agricultural.
  • Mining
  • Tourism
  • manufacturing
  • Small and Medium Enteprse
  • Finance
 
Mimi nina swali kwenu wataalaum wa uchumi. au yeyote mweny jibu lisilo la kisiasa.

Wekeni siasa na maneno ya wanasia pembeni. Uchumi wa Tanzania unategemea nini.?????

Nauliza swali hili sababu nimesoma

  • nchi kama UK ni finacial econony
  • Nchi kama Ujemarumani na Japan ni manufactiring economy
  • USA nadhani ni mchaganyiko wa Fiance na manufactiring.
  • China inakuja juu sababu ya manufacturing
Je tanzania uti wa mgongo wa uchumi wetu wake ni nini ? Not politics please.

  • agricultural.
  • Mining
  • Tourism
  • manufacturing
  • Small and Medium Enteprse
  • Finance
Mimi nadhani ilitakiwa iwe KILIMO lakini tumekifanya kilimo kwanza kukidhi mahitaji yetu. Na tunategemea kudra ya Mwenyezi Mungu atatupa Utajiri gani zaidi pengine mafuta, maanake dhahabu na madini mengine tumepewa tumeyagawa..
Kazi kwako!
 
Nimemuelewa zitto lakini kama walivyoainisha wengi, anahitaji kutolea maelezo zaidi juu ya suala la IPO. Hivyo basi namsubiri atoe ufafanuzi zaidi kwanza.

Kwa sasa ningependa kujibu maswali makuu mawili: Kwanza, kuna mtu aliniuliza natumia vipi nafasi yangu ndani ya CCM kutoa mawazo yangu? Wa pili akaniuliza nina mawazo gani juu ya utatuzi wa hali ya sasa – bei za vyakula na nishati? Kwa swali la kwanza - kama unaulizia katika mazingira ya sera kitaifa, kwa kweli sina nafasi yoyote ndani ya chama zaidi ya kuwa mwanachama tu wa kawaida. Inawezekana ni kweli alichosema Doctor Kitila na wengineo kwamba mawazo kama yangu hayana nafasi ndani ya CCM, lakini ningependa kuamini sivyo kwani vijana kama Nape wamepitia hayo na sasa wanasikilizwa. Vinginevyo, kama nimevyokwisha ainisha, Falsafa yangu ni Tanzania Kwanza, Siasa baadae, CCM sio msingi wa kunipa jukwaa kutoa mawazo yangu. Nikipata nafasi hiyo, sawa, nisipopata, kuna maeneo mengine kama jamii forums, kwenye NGO sector na kadhalika ambako huwa tunakaa na kujadili masuala muhimu kama haya. Vinginevyo nadhani mnakubaliana name kwamba mchango wa dhati hauitaji uwe na cheo CCM. JamiiForums mbona tosha? Pakubwa hapa!.............

Mkuu nimeelewa hoja zako lakini nadhani hapa vijana wengi na wataka mabadilio wengi ndipo tunapokosea . hatutumii nji za kiofisi kupeleka maoni yetu. Maoni haya uliyoandika jf ni mazuri but what if ungewalk a mile furher just ungeandika offficialy ushauri wako kwa chama iwe ni ngazi ya taifa au mkoa. eg YAH HALI YA UCHUMI.

At least wewe zaidi ya mwanauchumi ni mwanasiasa wengine tunakomaa na jf sababu kazi zetu zinatubana na sio wanasiasa. Hatuna altenative zaidi ya kuandika hapa Leo hii siwezi kunadika barua CCM au Chadema mkoa au taifa sababu kwanza si mwannachama. hata ikiandika nadhani itaweka kwennye bin sababu sina jina. Wewe uko tfauti unaweza kusikilzwa.

Mimi nakushauri katika observation zako japo kichama hauna rank kubwa document your ideas and submit them officialy ili hata in the future zinaweza kutumika kama reference.

Mawazo Uliyonayo mazuri ukichanganya na mengineyo ya hapa ya wana JF wewe unaweza kuwa daraja. Am telling you kuna mambo mengi watu tunaandika hapa ni manufaa kwa taifa lakini hakuna kichaofanyika. Lakini kuna watu fulani hatutuoi ushauri kwa hao viongozi na wengi wao waaotakiwa kuyaona na kuwapa ushauri wazee ni sisi vijana amabao tunafanya kosa la kusubiri mawazo ya wakubwa.

Mi nadhani ushauri wako usipofanyiwa kazi sio weakness. alafu elwa kuna tofauti ya kuandika JF na kuandika CCM mkoa au taifa. Wich one if official? Wich one can be refered ?

But simaanishi eti usiandike jf nimejifunza mengi kwenye article yako na am looking to learn more.

So boss walk mile further and try to press some button on your side too nakuomba usiishie tu jf mkuu uwe unawatumia docs kitaalam pale chamani. U never know

Tanzania kwanza siasa baadae.

 
Mimi nina swali kwenu wataalaum wa uchumi. au yeyote mweny jibu lisilo la kisiasa.

Wekeni siasa na maneno ya wanasia pembeni. Uchumi wa Tanzania unategemea nini.?????

Nauliza swali hili sababu nimesoma


  • nchi kama UK ni finacial econony
  • Nchi kama Ujemarumani na Japan ni manufactiring economy
  • USA nadhani ni mchaganyiko wa Fiance na manufactiring.
  • China inakuja juu sababu ya manufacturing

Je tanzania uti wa mgongo wa uchumi wetu wake ni nini ? Not politics please.


  • agricultural.
  • Mining
  • Tourism
  • manufacturing
  • Small and Medium Enteprse
  • Finance

Unaendshwa KIMJINIMJINI
 
Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.
Nimefuatilia through media nini kilichosemwa Sumbawanga na Mbeya! Nawapongeza kwa kazi nzuri na kwa kujaribu kuwafikia wananchi! Anachowagombeza JK watendaji wake kuwa "Waende kwa wananchi kusikiliza matatizo yao" ni "cut and paste" ya kutoka kwenu! CCM wameona sasa CDM imetufikia na tunajisikia huru kuwasilisha kero zetu kwa serikali kivuli kuliko serikali ya mafisadi....Honereni kwa hilo, lakini tusibweteke!
...Kwa hoja ya DSE na serikali kuuza hisa zake nakubaliana nayo, lakini who cotrol DSE? Mwananchi wa kawaida atanufaikaje? SIyo kama ni walewale wachache watafaidika? Mimi bado na-admire sana uchumi kuwa unamilikiwa na umma! Najua kwa zama hizi hii inaonekana ni old fashion lakini still umma unaweza kuwa na say katika uchumi....how can we do that? Sera ya CDM inasemaje katika hili?
 
Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.
Mheshimiwa hapo ndipo pa kuweka sawa kwani wengi wakisikia kuuza wanalenga moja kwa moja kuwauzia wageni.

Nashukuru umeliweka sawa hili kabla lilinipa presha.
 
Back
Top Bottom