Mheshimiwa Msechu unastahili pongezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Msechu unastahili pongezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by I have a dream, Jul 4, 2012.

 1. I have a dream

  I have a dream Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimekuwa nikitafakari kazi anazofanya mweshimiwa mchechu ni nzuri sana na anastahili pongezi.

  Tangu amekuwa mkurugenzi wa NHC ni mengi amefanya kuanzia na utawala na hatimaye upatikanaji wa makazi bora kwa watanzania. Upatikanaji wa makazi bora unapitia mchakato mrefu sana lakini at the end ameweza kufanikisha to some extent. Ana maamuzi ya busara na ya kutokuogopa( RISK TAKER) na ni smart. Hasiti kumpa mtu nafasi ya kuonyesha ujuzi wake professionally. Hii ndiyo siri ya mafanikio. Mimi mwenyewe nilipata nafasi ya kufanya naye kazi eventhough siko kikazi NHC.

  Pia natoa pongezi kwa viongozi kumwamini na kumchagua

  Wito wangu ni kwa sister organisations kumuunga mkono mia kwa mia mfano tanesco, maji, tanroad, TBA na nyinginezo ili kurahisisha utekelezaji wa project alizoazisha na anazoplan kufanya. Hatimaye na mimi nitaweza kupata nyumba inayomilikiwa na NHC.

  Marafiki zangu mnaofanya kazi NHC Juhudi zisipungue

  Wito wangu kwa JF panapostahili kusifiwa ni vizuri tukasifia: HONGERA SANA MH.MCHECHU KWA KAZI NZURI
   
 2. piper

  piper JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa mui muue haki yake mpe, huyu bwana ni jembe la maana bali serikali hii ya magamba isivyopenda wachapakazi lazima apigwe zengwe ili aondolewe, rejea lilomkuta Tido TBC
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hivi mnapomsifu huyu Jamaa kila siku amefanya nini hasa? Mbona mi naona project zake zinakidhana sana na mahitaji ya watanzania wa kawaida? nyumba za mchikichini nasikia bei ni zaidi ya Millioni mia moja hamsini, kuna mfanyakazi atanunua apo?
   
 4. I have a dream

  I have a dream Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Unachosema Inaweza kuwa na ukweli lakini ukianza project yoyote inabidi ujitahidi urudishe kwanza madeni then unaanza kujenga nyumba ambazo zinabei nafuu
   
 5. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ingawaje hii si hoja lakini kwa mshahara anaovuta kwa mwezi i.e mara 20 ya mshahara wa daktari wa sasa (Tshs 970,000), inabidi achacharike.
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mtu ukianza kula nyama za watu utakula mpaka watoto wako mwenyewe, huyu akimaliza hizo project zake za makazi ya watu ataanza kujenga za maofisi na mahoteli.

  Kitu kimoja watu wanashindwa kukumbuka ni kwamba, Mchechu kapata ukurugenzi NHC sababu ya success yake katika kufinance real estates hapa mjini very profitably akiwa na CBA. anachokijua ni profitability basi na ndio maana unamuona atafuta sifa kwa kutoomba fedha serikalini ili kuwezesha ujengaji wa nyumba nafuu kwa watanzania wakawaida, mtafute akiwa anaongelea haya mambo ndio utamuelewa ni mtu wa namna gani. Hauwezi kukopa pesa Bank alafu ukafanya project za Kisiasa.

  NHC inatakiwa kutumika kisiasa, kwa maana ya kuwasaidia watanzania ambao hawawezi kuhimili uchumi wa soko huria, not less than that. Lakini kwa sababu serikali yetu inaongozwa bira sera wa dira zinazoeleweka ipo siku utasikia yuko board ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu
   
 7. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nilishawahi kuchangia humu jamvini kuna teknolojia ya matofali hydroform na interlocking blocks ni nafuu sana hasa kwa wananchi wa kawaida na mtu anaweza kumudu kutumia matofali hayo kwa shughuli za ujenzi kama NHC ingeweza kuingiza teknolojia hiyo katika ujenzi wa nyumba zake nauhakika gharama zingekuwa chini na nyumba hizo zingeuzwa kwa bei nafuu sana
   
 8. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  I have a dream,

  Tendo la kumsifia ndani ya JF ya 2012 Mtanzania mwenzio kwa mema au mafanikio aliyosotea na kuyapata ni kusaka matusi na kejeli.

  Pamoja na hayo, ukweli unabaki kuwa ukweli; Nehemia anafanya kazi na kutoa matokeo yenye mafanikio ya hali ya juu. Ni rahisi kwa kipofu kushuhudia hili kuliko baadhi ya wana-JF
   
 9. +255

  +255 JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,910
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Mnamsifia mtu kwa kutimiza majukumu yake...Af hizo nyumba kuna mtu mwenye kipato chawaida alishawahi kununua?
   
 10. s

  spiritual-thinker Senior Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Sio kila mshahara lazima ulinganishwe na wa daktari, Mchechu ni Director General na mshahara unaotaja ni wa daktari anayeanza, hv ni vitu viwili tofauti. Linganisha mshahara Mchechu na CEO wa Vodacom, NMB au at least Dr. Njelekela(Director wa MNH)
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Waliopo ndani ya NHC wanasema Mchechu amejitengenezea anguko lake kwa kuwagawa wafanyakazi. Wafanyakazi wa zamani kulipwa mishahara kiduchu huku wapya na ambao wengi wanapata ajira za memo wakilipwa mishahara mikubwa. Tatizo jingine linadaiwa ni menejimenti kubwa ambayo inatumia pesa nyingi bila sababu za msingi. Kama atataka kupata mafanikio hanabudi kurekebisha hayo mambo pamoja na kumdhibiti mkurugenzi wake wa branch operations ambaye anadaiwa kuwa ni mchwa hatari kote alikopita!
   
 12. s

  spiritual-thinker Senior Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Watanzania huwa wananishangaza sana, wapo wanao onekana kupenda maendeleo kwa maneno lakini anapotokea mtu anayetekeleza mipango ya maendeleo kwa vitendo wanapiga mayowe. Mchechu ni katika majembe machache sana yaliyo kwenye mashirika ya umma chini ya serikali ya magamba. Hili shirika lilikuwa linakufa kama asingetokea Dr. Magufuli kuliokoa ile mwaka 2006. Hata hivyo halikuwa na kiongozi visionary na chapa kazi kama Mchechu.

  Huna aibu kusema anatafuta sifa kwa kutoomba fedha serikalini???!!! Hivi akianza kutegemea fedha kutoka kwenye serikali hii dhaifu ya magamba kuna mradi hata mmoja utakaofanikiwa!! hawawezi kununua CT scan, watajenga nyumba??? Ndugu yangu use the white matter in your skull.

  Eti, amezoea profitability!!! Unataka aliongoze shirika kwa hasara ili muuziane kama mlivyozoea kufanya kwa kisingizio cha hasara??!!

  All in All Mchechu is a rare gem. Jembe lingine la kwenye shirika la umma ni new CEO wa Posta Bank Mr. Moshingi, ndani ya mwaka wake mmoja ofisini, profit growth 300 perc. Bravo!! this is what we want.
   
 13. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sawa ila nataka tu kujua kuwa ni lini huyu bwana amepata status ya kisiasa kuitwa mheshimiwa?
   
 14. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kumbe na yeye ni Mheshimwa??
   
 15. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Disgusting. Orodhesha hayo mafanikio unayosema kwa Watanzania. NHC inapaswa kujenga low cost housing nyiiingi ziwanufaishe Watz wengi. Sasa mill 150 si za matajiri na process ya kuziuza ni rushwa tupu? Hamna issue. Atimize malengo ya NHC kwa walengwa sio kubabaisha kwenye TV na yule jamaa wa Clouds as if kuna chochote tunachofaidi kwenye hivyo vipindi.
   
 16. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Tatizo la walamba viatu na kujipendekeza. Anayeonyesha mapungufu ama udhaifu ndiye anamsaidia Mchechu kurekebisha makosa ili afanikiwe zaidi. Binadamu wote tuna udhaifu wa aina mbalimbali,rafiki mwema ni yule anayekutahadharisha siyo anayekusifu sifa za kinafiki!
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa kukusaidia ili kupima perfomance ya mkuregenzi wa NHC unaangalia yafuatayo

  a. Nyumba ngapi zimejengwa na kukodishwa au kuuzwa kwa wananchi wa kawaida???

  b. Nyumba ngapi zimekarabatiwa vema na kuondoa nepotism/upendeleo katika upatikanaje wake..hadi leo wenye kupewa nyumba za NHC ni wahindi na waafrika wachache kwanini (operation morandi ni ileile) ambayo mtu wa kawaida kupata nyumba ni haiwezekani

  c. Wafanyakazi wake wanalipwa vema, wameacha kula rushwa, utaratibu wa ajira uko wazi kwa watanzania wote au ni kwa wale wanajumuia wenzake tu??


  Hizo tatu zote kama hujaona chochote usituletee ujinga wako kwasababu amekupa kazi, au amekununulia pombe ..
   
 18. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Jamani kuleta mabaadiliko serikalini si kitu rahisi kwani utaratibu wa serikali ni business as usual so unapoona hata dalili za mabadiliko ujue mtu kafanya kazi. Nehemia amejitahidi sana kwenye shirika hili na kigingi moja wapo ni kuwa serikali na hasa wajeda aka wanajeshi wanagoma kulipa kodi za pango japo budget wanatengewa. Nehemia awafanyaje JWTZ? Wakilipa wadaiwa sugu wote hapo atakuwa na fungu la kujenga na hizo nyumba za akina sisi. meanwhile lazima aoparate on business basis otherwise ataanguka puuu. Hongera Nehemia unajitahidi.
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  ni bahati mbaya sana namna nilivyoandika ni rahisi kuonekana namshambulia mchechu, hata mimi namkubari lakini umenielewa niliposema NHC inatakiwa kuendeshwa kisiasa?
   
 20. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  You may be right but missing some points. Shirika la Nyumba la Taifa si sawa na benki binafsi eg. CBA. For one thing, NHC ni shirika la umma. Lengo lake si kuingizia serikali mapato. Bali ni kutoa huduma kwa watanzania. Yes. Linapaswa kujiendesha kwa faida lakini lengo kuu si profit maximization. Unapoendesha shirika hili, ambalo waasisi wake walilenga watu wenye kipato cha kawaida, kama benki ya biashara unakuwa unaongozwa na malengo ya kutengeneza faida kubwa ili usifiwe (Kama unavyomsifia Bosi wa Posta) na kuwasahau walengwa ambao ni Watanzania wa kipato cha kawaida. Huyu Bwana amelichukua Shirika likiwa halina uwezo wa kifedha (so they say). Hivyo, akaamua kuja na style ya kujenga nyumba kwenye "prime plots" za shirika hili na kuziuza ili kujenga uwezo wa kifedha (ninaambiwa hata mtumishi wa NHC ni shughuli kupata nafasi ya kuuziwa nyumba hizo, if you know what I mean). Fine. Uwezo wa kifedha utaongezeka (if it works) lakini asset za shirika zitapungua. Kupungua kwa assets za shirika kunapelekea kufa kwa shirika, regardless of how much money you have at hand. Na kumbuka kutengeneza faida kubwa si lengo la shirika.

  Lengo la shirika ni kuwapatia Watanzania makazi bora kwa gharama nafuu. Kabla ya huyu bosi kuongoza Shirika na inavyofanyika nchi nyingine, Shirika hili linapaswa kujenga makazi bora ya gharama nafuu na kuendesha renting business. Watanzania walio wengi watamudu kulipa gharama ya pango kila mwezi lakini hawawezi kumudu kulipa Shilingi 100 million kwa mkupuo. Hawakopesheki. Hii itaondoa matatizo mengi sana. Itapunguza rushwa. Itaongeza ufanisi wa kazi. Badala ya mfanyakazi kufikiria namna ya kuiba ili aweze kujenga nyumba au kununua nyumba ya NHC, atatulia na kufanya kazi. Kwa sababu uhakika wa makazi anao. Na usipolipa pango kwa mwezi, unatolewa anapewa mtu mwingine. This is how it should work. NHC isishindane na mabenki kutengeneza faida kubwa. Hili ni shirika la umma. Lilenge kutoa huduma zaidi. And yes. Linastahili ruzuku ya serikali at some point (economists hate subsidy arguing it's an inefficient way to allocate resources. But who doesn't do it?).

  Na NHC ikifanya kazi yake vizuri, gharama ya pango inayotozwa sokoni kwa sasa itaji-regulate vizuri sana. Kwa sasa wenye nyumba wanatoza bei yeyote wanayotaka. Hakuna wa kumuuliza. Na kwa kuwa kuna shida ya makazi, watu wanaishia kuiba ili kumudu gharama za pango. Mishahara haiendani na gharama za pango sokoni. Watu wanamudu vipi kulipa kama si kwa kuiba?

  Bw. Mchechu, NHC ni mkombozi wa Watanzania linapokuja swala la makazi.Jitahidi kuhudumia Watanzania wenye mahitaji na si matajiri wanaotafuta kujilimbikizia mali. Kwa kuuza maeneo mazuri ya NHC, huna tofauti na wale waliojiuzia nyumba za Serikali. We are counting on you!
   
Loading...