You may be right but missing some points. Shirika la Nyumba la Taifa si sawa na benki binafsi eg. CBA. For one thing, NHC ni shirika la umma. Lengo lake si kuingizia serikali mapato. Bali ni kutoa huduma kwa watanzania. Yes. Linapaswa kujiendesha kwa faida lakini lengo kuu si profit maximization. Unapoendesha shirika hili, ambalo waasisi wake walilenga watu wenye kipato cha kawaida, kama benki ya biashara unakuwa unaongozwa na malengo ya kutengeneza faida kubwa ili usifiwe (Kama unavyomsifia Bosi wa Posta) na kuwasahau walengwa ambao ni Watanzania wa kipato cha kawaida. Huyu Bwana amelichukua Shirika likiwa halina uwezo wa kifedha (so they say). Hivyo, akaamua kuja na style ya kujenga nyumba kwenye "prime plots" za shirika hili na kuziuza ili kujenga uwezo wa kifedha (ninaambiwa hata mtumishi wa NHC ni shughuli kupata nafasi ya kuuziwa nyumba hizo, if you know what I mean). Fine. Uwezo wa kifedha utaongezeka (if it works) lakini asset za shirika zitapungua. Kupungua kwa assets za shirika kunapelekea kufa kwa shirika, regardless of how much money you have at hand. Na kumbuka kutengeneza faida kubwa si lengo la shirika.
Lengo la shirika ni kuwapatia Watanzania makazi bora kwa gharama nafuu. Kabla ya huyu bosi kuongoza Shirika na inavyofanyika nchi nyingine, Shirika hili linapaswa kujenga makazi bora ya gharama nafuu na kuendesha renting business. Watanzania walio wengi watamudu kulipa gharama ya pango kila mwezi lakini hawawezi kumudu kulipa Shilingi 100 million kwa mkupuo. Hawakopesheki. Hii itaondoa matatizo mengi sana. Itapunguza rushwa. Itaongeza ufanisi wa kazi. Badala ya mfanyakazi kufikiria namna ya kuiba ili aweze kujenga nyumba au kununua nyumba ya NHC, atatulia na kufanya kazi. Kwa sababu uhakika wa makazi anao. Na usipolipa pango kwa mwezi, unatolewa anapewa mtu mwingine. This is how it should work. NHC isishindane na mabenki kutengeneza faida kubwa. Hili ni shirika la umma. Lilenge kutoa huduma zaidi. And yes. Linastahili ruzuku ya serikali at some point (economists hate subsidy arguing it's an inefficient way to allocate resources. But who doesn't do it?).
Na NHC ikifanya kazi yake vizuri, gharama ya pango inayotozwa sokoni kwa sasa itaji-regulate vizuri sana. Kwa sasa wenye nyumba wanatoza bei yeyote wanayotaka. Hakuna wa kumuuliza. Na kwa kuwa kuna shida ya makazi, watu wanaishia kuiba ili kumudu gharama za pango. Mishahara haiendani na gharama za pango sokoni. Watu wanamudu vipi kulipa kama si kwa kuiba?
Bw. Mchechu, NHC ni mkombozi wa Watanzania linapokuja swala la makazi.Jitahidi kuhudumia Watanzania wenye mahitaji na si matajiri wanaotafuta kujilimbikizia mali. Kwa kuuza maeneo mazuri ya NHC, huna tofauti na wale waliojiuzia nyumba za Serikali. We are counting on you!