Ukitaka kujua uozo wa NHC kaulize wafanyakazi wake! Wengi wamekata tamaa na Mchechu amebadilisha Malengo ya awali ya Shirika! Leo shirika la nyumba la taifa halina tena hadhi ya Utaifa, ni kama Taasisi binafsi ya kibiashara! Mchechu aliahidi Kujenga Nyumba 15000, Muulize leo hii ameshajenga Nyumba ngapi?? Leo hii shirika lina Engineer mmoja tu, ambaye kwa stress ambazo alizipata alitaka kuacha kazi mwaka jana, akabembelezwa kwa kuwa tu yeye ndiye pekee ana muhuri unaokubaliwa kuidhinisha miradi mikubwa!! Kuna wazee wana matatizo ya kiafya ila Mchechu awehamishia kwenye remote areas kama Bukoba, shinyanga, singida Lindi na kwennengineko, ambapo kwa mahitaji yao matibabu wanatumia pesa nyingi na muda mwingi kwenda Dar esalaam kwa matibabu yao! Kaulize viwanja vya NHC walioziwa Wakubwa kwa bei chee! Utalia! NHC sio kwa watanzania wa kawaida tena!!