Kinachosikitisha na kwa serikali kuamini katika kusema uongo na kudharau wananchi kwa kiwango cha hali ya juu
Dr Mrisho Jakaya Kikwete ni raisi aiyekubuhu kwa kusema uongo asiye hata na chembe moja ya uoga,haheshimu kabisa wananchi wake,ni mjivuni na mropokaji haijapita hata miezi miwili aliposema yeye sio mvua kwa hiyo hawezi kujaza mabwawa lakini alipokua anasaini ununuzi wa IPTL miongo miwili iliyopita hakujua kwamba mabwawa hayatoshi tena bali angeweza kupanga mpango wakutengeneza mabwawa mengine ya kuvuna maji
Amemuambukiza Waziri wake MKuu Mh.Mizengo Kayanda Peter Pinda,huyu ndio hovyo na muongo sana ,anakisilani anadharau hata wabunge wanaowakilisha wananchi kwa kuwajibu majibu ya mkato yasiyojitosheleza,hakuna analofanya zaidi ya kuzungusha mikono akihitaji huruma ya wananchi karibu miaka minne yuko madarakani,amengia kukiwa na tatizo kubwa la uemem nchi ikiwa gizani hadi leo amebaki kutuambia wananchi tumuelewe utamuelewa mtu asiye adilifu,aliyelewa madaraka asiyemfikiria mwananchi
Waziri Ngeleja kafundishwa uongo mpaka amehitimu kuwa mwongo nambari one asiye na tone moja la aibu kazi kuzungusha macho akitunga uongo kugeuza watanzania mafara,mwishoni mwa mwaka jana pale ubungo alisema ikifika machi mwaka huu tatizo la umeme ingekuwa historia,hatujakaa sawa mwezi machi akasema mitambo itaingia mei na hakutakuwa na shida tena ,sasa anasema mwishoni mwa mweezi wa Agusti,aibu na haiwezekani kuwa na viongozi wasio waadilifu wanadharau wananchi,waongo,wala rushwa,ten parcent hizo ,kila mtu ajifikirie alipo jee hawa watu waongo waendelee kuwa na dhamana yetu mpaka baada ya miaka minne ijayo hilo haliwezekani
Mtanzania amka sasa hakuna wa kukuinua wewe mwenyewe amua sasa kataa hawa viongozi waongo waliokosa heshima