Kelele zilizopigwa zimetosha sana, na sasa hivi zimezoeleka sana na kwa yote mpaka tulipofika, sasa hivi watanzania tunatabilika sana, ndiyo maana huoni dalili ya respond yeyote ile, I trust no Politician, iliyobaki kwa sasa tujipigania, tuna silaha za kutosha sana, nazo ni kama zifuatazo, vijana wasio na ajira, wananchi waliodhurumiwa (mambo mbalimbali) na sheria ikashindwa kuwapigania, watu wenye vinyongo, na wale ambao wanahisi mapambano haya yatawasidia, pamoja na wataalumu katika nyanja mbalimbali ambao wanauhisi uchungu huu wa watu kudhurumiwa bila ukomo.
Ni furaha yangu kama serikali yetu itabadilika na kuwa na sifa zifuatazo....yaani usikivu na uwajibikaji na kutovumilia uzembe, ufisadi wala kutokuwa na rafiki wa kudumu pale maslahi ta taifa yanapoingiliwa.
Ni sisi wenye jukumu la kuiweka madarakani serikali lakini bahati mbaya sana ni kuwa katika kutafuta fursa wenzetu wanakuwa na ajenda mbili, moja ya kuombea ridhaa, nyingine na kubwa kwa ni malengo yao binafsi.
Lakini kabla ya kutengeneza msimamo au kuchukua au kukubaliana kuchukua hatua stahiki dhidi ya serikali tujiulize kwanza ni kitu gani tumekifanya ambacho tunaweza tukatumia kama silaha na sababu ya kufanya maamuzi...Je binafsi tunawajibika ipaswavyo katika maeneo yetu? Je tu waadilifu kwa kiasi gani? Je dhamira zetu za kimapinduzi ni matokeo ya kimkumbo na kimakundi au ni dhamira za kweli na dhato toka katika mioyo yetu?
Tujiulize haya kwa lengo la kujua kama kweli tupo tayari kwa mabadiliko na tuna weza kuwa ni mibadalala mizuri.
Vingenevyo tunaweza tukamtoa mgonjwa na kuweka maiti.....
Tujiulize kabla ya kufanya maamuzi