Mheshimiwa John Mnyika: What is Plan C

Mheshimiwa John Mnyika: What is Plan C

Plan C ingeweza kuwa kwa serikali kualika wawekezaji kuja kufungua mradi wa Photovoltaic power plant. Jua tunalo a kutosha halafu tunakaa kwenye gizs? Nina uhakika wakianza na walau 25 MW kwa jiji la Dar au Ars itasaidia sana kupunguza tatizo hili umeme.

I am sure kama serikali ina nia, wawekezaji wapo and that could be done on credit.
 
Mbona Nd. Mnyika mbunge wa ubungo kimya?
 
Jamani suala hili ni kubwa sana na nawashukuru Mods kwa kuiacha hii post siku kadhaa hapa... Plan C kwangu ni DHAMIRA YA KWELI YA KULITATUA TATIZO HILI, hii kwangu ndo Plan C.. Kwanini nasema hivyo: Kama ni kuchangisha wananchi viongozi wetu wanaweza kuchangisha pesa ya kununua mitambo kama ile ya Symbion (zamani Dowans) mipya katika muda wa siku 4, wakifanya harambee Dar, Mwanza, Mbeya na Arusha kwa kuwaalika matariji wetu, pesa ya kununua mitambo itapatikana.
DHAMIRA... Angalia sasa tunaona viongozi wenye ushawishi ambao labda wanataka kuwania urais 2015 wanafanya harambee kwenye makanisa inapatikana kama 800mils sasa tukilifanya hili suala kuwa ni la kitaifa zaidi tutalitatua. Lakini kwa sasa serikali haiwezi kufanya hivyo kwa sababu wanaogopa kukiri kuwa wameshindwa..
Kila mtanzania akiwa na DHAMIRA ya kweli kuanzia KIongozi alieko juu mpaka wa chini hii aibu tutaishinda vinginevyo historia hii itajirudia.
 
Plan C

NI ya uhakika,ina hitaji uamuzi tu,

maandamano ya amani ya wananchi kuhamia katika ikuu za wilaya, mikoa na magogoni kuomboleza na kuwazomea CCM na kikwete mpka wakabidhi serikali na mamlaka kwa wananchi. Wote walio fanya hivyo wamefanikiwa. Misri, Libya, nk nk

If this will be plan c then there will no more plans,it will be end of the opressors and thugs who are ruling us now. tofaouti na plan c kuwa hii nikwamba kutakuwa mpaka plan Z, and still the void will leave.

Kama mnafikiri haki tutapewa kwenye sahani ya dhahabu, basi sisi ni ''kwisha kabisa!'

Right is bought for blood,
lucky for the nation whose sons have got blood.
 
Kwa wananchi plan c ndiyo suluhisho lakini plan c kwa ccm polisi na jeshi dhidi ya wananchi
 
Kwa wananchi plan c ndiyo suluhisho lakini plan c kwa ccm polisi na jeshi dhidi ya wananchi
<br />
<br />

Polisi na jeshi hatimaye ni wananchi, baba zao,mama zao,watoto,wake zao ndugu na jamaa zao watakuwa kwenye maadamano yasiyo na kikomo!
 
hata kama tukichangia mafuta,bado kama hakuna uadilifu wanawza kuyaiba na kuyauza vile vile..nafikiri nchii haijakosa fedha za kuhakikisha umeme wa uhakika unakuwepo..TATIZO NI VIONGOZI WAIOTAKA KUWAJIBIKA NA HII INATOKANA NA KUWEKANA MADARAKANI KWASABABU ZA KUFAHAMIANA AND NOT KUTOKANA NA UWEZO WA MTU
 
Kuchangishana mafuta naöna ni ngumu sana. Hebu tuangalie ni watu wangapi wanaotumia huu umeme wa tanesco. Kati ya hao ni wangapi wana majenereta, kati ya wenye majenereta ni wangapi wana uwezo wa kununua mafuta pindi wanapokosa umeme wa tanesco?
Kwa mtazamo wa haraka haraka idadi ya hao watu itakuwa inapungua, na kama inapungua malengo yatatimia!
Kuchangia itawezekana iwapo.
1. Watu wote either wana umeme majumbani kwao au hawana wawe tayari.
2. Watu hawatakuwa wabinafsi, yaani mwenye uwezo wa kuchangia million akachangia million bila kujali wengine wamechangia kidogo kiasi gani.
 
Kuchangishana mafuta naöna ni ngumu sana. Hebu tuangalie ni watu wangapi wanaotumia huu umeme wa tanesco. Kati ya hao ni wangapi wana majenereta, kati ya wenye majenereta ni wangapi wana uwezo wa kununua mafuta pindi wanapokosa umeme wa tanesco?
Kwa mtazamo wa haraka haraka idadi ya hao watu itakuwa inapungua, na kama inapungua malengo yatatimia!
Kuchangia itawezekana iwapo.
1. Watu wote either wana umeme majumbani kwao au hawana wawe tayari.
2. Watu hawatakuwa wabinafsi, yaani mwenye uwezo wa kuchangia million akachangia million bila kujali wengine wamechangia kidogo kiasi gani.

Issue ni kwamba hata wale ambao hawana umeme kukosa umeme kuna madhara kwao sababu na viwanda vichache vilivyopo vinatumia umeme, vile vile ni kwamba kuchanga kwetu maybe hata wachache wakichanga serikali itaona aibu na tutakuwa tumewalazimisha kufanya kazi yao..., Sababu wataona ni kama sisi wananchi tunawafundisha kazi na wenyewe wameshindwa kazi (yaani inakuwa symbolic)
 
Issue ni kwamba hata wale ambao hawana umeme kukosa umeme kuna madhara kwao sababu na viwanda vichache vilivyopo vinatumia umeme, vile vile ni kwamba kuchanga kwetu maybe hata wachache wakichanga serikali itaona aibu na tutakuwa tumewalazimisha kufanya kazi yao..., Sababu wataona ni kama sisi wananchi tunawafundisha kazi na wenyewe wameshindwa kazi (yaani inakuwa symbolic)
<br />
<br />
issue ni kwamba watakuwa willing kuchanga?
Maana sumu ya ubinafsi/umimi ishatutafuna kuanzia ngazi za juu hadi chini.
 
Mkuu samahani kidogo, naona umeshindwa kutofautisha serikali na uongozi wake na badala yake ukasema serikali imeshindwa hivyo wananchi tuchukue hatua wenyewe za kuchangishana.

Serikali ndo raia wenyewe kwa ujumla wao, tatizo lililopo ni kwamba viongozi tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha wamechemsha.
Suala la kuchangishana halipo kabisa kwasababu tayari tulishachangia sana maendeleo ya taifa letu kupitia "Diect and indirect tax".

Bado ikwa kama vile haitoshi, tukatangaza tatizo la umeme kuwa ni janga la taifa ili mataifa tajiri waje kutusaidia lakini bado hamna kitu, nadhani kama watz kama tuna akili timamu i think its a right time to take right measurea against our representatives, otherwise we must forget changes against these problem, kwa pamoja tuseme CCM ITOKE WATZ WAPATE UMEME, MAJI, ELIMU, AFYA na matatizo mengine yanayosumbua taifa hili.
 
Mkuu samahani kidogo, naona umeshindwa kutofautisha serikali na uongozi wake na badala yake ukasema serikali imeshindwa hivyo wananchi tuchukue hatua wenyewe za kuchangishana.
Serikali ndo raia wenyewe kwa ujumla wao, tatizo lililopo ni kwamba viongozi tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha wamechemsha.
Mkuu hii serikali ndio raia wenyewe kwa ujumla wake ni theoretical au practically...., hii serikali ni ya chama tawala na ndio wenye say ya kila kinachofanyika...

Suala la kuchangishana halipo kabisa kwasababu tayari tulishachangia sana maendeleo ya taifa letu kupitia "Diect and indirect tax". Bado ikwa kama vile haitoshi, tukatangaza tatizo la umeme kuwa ni janga la taifa ili mataifa tajiri waje kutusaidia lakini bado hamna kitu, nadhani kama watz kama tuna akili timamu i think its a right time to take right measurea against our representatives, otherwise we must forget changes against these problem, kwa pamoja tuseme CCM ITOKE WATZ WAPATE UMEME, MAJI, ELIMU, AFYA na matatizo mengine yanayosumbua taifa hili.

Mkuu ndio ni kweli kwamba hizi pesa zote ni zetu through taxes lakini the question is je inafanya kazi mpaka sasa ni kwamba yote tuliyoyajaribu mpaka sasa hayafanyi kazi kwahiyo hapa nikamuuliza waziri kivuli je tunaweza kufanya nini..., ? na sababu wenyewe hawakusanyi kodi je tunaweza kujitolea hata kidogo sisi wananchi na kuwaunga mkono kwenye plan yoyote ambayo ikifika 2015 wanaweza wakasema walijaribu kufanya ABC na ikafanikiwa kuleta nishati hata ikiwa ni kijiji kimoja popote pale..., kwa kufanya hivi itakuwa ni mtaji tosha wa kuiongoa CCM huenda hata wale wapenda Tshirt watapigia kura upinzani na hiyo ndio itakuwa njia ya kuongoa CCM
 
Kama ilivyo kawaida ya watanzania tutaendelea kupiga vuvuzela but kama suluhu ni kuing'oa CCM who dares to sacrifice him/herself to the Front Line?
Hii ndiyo tofauti ya waarabu na wabongo, kwao wao ni 'kujilipua' kwa bomu kwanza maneno baadaye..kwetu sisi ni maneno mengi hakuna hata wa kujifunga bomu akajilipue katika mlango wa Ikulu!!!

Karibuni katika nyumba ya lawama....bila vitendo......Tanzania..home sweet home!
 
  • Thanks
Reactions: BBJ
naam mkuu ndio maana nikashauri kama tatizo ni hakuna mafuta na baadhi ya mitambo imezimwa.., basi inabidi hata tufahamu gharama ya kuendeshea mitambo hio kwa siku hata moja tu..!! Na sisi wanajamiii na wananchi tuchangishe na kuendesha hio mitambo kwa siku moja kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeonyesha njia ya kufanya ambapo serikali itaona aibu na hata waheshimiwa wetu itabidi waone aibu kwa kula maposho wakati wananchi tunakopa ili tu, tupate mwanga hata wa siku moja
Hata kama sisi wananchi tukichanga,bado hiyo hela tuliyoichanga pia wataila tu.solution ni kuwatoa kabisaa madarakani cause wameshaprove failure,they should step down.
 
VOR kwa kweli hali halisi iliyokuwepo ni matokeo ya muda mrefu ya kupeana posho na kupitisha bajeti zisizokuwa na mashiko nimesikia msemaji wa tanesco mwanza anasema mtakaa gizani kwa miezi 4 unless otherwise miujiza itokee.

Swali kwako, kama wizara ambayo ndo yenye mamlaka/madaraka ya kuregulate hali kama hii imetoa jibu rahisi namna hii kweli mnyika hata akitoa option yenye positive impanct kweli itafanyiwa kazi?

Miezi minne kwa mikoa kama mwanza,mbeya and arusha kukosa umeme ni janga la taifa kweli sh itaporomoka sana.

Note; Viongozi wengi hawawajibiki kwa kuwa hakuna wa kuwawajibisha......take a note
Kaka hawa watu wamekusudia, kwanini iwe MWANZA, MBEYA, NA ARUSHA TU, au kwa sababu CCM hawakupata kura huko?
 
Kusema kweli plan c ni kuwaondoa hawa mafisadi kwenye uongozi

then kuondoa vongozi wote wanaoshikilia nyadhifa muhimu na za maamuzi na kuweka wachapa kazi maana hawa waliopo wanaendekeza kujuana, na kujali matumbo yao.

Then kuweka taratibu bora za kuchagua viongozi mfano madirector, makatibu wa kuu yaani wale watendaji wote wasiwe appointee wa prez kuwa na kamati na wawe interviewed kama ilivyofanyika kenya.


Baadae mabadiliko yataendelea kuja polepole maana hawa jamaa wamejipanga kila sehemu.



heshima mbele mkuu na hongera kwa kazi nzuri....

Ni kweli kwamba nyie sio wakusanya kodi lakini tulipofika tunahitaji msaada sababu kinachofanyika sasa hakifanyi kazi….

plan a: Serikali, waziri ngereja na watu wake wameshindwa kazi kinachoendelea sasa ni usanii na watu hatupewi majibu yanayoeleweka

plan b: Kuandamana mpaka kieleweke lakini sidhani kama hii itasaidia na je isiposaidia ni nini kitafuata…. What is plan c:

Sababu watu waliotakiwa kufanya kazi yao wameshindwa tunaomba wewe waziri kivuli tushauliane ni nini cha kufanya, na tuone kama sisi wananchi tunaweza kujinasua wenyewe katika hii laana ya kujitakia ambayo imepelekea uchumi kusimama...

Ni ukweli usiopingika kwamba sasa hali ni mbaya sana sehemu kama mbeya, arusha na mwanza watu hawana umeme kwa takriban wiki sasa. Yaani umeme haurudi hata dakika moja watu wamebadilisha fridge kuwa kabati na kuvaa nguo ambayo haijanyoshwa imekuwa fashion.

Mwanza huwa wanapata mgao wa 42mw kutoka grid wakati sasa wanapewa 4mw… sasa je tatizo ni nini je ni mitambo au mafuta ndio hayapo na kama ni mafuta kwanini tunakodi mitambo ambayo itakuja kutumia mafuta hayo hayo na kama ni mvua iweje baada ya bajeti kupita ndio maji kuisha kabisa (yaani ule umeme tuliopata wakati bajeti haijapita ulitoka wapi..)

pendekezo
sababu serikali imeshindwa je sisi wananchi tunaweza kuchangia nini..?, kama tatizo ni mafuta ni vema tukajua hayo mafuta gharama ni kiasi gani ili wananchi na wadau tuweze kujitolea (sababu ni more expensive kutumia generator ndogo ndogo kuliko generator kubwa za tanesco ambazo ni more efficient). Mfano nyakato mwanza huwa kuna generator sasa kama hizi hazijawashwa nina uhakika wafanya biashara wote watakuwa tayari kuona kwamba hizi zinawashwa hata kwa kuchangia gharama...

Kwa niaba ya wananchi wengine tunakuomba tuchangie mawazo ni kipi tunaweza kufanya ili kuondokana na huu usumbufu.., hata kwa kuonyesha mfano kwa kuondoa huu usumbufu hata kwa kusaidia mtaa mmoja au kuhakikisha inapita harambee ya kuchangia mafuta… (kama tatizo ni mafuta..) (nina uhakika hii italipa dividends come 2015)

ninaomba mawazo yako mkuu wewe kama waziri kivuli na mwana-jamvi mwenzetu sababu hii emergency solution kama itafanikiwa december ambapo mvua zitaanza sioni kwanini ziitwe emergency kwangu mimi zinaonekana kama long term solution
 
Plan c:2kubali gharama kubwa ya mafuta kuokoa kidogo kuliko kupoteza kabisha,then sirikali iache hy siri yk na kutafuta wawekezaji kwani wako wengi mno,hapo 2tafanikiwa
 
Back
Top Bottom