Pezzonovante
JF-Expert Member
- May 1, 2008
- 638
- 41
bila kuing'oa ccm katu hatutaweza kuleta mabadiliko
lazima tungoe hadi mizizi
bila kuing'oa ccm katu hatutaweza kuleta mabadiliko
Mr rocky nna uhakika unajidai umelala na cku zote anayejidai amelala ni vigumu kumuamsha. ata kama hutaki kuamka cc 2takupa ukweli ivoivo mwisho utaamka tu. najua akifa baba ako au mama ako kwa tatizo la umeme hospitalini utaamka 2 kwan nnaona unaona wanakufa mahospitalini kwa kukosa operation juu ya tatizo la umeme unawaona kama wanyama tena wale wasio na faida duniani. mwogope mungu ongea ukweli acha kujidai umelala.

Heshima Mbele Mkuu na Hongera kwa Kazi Nzuri....

Ni kweli kwamba nyie sio wakusanya Kodi lakini tulipofika tunahitaji msaada sababu kinachofanyika sasa hakifanyi kazi .

Plan A: Serikali, Waziri Ngereja na watu wake wameshindwa kazi kinachoendelea sasa ni usanii na watu hatupewi majibu yanayoeleweka

Plan B: Kuandamana mpaka kieleweke lakini sidhani kama hii itasaidia na je isiposaidia ni nini kitafuata . what is Plan C:

Sababu watu waliotakiwa kufanya kazi yao wameshindwa tunaomba wewe Waziri kivuli tushauliane ni nini cha kufanya, na tuone kama sisi wananchi tunaweza kujinasua wenyewe katika hii laana ya kujitakia ambayo imepelekea uchumi kusimama...

Ni ukweli usiopingika kwamba sasa hali ni mbaya sana sehemu kama Mbeya, Arusha na Mwanza watu hawana umeme kwa takriban wiki sasa. Yaani umeme haurudi hata dakika moja watu wamebadilisha fridge kuwa kabati na kuvaa nguo ambayo haijanyoshwa imekuwa fashion.

Mwanza huwa wanapata mgao wa 42MW kutoka grid wakati sasa wanapewa 4MW Sasa Je tatizo ni nini je ni mitambo au mafuta ndio hayapo na kama ni mafuta kwanini tunakodi mitambo ambayo itakuja kutumia mafuta hayo hayo na kama ni mvua iweje baada ya bajeti kupita ndio maji kuisha kabisa (yaani ule umeme tuliopata wakati bajeti haijapita ulitoka wapi..)

Pendekezo

Sababu Serikali imeshindwa Je sisi wananchi tunaweza kuchangia nini..?, Kama tatizo ni mafuta ni vema tukajua hayo mafuta gharama ni kiasi gani ili wananchi na wadau tuweze kujitolea (sababu ni more expensive kutumia generator ndogo ndogo kuliko generator kubwa za Tanesco ambazo ni more efficient). Mfano Nyakato Mwanza huwa kuna Generator sasa kama hizi hazijawashwa nina uhakika wafanya biashara wote watakuwa tayari kuona kwamba hizi zinawashwa hata kwa kuchangia gharama...

Kwa niaba ya wananchi wengine tunakuomba tuchangie mawazo ni kipi tunaweza kufanya ili kuondokana na huu usumbufu.., hata kwa kuonyesha mfano kwa kuondoa huu usumbufu hata kwa kusaidia mtaa mmoja au kuhakikisha inapita harambee ya kuchangia mafuta (kama tatizo ni mafuta..) (nina uhakika hii italipa dividends come 2015)

Ninaomba mawazo yako mkuu wewe kama Waziri Kivuli na Mwana-Jamvi mwenzetu sababu hii emergency solution kama itafanikiwa December ambapo mvua zitaanza sioni kwanini ziitwe emergency kwangu mimi zinaonekana kama long term solution
Tanzania wake up!!!!!!!!!!!yaani unasikitisha unamuuliza Mnyika what next?yeye amekwambia wewe una mpango ngani kuikomboa nchi hii,good luck you!!you are well informed!!wewe kama wewe unnafanyaje?Tanzania wake up!!!!!!!!!!!!!
Bila kuing'oa CCM katu hatutaweza kuleta mabadiliko
Why asking John Mnyika, and not the Government. Serikali haina cha plan A wala Z. Ila kuna siku haya mambo yataeleweka tu wala wewe usihangaike na Mnyika.

Mimi nadhani kama ikifikia hatua ya sisi kuchangishana kwa ajili ya umeme hakuna sababu ya kuwa na serikali. Naona ni heri kuitoa serikali kwanza then tuangalie ustaarabu mwingine.

Mnaruka ruka weee, kuweni wawazi bana kuwa mnataka kuandamana kama Misri, Tunisia na kwingine ili kuingoa serikali kwanguvu
Mkuu gharama unazotoa sasa na unazoingia sasa kwa kukosa umeme ni maradufu kuongeza na kodi zako pia unazotoa.., ni ukweli usiopingika kwamba gharama ya kutumia generator moja moja ni zaidi ya gharama za kutumia generator za Tanesco za mafuta mazito.., ofcourse long term solution ni kuondokana na tegemezi la umeme wa mafuta na Tanzania tuna vyanzo vingi sana, hapa ndio serikalin inabidi ije na miradi ya kufaa (ambacho mpaka sasa hawajafanya..) hivyo basi tufanye nini ili tuweze kuwaforce wafanye kazi zao..., iwapo sisi wananchi tunaweza kuonyesha njia tutawaondolea kile ambacho kila siku wanasema hakiwezekani (kama wewe ulivyosema hapo juu) na hivyo basi watashindwa kuwadanganya wananchi kwa issue ya umeme ni ngumu...Ndugu yangu "senior expert member" sitaki kuamini kwamba tunachokijadili hapa hukijui na ndo maana unatoa mapendekezo ambayo kwa mtazamo wangu "hayawezi kusaidia". Nataka nikukumbushe tu kwamba hitaji la umeme sio hitaji dogo la kufanyia harambee kama mnavyofanya kwa ajili ya kicheni party, send-off, harusi au kuchangia mtoto aliyekosa ada ili aende shule. Tunaongelea hitaji la mamilioni, kama sio mabilioni ya pesa ili kuendesha miradi mikubwa ya kuzalisha umeme.
Mkuu hakuna mtu anayeibisha kwamba serikali inabidi ituangalie kwa pesa inazochukua, na maliasili zetu inazochezea, tena inabidi sio kutupa umeme tu, bali hata afya ya bure, elimu ya bure na uhakika wa kutuangalia tunapozeeka.., lakini swali ni kwamba je wanafanya hivyo...?, au tuendelee kukaa tu mpaka watakapoanza kufanya hivyo...??Kumbuka pia kwamba mafuta yanayohitajika si kwa kiasi cha kufanyia harambee kama unavyopendekeza. Hayo yote tisa, la mwisho, ambalo kimsingi ndiyo hoja yangu, nataka kukumbusha kwamba kama ni harambee wananchi tumefanya nyingi na za kutosha, na bado tunaendelea kufanya kwa ajili ya kutatua matatizo tuliyonayo kwa maendeleo ya nchi yetu-ikiwa ni pamoja na umeme.
Pengine utajiuliza tunafanya harambee hizo kwa njia gani! Jibu liko wazi: Ni kupitia kodi yako na yangu, na ya watanzania wote. Mimi binafsi nalipa zaidi ya Tsh 150, 000 kama kodi ya mapato kila mwezi-achilia mbali kodi kubwa ninayolipa kupitia kununua bidhaa na huduma itokanayo na VAT. Wewe pia unajua ni kiasi gani unalipa na wengine wote. Hata kama hulipi kodi ya mapato kwa maana ya kwamba wewe si mfanyabiashara wala mfanyakazi katika sekta rasmi (serikali na taasisi zake au mashirika ya umma na binafsi), bado unalipa kodi nyingi tu kupitia kila kitu unachonunua maana kuna kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ambayo inajumuishwa katika garama ya kila bidhaa unayonunua au huduma unayolipia.
Hivyo ni vema watanzania tukajua kwamba heal inazozitumia serikali ni hela zetu. Kwa lugha nyingine: Watanzania tunaji-mobilize kila siku kufanya harambee kupata hela ambazo ndizo akina Jairo na wengine wanazitumbua. Kwa msingi huo sioni mantiki ya hoja ya watanzania "kuji-mobilize kwa hali na mali" ili kondokana na matatizo tuliyo nayo ilihali tayari tumejimobilze vya kutosha. Itoshe watanzania tukaelewa kwamba wale tuliowapa dhamana ya kuzitumia hela hizo kutuletea maendeleo wameamua kuzitumia kwa namna wanayojua wao ili wajiletee maedeleo yao binafsi kwa jasho letu watanzania.
Kwa hiyo mkuu waTanzania watajimobilize lini (ambayo ni kazi kubwa sababu wengi wetu wapo usingizini); na hata kama tutafanya maandamano mpaka miguu ikaingia tumboni kwa kutembea ni kweli tutaleta mabadiliko...????KWA MSINGI HUO, NAKUBALIANA NA HOJA YA WATANZANIA "KUJI-MOBILIZE" LAKINI KWA LENGO MOJA TU, NALO NI "KUIONDOA SERIKALI YA SISIEMU AMBAYO IMELEWA NA KUJISAHAU KIASI KWAMBA HATA SERIKALI YENYEWE INAPINGANA KIMAAMUZI. MFANO WA HIVI KARIBUNI NI LILE SUALA LA NDG DAVID JAIRO. WATANZANIA TUMEONA NAMAN SERIKALI YETU ILIVYOSINZIA KIASI KWAMBA KILA KIONGOZI ANAKUJA NA MAAMUZI YAKE AMBAYO NAWEZA KUSEMA NI MAWAZO BIANFSI YA MTU HUSIKA KWA MASLAHI YAKE..