Mhe.Tundu Lissu ndani ITV


mkuu kwa hiyo mimi na wewe tuna kubaliana kuwa lissu amesema chama bado hali si shwari?

Basi tumpongeze kwa kusema ukweli.
 
Mh Godbless J Lema popote ulipo naomba uje utupe nukuu yeyote kutoka kwa viongozi maarufu duniani kuhusu Viongozi wanaosema ukweli hata kama ukweli huo utawauma wengi.
 
Last edited by a moderator:
Wengine inaonyesha walitazama sio walisikiliza

Wanamwekea kamanda Lissu maneno mdomoni
 
wengine inaonyesha walitazama sio walisikiliza

wanamwekea kamanda lissu maneno mdomoni

mkuu hebu wathibitishie wana jamvi ni maneno gani kamanda wako ame wekewa?
Uliangalia kipindi toka mwanzo kamanda wa lissu?
 
mkuu kwa hiyo mimi na wewe tuna kubaliana kuwa lissu amesema chama bado hali si shwari?

Basi tumpongeze kwa kusema ukweli.

usijishushie hadhi yako kirahisi namna hii,
Chama kina kesi mahakamani na hili sii jambo la siri na haihitaji darasa kujua kuwa hapo kuna mgogoro.

ukiona akili yako inasubiri kuambiwa jambo unaloliona kwa macho ujue uko kwenye distiction zone kama ile mimnyama ya zamaaani (dinosauria) yalivyoangamia kwa kushindwa kuchukua hatua ya kujiokoa na majanga.

Hakuna ajabu Lissu kusema chadema kuna mgogoro mpaka utake kutushikia akili eti tumpongeze.
 
Ndiyo maana JULIANA imewamaliza kwa kuingia Kichwa Kichwa mkiwa wazima wazima.
 
Hilo la sheria kuandikwa kwa Kiingereza ni jambo la kipumbavu kabisa. Na mimi nimeshalipinga mara nyingi tu humu.

Sheria zetu wenyewe, tuna lugha yetu wenyewe, tena ambayo tunapenda kujitamba nayo hapa na pale.

Sasa iweje sheria zetu wenyewe tuziandike kwa lugha ya kigeni ambayo ni watu wachache sana wanaielewa?

Ni kwamba hatuna akili za kutosha kutunga sheria zetu wenyewe katika lugha yetu wenyewe?

Kama hilo tu linatushinda, nini ambacho tunakiweza sisi?

Huo ni upumbavu kabisa.

Kuna wakati niliwahi kumsoma mmoja wa "wasomi" wa sheria humu katika mjadala wa kwa nini sheria zetu haziandikwi kwa Kiswahili, huyo jamaa "msomi" akasema sheria ni "noble profession", kana kwamba zikiandikwa kwa Kiswahili basi fani haitakuwa "noble" tena.

Matatizo yetu ni makubwa kuzidi lugha!!
 
mkuu huko kwenye sheria huwa ana wachanganya wengi hasa viongozi wake.

Kumpeleka kwenye tume ni kutaka kuwapotosha wananchi, inapofika kwenye maswala kama haya ana kuwa na jaziba sana.

Lakini kwa leo naona ana stahili pongezi.
sijawahi kuona mhaya Mjinga Kama wewe jitambue uwe unapangilia ya kuongea sio muda wote ni. CDM Pambaf
 
mkuu unazidi kudhihirisha kuwa bavicha ni chuo cha matusi na unajisumbua bure.

Naomba tuungane kumpongeza Tundu Lissu.

Pongezi za nini, Lissu hahitaji pongezi na sifa za kijinga, kaelezea hali halisi ilivyo CHADEMA na wala haihitaji mtu kusubiri kuelezwa na Lissu jinsi hali ilivyo. Kuna watu wanakuwa subjective/wafuasi wa mtu, wapo ndani ya chama kwa sababu ya mtu fulani, akiondoka na wao wanaondoka, ndio hali halisi ya Watanzania walio wengi, hawapo objective.

Sasa wewe umesubiri Lissu aseme ndo uelewe, sisi wengine tunalielewa hilo toka mwanzo. Ndio maana nikasema hakuna uzalendo wowote kwa Lissu kuongelewa hilo, na ndio maana nikatoa mfano wa mkeo na vidume na simulizi utayoitoa baada ya kuwashuhudia.

Ukiwa unafanya maamuzi ni lazima utambue matokeo ya hayo maamuzi na jinsi unavyoweza kabiliana na matokeo hayo. Iwe ni matokeo mazuri au mabaya.

Acha ushabiki wa.....
 

Unastahili zaidi ya kujadiri Zitto.
 

Unachotka tukielewe kutokana na hoja zako hata wewe hukielewi. Komaa tu na Zitto wako.
 
Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge.

Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.

Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.

source; cluods fm na star tv.
 
Hili tatizo siyo kwa wabunge peke yao ni tatizo la kitaifa. Nchi hii hata baadhi ya wasomi wa vyuo vikuu na wa kwenye sekta za umma hawajui kiingereza vizuri na wanapata shida wanapokutana na wenzao wa nchi za nje kujadili masuala yanayogua maslahi ya nchi.
 
Aibu. Ni kweli na sio bunge tu bali pia katika nyanja zote za uendeshaji nchi hii. Hivi majuzi nilikuwa kwenye mkutano nje ya nchi (nahifadhi), kukaja delegation ya Tanzania kama watu 8 hivi. Kwenye kutoa michango ya panel ilikuwa ni aibu kwani jamaa hawajui kabisa kutengeneza sentenso za kiingereza. Ilinibidi niiname chini kwa kuona aibu jinsi waTanzania wenzi wangu walivyokuwa wanachemsha. Ifanyike juhudi ya makusudi kuwapiga msasa wabunge na watanzania wote kwa ujumla ili waweze kuimudu lugha hii muhimu katika ulimwengu wa sasa.
 
^^
Mfumo wa kuwapata wabunge ndio mbovu sio lugha.
^^
 

Anampiga Mwenyekiti wake. Lissu kweli mhafidhina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…