Mhe.Tundu Lissu ndani ITV

Mhe.Tundu Lissu ndani ITV

Hivi umeelewa Lissu alichokuwa akisema? Au umekurupuka. Lissu anahimiza matumizi ya lugha ya kiswahili bungeni. Anashangaa bunge linatunga sheria zinaandikwa kwa kiingereza wakati hata spika wa bunge bi Kiroboto hajui lugha hiyo.

Samahani ndugu Don-oba, naomba tusaidiane hapa. Kwanza nanukuu thread hii "Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge.

Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.

Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.

source; cluods fm na star tv."
Mwisho wa nukuu.


Nukuu toka kwako quot hapo juu "Lissu anahimiza matumizi ya lugha ya kiswahili bungeni" Tafadhali hebu nionyesha hata neno moja katika THREAD anaposisitiza matumizi ya lugha ya KISWAHILI BUNGENI.

Ukipakosa niombe RADHI.
 
utaifakwanza unapotosha; alichosema ni kuwa miswada ya sheria huandikwa kwa Kiingereza hivyo wabunge huishia kupiga makofi kwa maana hawajui kiingereza. Na alisema kuna watu wenye elimu na vyeo vikubwa lakini hawajui kiingereza alichoshauri ni kuwa miswada ya sheria iandikwe kwa kiswali ambacho kinazungumzwa na kila mtu

wee nanga kweli, sasa unapinga nini na unasapoti nini? Mbowe ana cheo kidogo? Msigwa ana cheo kidogo? Sugu ana cheo kidogo?
 
Ukweli huwa haubagui. Km mwenyekiti wake hajui kiingereza huo utabaki kuwa ndio ukweli.
Hoja ya Lissu iko kwenye uelewa na uchangiaji. Labda niwaulize wote wanaopiga vijemba; Je, kuna ushahidi kuwa Mbowe ameshindwa kuchangia hoja kwa ufasaha wakati wowote?

mbowe ameshindwa kukiwakilisha chadema vyema nje ya nchi kwa fursa mbalimbali alizopata. Kikwazo kikubwa ni communication barrier..hajui kiingereza, ndio maana wenzake wanasema, 'he is too local'
 
Lissu sasa anauona ukweli na anaungana mawazo na mtizamo na akina kitila mkumbo na mwigamba kwamba he is too local
 
Qualification kubwa kabisa ya kuwa mwanasheria ni lazima ujue oral english.
Hii ni imani potofu inayotokana na fikra za ukoloni-mamboleo. Yaani unataka kuniambia wanasheria walioko kwenye nchi zisizoongea Kiingereza sio wanasheria?
 
wee nanga kweli, sasa unapinga nini na unasapoti nini? Mbowe ana cheo kidogo? Msigwa ana cheo kidogo? Sugu ana cheo kidogo?

T2015CCM ulifuatilia hicho kipindi au na wewe umesoma tuu hapa JF? Kama hukufuatia mimi nilifuatilia na hoja ya Lissu ilikuwa ni miswada iandikwe kwa Kiswahili, mwenendo wa kesi uandikwe kwa kiswahili; hata hivyo wabunge wanaopiga makofu bungeni badala ya kuchangia hoja si hao uliowataja hakika unawafahamu ila umeamua kunitukana, ahsante sana
 
Huyu mtu wenu kweli njeke yaani anaona lugha hii ya kishoga ni bonge la deal,huu ni upumbavu uliochupa mipaka kujisifu kuwa unaongea lugha ya mwenzako ilhali mwenye lugha anakucheka kwa kuongea lugha yake,mara nyengine uje na malalamiko ya wabunge wasiojua kiswahili au umesahau kuwa kiswahili ni lugha ya taifa.ningekuona WA maana sana kama ungefanya hivi.
Nalog off
 
kwa matusi aya kwa mkt wake lisu atapona kwel!,,tehe tehe kaamua kuwalipua akina zero
 
Samahani ndugu Don-oba, naomba tusaidiane hapa. Kwanza nanukuu thread hii "Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge.

Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.

Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.

source; cluods fm na star tv."
Mwisho wa nukuu.


Nukuu toka kwako quot hapo juu "Lissu anahimiza matumizi ya lugha ya kiswahili bungeni" Tafadhali hebu nionyesha hata neno moja katika THREAD anaposisitiza matumizi ya lugha ya KISWAHILI BUNGENI.

Ukipakosa niombe RADHI.

thread imekaa kiuongo uongo, nahisi aliyeileta hapa alikuwa na tumbo la kuhara, UKITAKA KUJUA UKWELI TAFUTA MARUDIO YA KIPINDI CHA DAKIKA 45 CHA ITV kwenye you tube ndio umsikie HON. LISSU VIZURI
 
Hii ni imani potofu inayotokana na fikra za ukoloni-mamboleo. Yaani unataka kuniambia wanasheria walioko kwenye nchi zisizoongea Kiingereza sio wanasheria?

kwa tz lazima iwe hivyo kwasababu sheria zipo kwa kingereza
 
hivi lema na mchungaji msigwa wanajua kiingereza kweli?
 
Wanaomponda lema ktk lugha hawamjui.Ni kati ya wabunge wanaozungumza kiingereza kizuri sana
 
Kiingereza cha kikwete wakati wa ujio wa Obama


I... I think the... the issue of satisfied with MCC should have com... should have been asked .z38'rvme.


eMCC has been great assistance from the United States government to the people of Tanzania.


There are three.... three... three sectors here. There is the road sector. And the good thing about the MCC is that we decide on the..... on the areas or sectors that we need assistance. But even we decide on where. For example in the case of roads. There are roads that we spo.... we talked to many donors, who were not ready to support us. But when... when you said there is going to be support on roads I said "Let's try these roads, let's see what the American are going to say." The American said fine, if you think you need these roads fine, we will give you the money.


Those fellow Tanzanians know Namtumbo-Songea-Mbinga, Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro, the roads in Pemba. But we chose those roads because, these roads are actually in our bread basket area. This is where we get the corn: Ruvuma, Rukwa and Mbeya.


We decide.. we chose the US to assist us to increase water supply in Dar es Salaam. It is our decision. The project is now being implemented.


With electricity we said, one of our biggest problems is access to electricity for people in the rural areas. The US said fine. We have m m .. in grid 10 regions of Tanzania. Coverage of electricity has increased from 10% to 21%, is phenomenal increase.


So I want to underscore the fact that I am satisfied with the support from MCC.


Is US doing enough? The US has done a lot, but if I say they have done enough, then the President will not listen to my new requests... hahahahahaaaaaaaaaaaa


But so far so good.


Deaths from malaria have declined by over 50%, infant mortality rates have declined, HIV infections have declined. Through PMTCT (Prevention of Mother to Child Transmission) more children born by HIV infected mothers are born free of the disease. More people now...


The US has supported us now with over 2 million books. And today I asked the president we want another 2.4 million and he said we will ... to .... and I see from their face that they are in agreement with the president. So that when it comes to science and mathematics books, we will have every Tanzanian child .. have a book of his or her own, instead of the ratios that we are talking today 5 to 1 now reduced to 3 to 1. So the list is endless.


We have a lot of support, we are very appreciative, we are very thankful, it has really helped changing the lives of our people.
 
Mbona Wabunge wa mataifa mengine hawajui hiyo lugha ya mkoloni na wanapiga hatua za kimaendeleo?

Taifa kama China viongozi wengi tu hawajui Kiingereza lakini gurudumu la maendeleo linasonga?
 
Tatizo sio kukifahamu au kutokifahamu kingereza, tatizo ni kutokuwa weredi na wajuzi wa mambo yanayotuzunguka, kama tungelikuwa wajuzi wa mambo bado tungekuwa mbali tu , kwa mfano nchi kama china, japani na korea ni mifano tu ya nchi ambazo azitumii kiingereza kama kipimo cha ujuzi wa mambo lakini pia ni inchi hizo hizo ambazo maendeleo yake ni makubwa kulinganisha na nchi nyingi zinazotumia kiingereza, hivo kwa upande wangu kujua au kutokujua kingereza sio swala la kuumiza kichwa ila swala la kuumiza kichwa ni juu ya hao wawakilishi wetu kuwa na uweredi mkubwa wa mambo yanayoizunguka hii dunia kwa mstakabali mzima wa nchi yetu
 
Back
Top Bottom