Mhe.Tundu Lissu ndani ITV

Mhe.Tundu Lissu ndani ITV

Tundu Lissu bhana anapenda kuwadanganya watanzania.

Sidhani kama kingereza ni kikwazo kabisa katika shughuli nyingi za wabunge maana asilimia 70% ni kiswahili ndio kina tumika na bado utendaji ni mbovu.

Ni sehemu chache sana zina mlazimu mbunge kujua kingereza tena cha kusoma hasa kwenye mikataba.

Si kweli kingereza ni kikwazo.

Hata yeye tundu lissu aliomba msamaha kitumeke kiswahili kwa kisingizio cha maslahi ya umma kumbe kijana msando alberto alimtoa jasho kwenye lugha ya kigeni.
 
Last edited by a moderator:
Hoja ya Lisu ni kwamba; Kwa nini sheria ziandikwe kwa kiingereza ikiwa lugha ya taifa ni Kiswahili, wanaotunga sheria (wabunge) hawajui kiingereza na hata wananchi zaidi ya asilimia 95 hawajui.
Kwa hali hii kuna tatizo kubwa!
 
Sheria ni noble profession bana...hivyo sheria haziwezi kuandikwa kwa Kiswahili.
 
Sheria ni noble profession bana...hivyo sheria haziwezi kuandikwa kwa Kiswahili.

Mkuu,

Tukiwa na mawazo ya namna hii tunathibitisha utumwa wa fikra. Tunatakiwa kuwa huru kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
Mawazo yanahusiana na utamaduni na hivyo siasa na uchumi imara unatokana na utamaduni usio tegemezi!
 
Bunge hutumia lugha ya kiswahili kufikisha ujumbe kwa wananchi.

Ni muhimu kumkumbusha Tundu Lisu kuwa hatutumii kisukuma, kindengeleko, kijerumeni wala kiingereza kwenye bunge wala kwenye kampeni za kugombea Ubunge. Na wala si sherti kuwa mbunge LAZIMA AJUE KIINGEREZA kwani wabunge wengi wa Ujerumani, Ufaransa, URUSI n.k hawajui kiingereza.

Ushauri wangu kwa T. Lisu: Kama umeshindwa kufanikisha AJENDA KUU YA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI NI BORA UJIUZULU UBUNGE. HATA SIKU MOJA SITOCHAGUA MBUNGE KWA KIGEZO CHA KIINGEREZA BALI KWA UADILIFU, KUJALI WANANCHI, KUWA MBUNIFU WA UTATUZI WA MATATIZO YA WANANCHI NA KUWA SEHEMU YA WANANCHI.
Upo sawa kabisa, kwa sie wanananchi tutaona kiswahili kinatumika lakini makabrasha yao yanaandikwa kwa kizungu, nadhani hoja hapa either kuwa na wabunge wenye uweledi wa kiingereza au kiswahili ambacho ni lugha ya taifa kitumike kikamilifu mpaka kwenye makabrasha yao alafu serikali ifanye kazi ya kupeleka kwenye kiingereza
 
Tatizo kama ni english si waachane na hiyo lugha watumie kiswahili tu?wanang'ang'ania kiingereza wakati hawakiwezi?kwa nini?
 
Mbona yeye Tundu Lisu kwa wakili Msando aliomba Kitumike Kiswahili,baada ya kuchemka Kiingereza
CC
msando
Nadhani ndio maana akatoa kauli ile ili hoja hapo itumike lugha ambayo inaeleweka alafu serikali irudishe miswada kwa kiingereza mara baada ya kujadiliwa, lakini utaratibu uliopo watu wanabwabwaja kwa kiswahili alafu mambo yanaandikwa kwa kiingereza
 
Mwacheni TUNDU adadavue ukweli wewe utaendaje mjengoni kule kama ngeli haipandi bana unatuabisha, wakati mwingine tutakutana na mataifa mbalimbali utazungumza kiswahili chako na kiswangish nani ataelewa, kiingereza kiwe kigezo mojawapo wasituletee aibu hapa
 
Nakumbuka kijana Albert Msando alivyomtoa nduki Lissu kwenye matumizi ya kugha ya kiingereza wakati wa kesi ya Zitto mpaka Lissu akaomba poo kwa kuomba mahakama itengue matumizi ya lugha ya kiingereza na kutumia kiswahili

Kwa faida ya jukwaa eb tuambie ulishabahatika hata siku moja kumsikia Lukuvi, Wasira, Sofia simba au hata kiboko yenu lowasa wanaonge kizungu mkuu? Kama umeshabahatika tupe hata link tuone mkuu. Mm nlimuona comrade Philipo tu. Anatisha sana
 
Ccm wanawatongoza wananchi!!! komba alivyosikia hivyo alikurupuka kama mabomu ya mbagala, ccm kwakutafuta point 3noma.
 
Bunge hutumia lugha ya kiswahili kufikisha ujumbe kwa wananchi.

You're right, lakini pia Bunge huwa linaletewa miswada ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza ili kujadili na kuipitisha.

Sujui kama Lissu alikuwa anamaanisha hili, but hapa ndiyo penye tatizo kubwa. Niliandika kuhusiana na zile sheria za kuanzisha kodi ya simkadi kuwa pengine baadhi ya wabunge walikuwa hata hawajui walikuwa wanapitisha nini, and probably ndo maana vipengele vingine vilichomekewa kiaina bila wao kujua.

Kwa nchi kama Tanzania, Bunge linapitisha miswada mingi ya sheria iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza bila hata kuijadili kwa undani na kuifanyia marekebisho stahiki. Ndiyo maana wapo baadhi wanaopinga wale wanaopendekeza mikataba ya madini iwe inapitishwa na Bunge kwa sababu they are even more complex kujadiliwa na aina ya wabunge wengi tulionao sasa.

Kuna wabunge wengi ukija mswada wa masuala ya kodi hawataki kabisa kuigusa kwa sababu vipengele vyake mara nyingi viko too complex. Hii inatokea siyo tuu kwa wabunge wetu bali pia kwa wabunge ya nchi zilizoendelea. Lakini kwa wenzetu miswada complex kama hii huwa inapitia kwanza kwenye kamati husika ya Bunge na kujadiliwa kwa undani. Kamati za bunge zinatakiwa ziundwe na watu ambao ni experts kwenye masuala husika. Sijui kamati zetu za bunge zinaundwa na watu wenye uelewa wa aina gani.

Ni muhimu kumkumbusha Tundu Lisu kuwa hatutumii kisukuma, kindengeleko, kijerumeni wala kiingereza kwenye bunge wala kwenye kampeni za kugombea Ubunge. Na wala si sherti kuwa mbunge LAZIMA AJUE KIINGEREZA kwani wabunge wengi wa Ujerumani, Ufaransa, URUSI n.k hawajui kiingereza.

Ni kweli wabunge wengi wa Ujerumani, Ufaransa, URUSI n.k hawajui lugha ya Kiingereza, lakini serikali zao hazileti bungeni miswada iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza bali kwa lugha zao.

Lakini pia inawezekana wala tatizo siyo kutojua lugha bali ni ukosefu wa fikra tunduizi. Bunge liko taabani na halina mvuto. Mpaka wengine ikifikia kipindi cha bunge kukaa wanaishia kusema "Not again". Wabunge wanaongea kwa Kiswahili lakini mijadala mingi wanayoianzisha na kuijadili haina tafakuri tunduizi.
 
Tundu Lissu bhana anapenda kuwadanganya watanzania.

Sidhani kama kingereza ni kikwazo kabisa katika shughuli nyingi za wabunge maana asilimia 70% ni kiswahili ndio kina tumika na bado utendaji ni mbovu.

Ni sehemu chache sana zina mlazimu mbunge kujua kingereza tena cha kusoma hasa kwenye mikataba.

Si kweli kingereza ni kikwazo.

Hata yeye tundu lissu aliomba msamaha kitumeke kiswahili kwa kisingizio cha maslahi ya umma kumbe kijana msando alberto alimtoa jasho kwenye lugha ya kigeni.
wewe mwenyewe kiingereza hujui zaidi ya kusema "so called Lema" tunakujua sana wewe Mjinga unaejipachika jina la kihaya
 
Ni kweli wabunge wengi wa Ujerumani, Ufaransa, URUSI n.k hawajui lugha ya Kiingereza, lakini serikali zao hazileti bungeni miswada iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza bali kwa lugha zao.

Hivi sisi hatuwezi kutumia lugha yetu kwenye hiyo miswada na sheria?

Kigumu ni nini hasa? Ni hatuna kabisa uwezo huo (wa kuandika miswada na sheria kwa Kiswahili)? Ni kwamba labda hatujiamini kama tunaweza?

Sheria zetu wenyewe halafu tunaziandika kwa kutumia lugha ya wengine! Hmm....
 
Back
Top Bottom