Mhe.Tundu Lissu ndani ITV

Mhe.Tundu Lissu ndani ITV

Hivi sisi hatuwezi kutumia lugha yetu kwenye hiyo miswada na sheria?

Kigumu ni nini hasa? Ni hatuna kabisa uwezo huo (wa kuandika miswada na sheria kwa Kiswahili)? Ni kwamba labda hatujiamini kama tunaweza?

Sheria zetu wenyewe halafu tunaziandika kwa kutumia lugha ya wengine! Hmm....

Nyani Ngabu;

Kwa kifupi tu. Elimu bila enlightenment ina matatizo yake. Katika fani za uendeshaji wa serikali na mahakama kiswahili au lugha za makabila zinaweza kufanya kazi bila ya matatizo yoyote yale. Suala ni kujiamini tu.
 
Twaib!
 
mbowe ameshindwa kukiwakilisha chadema vyema nje ya nchi kwa fursa mbalimbali alizopata. Kikwazo kikubwa ni communication barrier..hajui kiingereza, ndio maana wenzake wanasema, 'he is too local'

Wenzake wanasema, but no proof and no definition of locality
 
Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge.

Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.

Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.

source; cluods fm na star tv.

Hii habari imepindishwa, nimemsikia mimi mwenyewe alichosema Lisu ni kwamba, kwa nini bunge lisitumie moja kwa moja kiswahili ili kuleta ufanisi wakati wa kutunga sheria. Kwani mijadala hufanyika kwa kiswahili na sheria huandikwa kwa kiingereza jambo linalowaacha mbali wabunge wengi ambao kimsingi lugha ya kiingereza inawapa taabu, matokeo yake kupigia kura za ndioooo sheria anbazo hawazielewi. Baadaye ukimwuliza mbunge juu ya sheria iliyopitishwa huikana kwamba hajapitisha "Tafakari Chukuwa Hatua"
 
Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge.

Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.

Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.

source; cluods fm na star tv.

Daaah watanzania bado limbukeni hivi tunasahau kuwa tuna lugha yetu ya kiswahili,Japan,China,Korea.,,,,,,,,nk ni nchi zilizoendelea sana mbona wanafanya mambo mambo yao bila ya kutegemea lugha za kigeni

Tuache haya mambo ya kuona lugha za kigeni ni bora kuliko lugha yetu...........
 
Tundu lisu alichosema ni kwamba kwa nn lugha ya katiba ni kiingereza haliyakuwa tanzania wananchi 100% wanatumia kiswahili,bunge asilimia 100 linatumia kiswahili,wabunge wengi hawajui kiingereza halafu wanajadili katiba iliyoandikwa kwa kiingereza,unadhani hapo si kila sheria watakuwa wanakubaliana nayo tu kwa kupiga makofi kwenye meza zao,haliyakuwa wengi wao hawajui ni nn walichokubaliana nacho!!nawasilisha.
 
Lissu anafikiri kujua sheria ndiyo kujua kiingereza nini?

Nadhani hapa kuna umuhimu wa kujua Lugha ya Kingereza ili kukupa unafuu wa kusoma na kuchambua mambo yaletwayo Bungeni hasa Miswada maana huandikwa in a technical language na ni kwa Kingereza . Sasa km hujui Kingereza utasubiri tafsiri ya Kiswahili ambayo kuna baadhi ya maneno hukosa tafsiri sahihi. Mm nafikiri suala la Lugha lipewe kipaumbele.
 
Nakumbuka kijana Albert Msando alivyomtoa nduki Lissu kwenye matumizi ya kugha ya kiingereza wakati wa kesi ya Zitto mpaka Lissu akaomba poo kwa kuomba mahakama itengue matumizi ya lugha ya kiingereza na kutumia kiswahili

hapa napingana na wewe,kwa lugha ya kiingereza Lissu yupo vizuri sana na hii inatokana na background yake,katika elimu yake alibahatika kuipata nchini marekani,suala la lugha wala halihitaji kiwango cha elimu,kuna watu wameishia elimu ya msingi na wengine kidato cha pili lakini wanazungumza kiingereza ile mbaya.Ujanja wa lugha ni kupata nafasi ya kuitumia mara kwa mara na wala siyo kukaa darasani.
 
Mbona Wabunge wa mataifa mengine hawajui hiyo lugha ya mkoloni na wanapiga hatua za kimaendeleo?

Taifa kama China viongozi wengi tu hawajui Kiingereza lakini gurudumu la maendeleo linasonga?

Unataka kufananisha Tanzania na China?

Really?
 
Mheshimiwa Lisu peleka hoja binafsi bungeni ili sheria zetu zijadiliwe bungeni kwa lugha yetu ya kiswahili.Japani wanajadili mambo yao kwa lugha yao,China halikadhalika.Tanzania tunaweza kufanya hivyo kabisa kwani tuna wataalamu wengi wabobezi wa lugha yetu ya kiswahili kwa mfano profesa Safari,profesa masamba,profesa Madumla wa Udom,profesa Kahigi mbunge wa Bukombe,Mlacha wa Udom kuwataja kwa uchache.Kwa kuwatumia wataalamu hao, ambao wengine ni wanasheria,hakuna kitakachoshindikana.
 
Back
Top Bottom