Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, Kwa Tanzania Bora Naomba zingatia haya!

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Mods naomba msiunganishe huu uzi maana una maudhui ya kipekee!

Amani iwe nawe Mama!
Kwanza napenda kukupongeza kwa jinsi gani umeonekana kuwa unasikiliza maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi haraka. Haya nimeyaona kwenye teuzi zako mbalimbali kuanzia Bandari, Katibu Mkuu Kiongozi na sasa Mkurugenzi wa TPDC.

Kama mtu ninayekuoenda na kukutakia mafanikio kwenye utendaji wako, napenda kukushauri yafuatayo.

1. Kivunje kitengo cha VETTING cha TISS na mteue Afisa Mwandamizi mzoefu kuongoza kitengo icho. Kuna walakini sana kwenye teuzi unazoletewa. Naomba uanze kukitumia kitengo hiki haraka sana.

2. Kwenye mashirika nyeti na yanayobeba uchumi wa taifa, zingatia sana uzoefu wa watu kwenye biashara na pia kimataifa ( exposure) ili upate watu sahihi watakaokuwa creative kuongoza mashirika haya. Achana na hawa makada uchwara wa CCM. Uzoefu kwenye biashara na kimataifa unafanya mtu awe creative kwenye kuongoza taasisi na kuifanya ijiongoze kwa faida. Tumia kitengo cha getting cha TISS kupata hata watu kutoka Diaspora na Taasisi za Biashara na Mabenki.

3. Usiache pia kushirikisha makatibu wakuu wako katika kutafuta watu wa kuongoza taasisi zilizo chini ya wizara zao. Makatibu wakuu ni viungo muhimu sana na pia wanajua changamoto zilizo kwenye taasisi na wanaweza kujua ni mtu gani anayeweza kufit kwenye nafasi tajwa. Makatibu wakuu pia wanazunguka sana na kukutana na watu wengi. Usiache kuwatumia.

4. Kwa upande wa Baraza la Mawaziri, Bado kwenye nafasi ya Waziri wa Viwanda na Biashara ninaona Kuna mapungufu. Sio kwamba ninamtakia mabaya kitila Mkumbo Ila kiukweli Naona hatoshi pale ulipomweka. Napendekeza tafuta mtu mwenye uzoefu wa kutosha wenye mafanikio kwenye sekta ya biashara hata mabenki mpe iyo nafasi. kama hayupo bungeni mteue awe mbunge, ninamuona Kimei anafaa sana hapa kwa mafanikio yake makubwa CRDB . Ila Kama unaona hafai napendekeza tafuta mtu wa aina yake aliyefanikiwa vizuri katika sekta binafsi.

5. Mwisho tunaitaji mabadiriko ya sheria hasa yakiwagusa TRA, Bandari na taasisi nyingine zinazosimamia biashara na uchumi ili kuzifanya ziwe taasisi za kufacilitate uchumi na biashara kukua zaidi na sio kuua biashara na wafanyabiashara.

Nakutakia jumatatu njema ya Pasaka.
 
Mda sio mrefu mtw mchoka mama Mapendekezo yenu ni mengi sana. Hakika hawezi kuyafanyia kazi yote.
 
Kidogo aingizwe chaka TPDC. Hongera Mh. Rais kwa kuona mapema, na kutengua haraka
 
Kidogo aingizwe chaka TPDC. Hongera Mh. Rais kwa kuona mapema, na kutengua haraka
Ni hatari sana! How comes shirika linalobeba uchumi wa nchi liongozwe na mtu ambaye hajawai hata kuwa kiongozi wa kikoba???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom