Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
Leo hii Rais Kikwete amekutana na baadhi ya waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari ambavyo ofisi yake ya mawasiliano ilitoa mwaliko. Baadhi ya vyombo vya habari havikupata mwaliko huo aidha kutokana na nia ya makusudi ya kutovikaribisha au kutokana na uzembe/wivu ndani ya vyombo hivyo.
Hata hivyo habari toka ndani ya mkutano huo zinaonesha kuwa mkutano ni majibu ya Rais kufuatia maswali mbalimbali ambayo yamekuwa yakiulizwa na wananchi wasitegemee jambo lolote kubwa. Waandishi wamependekeza mada ambazo wangependa Rais azungumzie (sitashangaa kama walituma maswali kabla) na Rais ataenda kwa mtindo huo wa kuangalia yale yaliyoletwa na waandishi. Sifahamu ni kwa kiasi gani waandishi watakuwa huru kuuliza mambo "nje ya" yale yaliyopendekezwa.
Hata hivyo hivi karibuni Serikali imeanzisha utaratibu ambapo mawaziri watakuwa wanakutana na waandishi wa habari kujibu maswali yao mbalimbali. Cha kushangaza ni kuwa kipimo hicho Rais mwenyewe hajajiwekea na anakutana na waandishi pale anapojisikia (kitu ambacho si kibaya ukizingatia ratiba yake ya usafiri). hata hivyo binafsi naamini kuwa wakati umefika mabadiliko makubwa yafanyike katika kutoa habari toka Ikulu.
a. Rais ajiwekee kiwango cha juu ambapo kila siku Ofisi ya Mawasilinao ya Ikulu ikutane na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya habari kwa wananchi kuhusu ratiba ya Rais anapokuwa ofisini. Mtindo huu unatumiwa sehemu mbalimbali duniani ambapo Ratiba ya kiongozi wa nchi inajulikana kwa waandishi kujua "leo Rais anakutana na nani". Na hapa nazungumzia kuhusu mambo yanayohusu kazi siyo mambo ya kukutana na mtoto wake aliyeenda kumsalimia ikulu!
b. Badala ya mtindo huu wa kuita waandishi kwa kuchagua na kubagua, Ofisi ya Mawasiliano ianzishe kitendo cha State House Press Corp ambayo itatoa press cards kwa waandishi wa vyombo vyote vya habari ambavyo vinataka kuwa katika kikundi hicho. Waandishi hao watakuwa ndio "State House Correspondents" ambao watakuwa ndio kiunganishi kati ya Ikulu na vyombo vya habari. Kimsingi Wahariri wakuu wabakie zao maofisini na waache waandishi wa chini yao na wale waliopewa nafasi hizo kufanya kazi za kuripoti toka Ikulu!
c. Rais Kikwete mwenyewe, Makamu wake, na Waziri Mkuu wajiwekee muda wa kukutana na waandishi wa habari angalau mara moja kila wiki mbili na kupokea maswali bila ya kutaka yatumwe kwanza kwao. Kipimo cha wao walichowawekea mawaziri walio chini yao waanzie wao wenyewe!
d. Kwa vile wao wamepata mwaliko wa kuzungumza na Rais, naomba na miye nijipe mwaliko wa kufanya mahojiano na Rais Live siku ya Jumapili kupitia bongoradio ikiwa ni sehemu ya kufunga mwaka na kutakiana heri ya mwaka mpya! Sitatuma maswali kwanza though.
M. M.