Mhasibu wa Benki atekwa, achomwa petroli porini

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Gazeti la kila siku la Nipashe la leo limekuja na habari nzito inayoelezea namna ya mhasibu mkuu wa bank moja hapa nchini alivyotekwa na watu wasiojulikana kupigwa ,kuteswa kisha kuchomwa moto kwa petrol porini.

=========

2527B457-71E3-482C-8B9E-0D8E3D864B8E.jpeg


JESHI la Polisi mkoani Pwani limesema mhasibu wa benki ya BOA tawi la Kahama ameuawa kwa kumwagiwa petroli na kuchomwa moto.

Inadaiwa kwamba mhasibu huyo alikuwa amefika Kibaha kwa wazazi wake.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Pius Lutumo amemtaja marehemu ni Martha Towo (30) mkazi wa Kwa Mbonde wilayani Kibaha.

Kamanda Lutumo aliwaeleza waandishi wa habari mjini Kibaha jana kuwa chanzo cha mauaji hakijafahamika na wanaendelea kuchunguza.

Inadaiwa kuwa Martha alitekwa jioni ya Machi 3 mwaka huu na saa 4:30 usiku siku hiyo hiyo alikutwa akiungua katika maeneo ya Mitamba Kata ya Pangani.

“Watu wasiojulikana walimteka kisha kummwagia mafuta na kumchoma moto,” alisema.
Kamanda Lutumo alisema taarifa zilitolewa na wasamaria polisi wakafika eneo la tukio na kumchukua kisha kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi.

“Mgonjwa alihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uangalizi zaidi wa kimatibabu lakini alifariki Alhamisi Machi 9,” alisema.

Lutumo alisema kutokana na utata kuhusu tukio hilo, polisi wanaendelea kuchunguza chanzo cha Martha kutekwa na kuchomwa moto hadi akapoteza maisha.

========
Wakati Jeshi la Polisi mkoani Pwani likithibitisha kutokea kwa kifo cha Martha Towo (30) ambaye aliuawa kwa kuchomwa moto baada ya kutekwa usiku wa Machi 3 mwaka huu wilayani Kibaha mkoani Pwani, Bank of Afrika (BOA) imesema, marehemu alishaacha kazi karibu mwezi mmoja uliopita
 
Alitekwa kama Leo jion kesho ilikua anamtambulisha mchumba wake...so wakamfunga na kumchoma na petrol.

Wasamaria wema ndo kumuokota akapelekwa muhimbili ....kauguzwa almost siku kama 4_5....na michango tumechangishana ya kuongeza nguvu kumuuguza maana alikua icu ila juzi akafariki.

Ninamfahamu na msiba naujua ila kisa Kwa kweli nahisi kinahusiana na mahusiano japo Sina uhakika maana unashindwa hata kuwahoji wafiwa .Kwa Sasa tunatazamana TU

Kwa udogo sana unaweza ukahusisha na mambo mengine ila nashangaa watu hapa mnahusisha na siasa
 
Alitekwa kama Leo jion kesho ilikua anamtambulisha mchumba wake...so wakamfunga na kumchoma na petrol.
Wasamaria wema ndo kumuokota akapelekwa muhimbili ....kauguzwa almost siku kama 4_5....na michango tumechangishana ya kuongeza nguvu kumuuguza maana alikua icu ila juzi akafariki..
Ninamfahamu na msiba naujua ila kisa Kwa kweli nahisi kinahusiana na mahusiano japo Sina uhakika maana unashindwa hata kuwahoji wafiwa .Kwa Sasa tunatazamana TU
Kwa udogo sana unaweza ukahusisha na mambo mengine ila nashangaa watu hapa mnahusisha na siasa
Poleni sana ndugu na jamaa Mungu ampe pumziko jema
 
Msiba usikie nyumba ya jirani mkuu. Hayo maneno yanaumiza kwa wafiwa
Mimi kitaaluma kabisa ni muhasibu japo ninayoyafanya sshv ni nje ya hiyo prof, nimesha fanya kazi hiyo japo sikufika mbali nikachochora, najua hekaya za hawa mabwana na nina mifano hai ya madhila yanayo wakuta waasibu, nimesha wahi simulia siku moja mkasa mmoja wa muhasibu fulani kwenye moja ya thread japo siikumbuki ilikua ina husu nini, ila ili pelekea nikakumbuka huo mkasa na kuuchangia!

Labda kwa fikra ndogo tu! Tofauti na ishu za ugoni nini kingine kinaweza kikasababisha tukio kama hilo kama sio zuluma ama ukuda makazini!? Kuna mahala tuliajiriwa kama wahasibu wanne hivi tukapewa tutorial ya kazi yao jinsi wanavyofanya, awali nilishituka, kulingana na utaratibu wao ikabidi tufanye kadiri walivyokua wanataka, kumbe tulikua mbuzi wa kafara
 
Back
Top Bottom