Mhariri wa Mwanahalisi akatwa mapanga

Nimeipata hii toka kwenye blog ya Michuzi

BREKING NYUUUUZZZZZZZ
SERIKALI itagharamia matibabu ya nje ya Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi, Saidi Kubenea, aliyesafirishwa leo, Jumatatu, Januari 7, kwenda India kwa matibabu zaidi.

Serikali inagharimia matibabu hayo ya Kubenea, kama inavyogharimia matibabu ya Watanzania wengine wanaokwenda kupata huduma za tiba nje ya nchi.

Msimamo huo wa Serikali umetangazwa mara tu baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amemtembelea na kumjulia hali Bw. Kubenea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Bw. Kubenea ambaye alilazwa Muhimbili usiku wa Jumamosi iliyopita, Januari 5, wakati watu wasiojulikana walipovamia gazeti la kila wiki la Mwanahalisi na kumjeruhi Kubenea pamoja na Mhariri wa gazeti hili, Bw. Ndimara Tegambwage.

Katika shambulio hilo, Bw. Kubenea alimwagiwa tindikali wakati Bw. Tegambwage alipigwa panga kichwani. Wakati Bw. Kubenea alilazwa hospitali, Bw. Tegambwage alitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Kama alivyokuwa ameeleza katika taarifa yake rasmi kwa vyombo vya habari jana, Januari 6, 2008, Rais Kikwete amemweleza Bw. Kubenea jinsi alivyosikitishwa na kuhudhunishwa na shambulio dhidi yake, na dhidi ya Bw. Tegambwage.

Rais amesema kuwa kama wahariri hao wameshambuliwa katika hali ya kawaida basi ni jambo baya.

Hata hivyo, amesema kuwa ni jambo baya zaidi kama wahariri hao watakuwa wameshambuliwa kwa sababu ya kazi yao ya uandishi wa habari, kwa sababu hilo ni pigo kwa juhudi za Serikali katika kulea na kuunga mkono vyombo vya habari huru na vinavyojitegemea nchini.

Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
 
Gharama za matibabu zimechangiwa na "wadau mbalimbali wa habari" na serikali si mmojawapo waliochangia.. as far as I know.. na kwenda India wengi wanapelekwa India hata watoto wenye matatizo ya moyo..

Mzee ukisoma vizuri utaona nilielezea kuwa serikali inamlipia na juzi walienda kumtaka hali kule hospitalini
 
Quote:-

"Hapa piga ua lazima pana mkono wa akina MVI"

Wakuu heshima mbele, hatimaye nimepata dataz za kwanza kutoka ground Zero ambazo sina uhakika how good they are lakini ninaiamini the source, Kubenea na Ndimara, walikuwa wakitayarisha article nzito inayotabiri kusukwa kwa baraza jipya la mawaziri, ambalo liko tayari, ndani yake walikuwa waseme kuwa mkulu ameachwa pembeni na "Tyson" kuchukua nafasi yake, info zika-leak wakiwa bado wanatayarisha hiyo article, na kufika pasipotakiwa, and the rest of the story......!,

Bado tunaendelea kuzitafuta zaidi, zikipatikana hapa hapa JF!

Ahsante Wakuuu!
 
Duh! Ahsante sana Mkuu, ukizipata hizo nyeti usikawie kutuwekea hapa.
 
Sasa katika kesi ya MWANAHALISI na huyu SAIDI naweza kuconfirm kuwa alipewa onyo na wahusika kutokana na mwenendo wake wa kutoipa serikali nafasi ya kupumua na aliiitwa mpaka kwenye mkutano lakini defese yake ilikuwa:
1)HAITOWEZEKANA kumpa matangazo as soon as that hivyo waliomba muda

2) ALIPEWA KIASI KIKUBWA TU CHA PESA ili kumkeep going for a while wakati azimio la kwanza linafanyiwa ufumbuzi

3)SAISI KUBENEA likubali zile pesa na kwa muda alisizi yale mashambulizi

Kijana Game Theory,

Mimi nakubalina na analysis yako 100%, na ninakubatiza na kukuita Real Facts. Huwesi kula kuka halafu unalilia mayai -- tanyolewa tu! Ukiamua kula na mwizi lazima siku itafika atakuibia tu. Amuulise kaka yangu Raila alidhani Kibaki ni binadamu tosha! Na mimi naamini he knows what happened to him and who did it na atanyamaza milile kwa vile conscious yake iko naye! Nzara inaponza sometimes! Kwa lugha yetu tunasema Bin En Bim translates as Nyani ni Nyani tu! ukichesa naye utaambulia mabua!

Sisi tumpe pole tu na kumkumbusha kuwa uaumuzi nusu nusu ndiyo matokeo yake.

OBAMA + ODINGA = Luo Ltd!
 
very interesting thread,wengi tuu wanapigwa mapanga lakini hapa seems kuna moshi unataka kutoka huko chini...pls dont kill this thread!
 
Quote:-

"Hapa piga ua lazima pana mkono wa akina MVI"

Wakuu heshima mbele, hatimaye nimepata dataz za kwanza kutoka ground Zero ambazo sina uhakika how good they are lakini ninaiamini the source, Kubenea na Ndimara, walikuwa wakitayarisha article nzito inayotabiri kusukwa kwa baraza jipya la mawaziri, ambalo liko tayari, ndani yake walikuwa waseme kuwa mkulu ameachwa pembeni na "Tyson" kuchukua nafasi yake, info zika-leak wakiwa bado wanatayarisha hiyo article, na kufika pasipotakiwa, and the rest of the story......!,

Bado tunaendelea kuzitafuta zaidi, zikipatikana hapa hapa JF!

Ahsante Wakuuu!

...mkuu hapo naona kuna nuclear bomb linakuja,tunasubiri!
 
hili la serikali kugharimia limekuja baadaye baada ya watu wa Baraza la Habari kuhangaika kutwa nzima kumsafirisha... Baada ya wao (mgonjwa na msindikizaji) ndipo serikali ikajikuta imeshapitisha uamuzi wa kufanya hivyo lakini initiative ni ya waandishi wenyewe.
 
wewe GT tunaomba evidence kwa maneno yako ,,kama unetumwa na mafisadi basi tujue tunashindana na wakinanani,,inasikitisha watu kama nyie kusupport watu kumwagiwa tindikali,,inaonyesha hata ubinadamu haupo kabisa,,hata kama alikuwa kwenye payroll bado hakutakiwa kupata adhabu hiyo waungwana ,,imagine ni ndugu yako wanamwagiwa tindikali ungejisikiaje,,

je unawez akutuletea hata sallar clip ya huyu mheshimiwa kuonyeshwa analipwa na mafisadi

kama kwenye uchaguzi tunawambia wananchi wale hela za mafisadi wapige kura chama kitannachoonekana kinafaa,,huoni na msemo wako tunakuwa tunawaingiza watu motoni,,,mimi bado nawaomba wanaforum HATA WAJE GT KUMI tupinge huu uhuni na uchafu aliofanyiwa ndugu yetu,,

mungu amponye na kurudi kwenye shuguli yake kama kawaida
 
PDIDDY

Naomba unionyshe ni wapi niliposuport KUBENA kumwagiwa Tndikali?

Its very simple unaweza ukaniquote niliyooandika hapo awali kisha uka highlight sehemu niliyosupport hilo

sidhani kama hiyo ni kaz kubwa

Quote:-

"Hapa piga ua lazima pana mkono wa akina MVI"

Wakuu heshima mbele, hatimaye nimepata dataz za kwanza kutoka ground Zero ambazo sina uhakika how good they are lakini ninaiamini the source, Kubenea na Ndimara, walikuwa wakitayarisha article nzito inayotabiri kusukwa kwa baraza jipya la mawaziri, ambalo liko tayari, ndani yake walikuwa waseme kuwa mkulu ameachwa pembeni na "Tyson" kuchukua nafasi yake, info zika-leak wakiwa bado wanatayarisha hiyo article, na kufika pasipotakiwa, and the rest of the story......!,

Bado tunaendelea kuzitafuta zaidi, zikipatikana hapa hapa JF!

mukulu hiyo article ya kutabiri kutemwa kwa mvi ilitoka alihamisi iliyopita [last issue] na waliahidi kutoa habari zaidi...

lakini hii kitu lazima inajulikana juu na mukulu anajua vijana wake wameharibu...hivi wewe ukiwa na kijana wako mtundu akapiga mtu huko ...si itabidi uingie gharama za kumtibia huyo mtu aliyepigwa...thats what is happening...amekua na huruma gani ya ghafla kumpeleka kabeneya india tena bila hata kuombwa ..ilhali yule masikini emmanuel aliyepasuliwa kichwa badala ya mguu..iliwachukua karibu mwezi mmoja kukubali maombi ya ndugu na wadau kumpeleka india kwa matibabu zaidi....nafikiri wameona bora wamkimbize india haraka haraka ili kumuondoa mbele ya macho ya hadhara na jamii isahau kidogo kumuongelea...wewe unafikiri angeendelea kuugulia hapa kama emmanuel kwa mwezi mzima ingekuwa na repuccation gani kwa PR ..ya mafisadi....sasa muhimu waandishi na watanzania msimsahau kabeneya na wahanga wengine kama yeye......ndimara[mbunge wa zamani nccr] aliyebaki nyumbani aendeleze libeneke....
 
Quote:-

"Hapa piga ua lazima pana mkono wa akina MVI"

Wakuu heshima mbele, hatimaye nimepata dataz za kwanza kutoka ground Zero ambazo sina uhakika how good they are lakini ninaiamini the source, Kubenea na Ndimara, walikuwa wakitayarisha article nzito inayotabiri kusukwa kwa baraza jipya la mawaziri, ambalo liko tayari, ndani yake walikuwa waseme kuwa mkulu ameachwa pembeni na "Tyson" kuchukua nafasi yake, info zika-leak wakiwa bado wanatayarisha hiyo article, na kufika pasipotakiwa, and the rest of the story......!,

Bado tunaendelea kuzitafuta zaidi, zikipatikana hapa hapa JF!

Ahsante Wakuuu!
ES
Mawazo yako hayana tofauti na baadhi ya watu wanaopenda kupata majibu ya haraka bila kutumia muda kutafakari.

Jana nilisikitika nilipoanagalia Taarifa ya Habari na leo niliposoma Tamko La BAVICHA,Mzee Mengi,Makunga,Sakina Datoo hawa nao niliona ni kwa kiwango gani walivokua wavivu wakufikiri pale walipo toa hukumu kabisa kua Kuvamiwa kwa kubenea kuna Uhusiano wa moja kwa moja na UANDISHI wake,hawa watu ktk matamko yao walitoa hukumu kabisa kua kubenea amehujumiwa,kama ilivo kwa JOHN MNYIKA ( ingiwa najua tatizo lake ni uanaharakati,na tabia yao nikutafuta majibu rahisi)kudai kua vijana waliofanya tukio wametumiwa na mafisadi so wasitumike, bila kukumbuka kua mmoja alie kamatwa ana miaka 65 sijui kama ni kijana.

RIOBA ktk waongeaji alikua more objective na hakutaka kuhukumu ingawa Prof wangu Shivji nae jana kidogo nilijiuliza is it uzee unamuanza au ni bcs nae ameaminishwa kua kubenea amehujumiwa na mafisadi, Mengi yeye simshangai ni mzee wa kuchukua oppprtunities na always hua ni mtu wa kukurupuka.

JANA NILIULIZA MASWALI HAPA JF KUA KAMA KWELI KUBENEA AMEKUA ANAKUMBANA NA VITISHO (JE ALISHINDWA KUWEKA ANGALAU MLINZI WA KIMASAI KTK OFISI YAKE? PIA WHY WATU WANAKIMBILIA KUDAI KUA AMEHUJUMIWA BCS YA UANDISHI WAKE NA TUSIJIULIZE MASWALI MADOGO MAY BE KADHULUMU,KACHUKUA MKE WA MTU,AU WALIOVAMIA NI VIBAKA,OR NI MATEJA BCS HATA SILAHA ZAO NI MAARUFU MIONGONI MWA MATEJA,etc)

Watanzania wengi wanataka kuaminishwa kwamba tukio hilo ni hujuma kwa vigezo kua amekua akipata sms za vitisho,or ametaka kugongwa naGARI makusudi,hivi kwa siku ni wangapi wanapoteza maisha kwa kugongwa na magari either kwa uzembe wa DEREVA au wa mtumiaji wa njia mwenyewe,why tusijiulize kubenea inawezekana alikua amelewa akashindwa kufata sheria za barabarani or dereva aliemkosa alikua amelewa mzembe.

Nachoomba kuptia Forum hii WAANDISHI walifanye tukio hili kama matukio mengine mpaka pale uthibitisho utakapo kua kweli ni hujuma.

Ni hatari kwa jamii kuwapa nafasi watu kama SAKINA DATOO wa SUNDAY CITIZEN bcs mara nyingi amekua ni mtu ambae ni opportunist wanao fanya nae kazi wanlijua hilo anapotoa kauli zake mara nyingi hana Facts,na anakua ni mtu wa kuongozwa na HISIA zaidi,MAKUNGA jana alionyesha kitu cha ajabu kua waandishi wanafanya uchunguzi kabla ya kuandika (theme ya maongezi yake) lakini nilishangaa je kabla ya kuongea alikua amefanya uchunguzi wa kiwango GANI? MAMA TAMWA sijashangaa ni NATURE ya kazi yake wana harakati mara nyingi ni watu hatari sana bcs to them kilakitu ni opportunity kama alivo wahi kusema PROF WANGU MAREHEMU CHACHAGE (TO TRUST ACTIVIST IS NOT SAFE AS TO TRUST REVOLUTIONIST)

Wana JF inawezekana ni kweli kahujumiwa,nani hatujui thats why TIBA anafanya uchunguzi tusubiri matokeo tujaribu kuangalia jambo la kubenea kwa mapana zaidi isije tukaifanya FANI YETU YA HABARI NI CHAKA LA MAOVU kila mwandishi akiguswa basi tu conclude hujuma bcs ni mwandishi ifike mahali tuliangalie jambo kwa UHALISIA WAKE kuliko HISIA.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Mkuu PM,

Heshima mbele, tunaendelea kutafuta more dataz, lakini this one so far bado ina stand, maana tulisema kuwa kule Ngorongoro, zile siku saba, baraza lilikuwa linapanguliwa, sasa amerudi mjni tu amemwagiwa mtu acid kwa kutabiri baraza jipya, ninakubaliana na wewe kuwa kumkimbiza India ni msaada na siasa pia!

Shame kwa wanaohusika, lakini it about time sasa Muungwana, akawatosa hawa nasikia mhezo sasa umefika mwisho na it is coming!
 
Quote:-

"Mawazo yako hayana tofauti na baadhi ya watu wanaopenda kupata majibu ya haraka bila kutumia muda kutafakari."

Wewe tafakari halafu uweke hapa analysis bila facts, I do not believe in that mkuu, nimetafuta dataz na hizo nilizoweka ninaziamini 100%, huzipendi I am not very sorry kama huna dataz kaa pembeni mkuu utaletewa, maana ndio kwanza tumeanza, na zinakuja, hili sio gazeti na uzushi sio sifa inayoifanya JF kusifika dunia nzima, mikataba ya Buzwagi na BOT, haikuwa uzushi ilipowekwa hapa, sasa kilichobadilika leo hapa JF ni nini mkuu?

Inaonekana huna dataz, basi subiri tu utawekewa hapa!, Mkuu PM lete dataz hapa tukate mzizi wa fitina!
 
That's why I respect you,Mzee ES.You always hit the bull.Tupe dataz mzee,achana na hao wanaoandika fikra zao bila kuwa na facts.Wanaweza kummwagia Tindikali Kubenea lakini JF bado ina watu kama wewe wenye data za jikoni.
 
Tangu jamaa kamwagiwa tingikali ambayo naamini ilikuwa too much neutralized, ndio maana haijamchubua hata ngozi, watu wamukuwa wakiolaani sana hapa but mimi naamini amepewa zawadi yake ya mwaka mpya na wale aliowachafua
 
Machivelle Niccolo alisema kuwa kiongozi bora ni yule ambaye ana ulimi mtamu lakini matendo makali kama upanga,awe tayari kuuwa mtu yeyote kwa maslai ya nchi yake.Kwa maana kiongozi legelege ahatarishi maisha yake peke yake bali maisha ya taifa zima.
 
Tangu jamaa kamwagiwa tingikali ambayo naamini ilikuwa too much neutralized, ndio maana haijamchubua hata ngozi, watu wamukuwa wakiolaani sana hapa but mimi naamini amepewa zawadi yake ya mwaka mpya na wale aliowachafua
Mkuu, lakini zawadi yenyewe inaonekana ilidhamiria kummaliza... Aliwachafua eh?
 
Chuma
DUH hizi habari zikoje? maana Halisi hua anakuja na data za mashaka...VP halisi ile kesi yako na TRA kule ARUSHA imeisha maana nshasahau kabisa,...

Invincible

Anayekuja na data za mashaka(controversial) nadhani ni Hasara. Namwiminia sana Halisi(Genuine).

Pole bwana mhariri. Wish you quick recovery.

Ahsante Invincible kwa majibu yako
 
Mkuu PM,

Heshima mbele, tunaendelea kutafuta more dataz, lakini this one so far bado ina stand, maana tulisema kuwa kule Ngorongoro, zile siku saba, baraza lilikuwa linapanguliwa, sasa amerudi mjni tu amemwagiwa mtu acid kwa kutabiri baraza jipya, ninakubaliana na wewe kuwa kumkimbiza India ni msaada na siasa pia!

Shame kwa wanaohusika, lakini it about time sasa Muungwana, akawatosa hawa nasikia mhezo sasa umefika mwisho na it is coming!

EL naye alikwenda huko alikokua amejificha mkuu na Membe naye aliitwa huko, nadhani labda waliyamaliza, ama walipanga mikakati mipya.
 
Back
Top Bottom