Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,589
- 28,754
cha ajabu hawa jamaa watafikishwa mahakamani kesho hasubui..ila kina mkulo mpaka leo wanapeta kitaaa
Bulesi, yule ni Mabhare Matinyi alikuwa mhariri Mkuu wa gazeti la Majira bado yuko DC. Hiyu ni Masiyaga Matinyi yeye yuko Rai na pia kuna Matinyi mwingine TBC-1!.
Sasa Mkuu Pasco naomba kuuliza, hivi nyie waandishi wa Magazeti, Radio na Tv hamlipwi mishahara? Mbona mnapenda sana hongo (Vibahasha vya Kaki)? Hamuandiki habari bila ya Vibahasha na msipopewa habari haitoki kwenye Magazeti au kwenye TV's. Hivi Taaluma yenu imeegemea sana kwenye vibahasha kuliko kwenye habari zenyewe.
Pasco kwani hamuwezi kufanyakazi bila ya kupewa Vibahasha vya kaki? Hivi waajiri wenu hawawalipi mpaka muombe uccm?
Kwa huyo kukamatwa kuchukuwa mulungula haishangazi kabisa -- yeye ni kinara pale New Habari.
Mwaka juzi pia alipokea rushwa kutoka kwa jamaa mmoja ambaye baadaye alikuja kulalamika pale lakini Muhingo Rweyemamu aliyekuwa Mhariri Mkuu (ME) alimkingia kifua na kurudishwa kazini baada ya kusimamishwa kwa muda.
Wawili hao, pamoja na mwingine aitwaye Munyuku ambaye sasa yuko gazeti lingine liitwalo Tabibu ndiyo walikuwa vinara wa milungula pale New Habari.
Duh kumbe Innocent Munyuku naye alikuwa kinara? Hii rushwa limekuwa donda ndugu yaani mtu unatoka Sinza kwenda hadi Monduli kudai rushwa ya millioni moja? Hizo gharama za kwenda huko si zinazidi
Sasa Mkuu Pasco naomba kuuliza, hivi nyie waandishi wa Magazeti, Radio na Tv hamlipwi mishahara? Mbona mnapenda sana hongo (Vibahasha vya Kaki)? Hamuandiki habari bila ya Vibahasha na msipopewa habari haitoki kwenye Magazeti au kwenye TV's. Hivi Taaluma yenu imeegemea sana kwenye vibahasha kuliko kwenye habari zenyewe.
Pasco kwani hamuwezi kufanyakazi bila ya kupewa Vibahasha vya kaki? Hivi waajiri wenu hawawalipi mpaka muombe uccm?
Then both of them are really good kwenye fani!.huyo wa merikani na huyu aliyekamatwa ni ndugu.
BigMan, umenichekesha, news is free!. Ila waandishi lazima wawezeshwe ili waweze kuzifikia hizo news!.pasco mbona kakujibu vizuri sana hivi wewe ukienda katika kongamano,warsha na mkutano mbona unalipwa posho kwani huna mshahara ? ebu tuangalie kwa mawakili kabla ya kuwaona siku zote lazima wawe na tozo la ushauri nenda kwa madaktari kwa nini waandishi nao wasikupige fedha kwa huduma wanayotoa ?
Wanabodi,
Kuna hoja ya waandishi wa habari kupokea bahasha ambayo inatafsiriwa vibaya kama rushwa/hongo/chochote
Mada itakuwa kwenye vipengele kadhaa!.
1. Bahasha za Waandishi ni nini?
2. Jee kuna bahasha aina ngapi?
3. Jee kuna uhalali wa Waandishi kupokea bahasha hizo?.
4. Jee ni bahasha zipi sio rushwa?
5. Jee ni bahasha zipi ni rushwa?
6. Jee Bahasha za "asante"-Takrima nayo ni rushwa?.
7. Jee ni kweli kwa waandishi kupokea bahasha ni kuendekeza njaa?
8. Kuibuka kwa kada ya Makanjanja kufukuzia Bahasha?.
9. Jee ni waandishi ndio waoomba hizo baasha au sources ndio huzitoa wenyewe?.
10. Pasco wa JF na msimamo wa kutetea bahasha!.
Bahasha za Kuzuia Habari Kutoka-Hii ni Rushwa!.
Kuna bahasha za kuzuia story fulani isitoke!, hizi ni bahasha zinazotembezwa kwa waandishi ili kuzuia story fulani isitoke ili kulinda maslahi fulani au jina la mtu fulani lisichafuke!. Hii inahusisha kuitwa kwenye tukia na kutake a good care ya waandishi ili wasiripoti kabisa kuhusu tukio fulani!. Hii mara nyingi huusisha ama scandals au black mail. Mfano kigogo mmoja mheshimiwa sana, ameshitakiwa kwa kosa la kufumwa akifanya mapenzi na Changudoa ufukweni. Story hiyo ikitoka itamvunjia heshima sana mzee, hivyo anakata fungu fulani la kutakata la kuwatake care waandishi wote wanaoripoti toka mahakamani ili kesi ya kigogo ikitajwa waipotezee. Au Wafanyakazi wa kiwanda fulani wamegoma, wewe ni mwandishi unakwenda kucoiver story, unaanza na mgomo, ili kubance story, lazima uwatafute na management, ile kufika management, unakuwa well taken care off, uamuzi ni wako, ulinde heshima ya taaluma yako na ulale njaa, ama uuze utu wako jioni ukakae viti virefu, uamuzi huwa ni individual!.
Blackmail na Framing ni rushwa mbaya kabisa!
Hii inahusisha waandishi kupata habari mbaya kuhusu vigogo fulani, mwandishi ku solicit money ili kuzuia kumlipua muhusika huyo!. Au umezinyaka picha za utupu za kigogo fulani unamuonyesha na kudai kiasi cha fedha ili uzizichapishe!. Kesi ya rafiki yangu Jerry Muro ili fall kwenye kundi hili!.
Sambamba na blackmail, kama polisi wanaweza kukuisingizia kesi ndivyo waandishi wa habari wanavyeweza kuku frame na kukuandikia habari mbaya za kutunga, mfano wa alichofanyiwa Dr. Salim Ahmedv Salim na gazeti la Mtanzania ili kumbeba JK awe mgombea!,
Saa hizi usiku umekuwa mkubwa sana, kesho nitaendelea na hizi bahasha chafu ambazo ndizo rushwa na ni za kuogopwa kama ukoma!.
Kwa huyo kukamatwa kuchukuwa mulungula haishangazi kabisa -- yeye ni kinara pale New Habari.
Mwaka juzi pia alipokea rushwa kutoka kwa jamaa mmoja ambaye baadaye alikuja kulalamika pale lakini Muhingo Rweyemamu aliyekuwa Mhariri Mkuu (ME) alimkingia kifua na kurudishwa kazini baada ya kusimamishwa kwa muda.
Wawili hao, pamoja na mwingine aitwaye Munyuku ambaye sasa yuko gazeti lingine liitwalo Tabibu ndiyo walikuwa vinara wa milungula pale New Habari.
Sordo, Jamaa alikuja Arusha kwa special assignment ya kuwalipua Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro!. Kama ni kweli anakula pesa ya Mwarabu na amemjengea nyumba, haiwezekani tena mtu huyo huyo aukate mti alioukalia!. Soma Rai la kesho uone alivyowalipua!.
Watanzania hatuna roho mbaya!. Kumuombea mwenzako mabaya kwa tuhuma tuu ni roho mbaya!. Acha roho mbaya yako!. Watu walikwapua Bilioni 40 za Kagoda na wanapeta!, itakuwa tuhuma za rushwa ya pesa mbuzi hiyo?!.
Japo nimesikitishwa na kuhuzunishwa, naombea kesi hiyo iishe kamanda wetu arudi mstari wa mbele wa mapambano!.
Mkuu Mzalendo, sio kweli kuwa mimi ni mpenda hivyo vibahasha bali ndie mgawaji wa hivyo vibahasha!. Naomba tafuta muda utembelee hapa www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-...a-sio-kila-bahasha-ni-rushwa-pasco-wa-jf.html ili tuambue kuwa siyo kila bahasha ni rushwa!. Mimi ni mtetezi wa haki za waandishi, kama wajumbe wa vikao, semina, warsha, kongamano au mikutano, wanalipana sitting allowance na kupeana trasport, why not waandishi?.