Mhariri Rai Matinyi anaswa kwa Rushwa Monduli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhariri Rai Matinyi anaswa kwa Rushwa Monduli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngurdoto, Jun 14, 2012.

 1. n

  ngurdoto Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wana JF,

  Taarifa za uhakika ambazo nimezipata hivi sasa kutoka chanzo cha uhakika zinasema Mhariri wa Rai Masyaga Matinyi amekamatwa kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh. M 1.8, Matinyi amekutwa na kashfa hiyo wilayani Monduli akiwa na wenzake wawili.

  Chanzo hicho kinasema, rushwa hiyo waliiomba kutoka kwa mfanyakazi wa TANESCO Monduli ambaye hana sifa za kuwa na nafasi ya kikazi aliyonayo hivyo, walimuomna fedha hizo ili wasiandike habari hiyo na kama angegoma kutoa basi stori hiyo ingeandikwa.

  Hata hivyo mfanyakazi huyo aliomba apunguziwe na atangulize Sh. 200,000 kumbe tayari alikuwa ameshaweka mtengo na PCCB ambao walifanikiwa kuwanasa wote wakiwa ndani ya ofisi ya mfanyakazi huyo.

  Kwa sasa Matinyi na wenzake Samson Mwita (32), Bora Yunus Bidiga wanashikiliwa TAKUKURU ARUSHA kwa mahojiano zaidi.


  Nawasilisha wadau
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  wanashikiliwa siyo "wanashikiriwa".
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kumbe waandishi ndio mlivo tena wahariri lol kwa njaa zao wanaficha uozo
  huo mfanyakazi licha ya kuwakamatisha lkn bado atimuliwe kazi kwa kutokuwa na sifa
   
 4. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Wanajamvi taarifa zilizojiri toka Monduli jioni hii ni kwamba Masyaga Matinyi ametiwa Mbaroni na maafisa wa PCCB kwa tuhuma za kuomba rushwa ya million 1 kwa sasa bado anahojiwa; tutawajuza zaidi baadaye
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  He mwandishi analamba rushwa tena? Ameomba toka kwa nani au halmashauri?
   
 6. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ameomba kwa afisa wa halmashauri anayedaiwa kufoji vyeti ila kamskisha fedha moto lk 2 tu mwandishi alikuwa andai ape we million I
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo katanguliziwa laki mbili za moto kadaka naye kadakwa! Ka nchi haka bwana kwa rushwa kapo juu. Rushwa kila mahala: Bungeni, waandishi, wabunge, wasomi, wanasiasa, wapinzani, watawala, nk.
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hawa makanjanja wa Tanzania wote ni njaa tu!! Pasco unaona jamaa zako wanavyoaibisha taaluma!!
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  njaa itaumbua wengi!
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa huyo kukamatwa kuchukuwa mulungula haishangazi kabisa -- yeye ni kinara pale New Habari.

  Mwaka juzi pia alipokea rushwa kutoka kwa jamaa mmoja ambaye baadaye alikuja kulalamika pale lakini Muhingo Rweyemamu aliyekuwa Mhariri Mkuu (ME) alimkingia kifua na kurudishwa kazini baada ya kusimamishwa kwa muda.

  Wawili hao, pamoja na mwingine aitwaye Munyuku ambaye sasa yuko gazeti lingine liitwalo Tabibu ndiyo walikuwa vinara wa milungula pale New Habari.
   
 11. h

  hoyce JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hapo issue sio njaa, ni tabia ya mtu. Kuna watu ni matajiri sana lakini walarushwa wakubwa tu.
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ujumbe si umekufikia? Ama umekosa cha kucomment ukaona bora uweke nonsense hapa
   
 13. S

  Sojochris Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  You are very right mkuu,mikataba mibovu yote Tanzania imesainiwa na wenye njaa? Wale wanaosaini mikataba ya kishenzi kuwaumiza wananchi tena wanasainia Hotelini na muhuli uliobebwa mfukoni nao wana njaa? Migodi yetu,maliasili na rasilimali kibao zinawekwa Rehani kiajabuajabu tena na watu walioaminiwa na wananchi nao ni njaa?

  Hadi mbunge wao anaomba rushwa na kukamatwa na vidhibiti nayo ni njaa?

  Tanzania is all corrupt from top to bottom so hao wameiga kwa mabwana zao sema dau lao dogo na wameshika makali
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ccm mmeendekeza rushwa mpaka mmewaambukiza waandishi wa habari
   
 15. A

  Arusha Leo Senior Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhariri na gazeti la Rai ,Masyaga Matinyi ametiwa mbaroni na takukuru kwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 200,000 kutoka kwa kigogo wa tanesco wilayani Monduli,kwa sasa ameletwa na anasota makao makuu wa takukuru Arusha
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Kiukweli mimi binafsi nimesikitishwa na hii kadhia kumkuta Masiaga Matinyi kwa sababu huyu ni miongoni mwa waandishi jembe wa ukweli.

  Waandishi kama mimi huitwa "wapiganaji" lakini Matinyi ni mmoja wa waandishi makamanda kama alivyo Manyerere Jacton. Hawa hawaendekezi njaa!.

  Matinyi ni rafiki wa karibu wa Joseph Kabila walisoma wote tangu primary mpaka sekondari na mara Joseph alipopata ulaji ilitegemewa angeachana na fani, lakini kwa vile ni mwandishi wa wito, aliendelea na fani.

  Mimi kupitia PPR huwa nafanya PR hivyo Matinyi akiwa Arusha amepita anga zangu fulani huko Arusha na mimi binafsi nimezungumza nae sana kuhusu ulipuaji wake na alishikilia msimamo wa kusimama kwenye fani kwa kufuata msimamo wa "no compromise no surrender!" Sasa ninaposikia mtu wa msimamo kama huyu kuja kuaibishwa na pesa mbuzi ni lazima nisikitishwe na kuhuzunishwa!.
   
 17. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waandishi wa habari wengi ndivyo walivyo.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Siku nyingine mtakuwa makini zaidi katika kutukuza lugha yetu ya adhim iliyotokana na lugha bora duniani ya Kiarabu.
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Pasco, kuna mwandishi mmoja alikuwa anaandika makala toka Marekani hasa Washington D.C. alikuwa na jina kama hili la Matinyi; je ndio huyu aliyepatwa na balaa huko Monduli?
   
 20. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rushwa kwa waandishi wetu zinaitia kinyaa taaluma yao.

  Nakumbuka jinsi 'vijana' wa Habari Corp. walivyokula mlungula na kuanza kutukwepa ènzi hizo. Sishangai kama leo wamenaswa! 'Vijana' wa Business Times (enzi hizo) wao ndo walikuwa kwa kila 'stori' wanazozizuia kuzitoa, wakilipwa wanakuja kutushukuru kwa kuwasababishia ulaji. Ilituuma sana hasa pale tulipokuwa Habari Maelezo na 'kreti' ya soda tuliwanunulia kama tulivyoambiwa lakini walivyotoka pale wakaenda kula mlungula kwa 'adui' wakasepa na hawakugusia suala hilo. Lakini bado kulikuwa kuna baadhi ya media zlizokuwa na uadilifu
   
Loading...