Japo sijafanya utafiti wa undugu wa mbali, Tido ni mtoto wa Mchungaji Daniel Mhando wa Anglican Chang'ombe. Mdogo wake ni mwandishi wa habarui na mtangazaji Jane Mhando yuko SABC Africa anaishi Kusini.
Neema alijiunga TBC hata kabla ya ujio wa Tido. Kwa upande wangu nadhani ni majina tuu, au Tanga line. Ila pia twende mbele tukirudi nyumba, kana ni ndugu jamaa ama marafiki, wanauwezo wa kazi, hawajabebwa kuingia TBC, sithani kama kuna ubaya wowote.
Angalizo, watu wa Tanga Line na ukanda wa pwani mara myingi hutokea kuwa watangazaji wazuri kwa lafudhi nzuri Tukianzia na
Tido Mhando- Tanga line-TBC Boss
Sekioni Kitojo-Tanga line-DW-Ujerumani
Ali Atasi-Tanga line-Radio Japan
Eraston Mbwana-Ujereumani
Abdalah Mbamba-Umoja wa Mataifa
Marriam Shamte-VOA
David Wakati-Zenji-Boss wa RTD Mstaafu
MohameD Dahman-Zenj -Ujerumani
Aboubakari Liongo-Tanga Line-Ujerumani,
Susan Mungy-Tanga line-BBC-TBC
Maulid Kitenge-Tanga line-Radio One
Eshe Muhidin-Tanga line-TBC Taifa
Abdul Masudi-Tanga line (RTD)
Philip Ciprian -Tanga line Clods radio/tbc
Hawa ni wachache tuu niliobahatika kuwakumbuka, nikifanya uchimbuzi, utakuta Tanga line ni wengi kwenye Utangazaji kama walivyo Chagga line kwenye mambo ya pesa ukianzia na TRA, walivyo Kurya line Jeshini, Nshomile kwenye kazi za kisomi etc.The list is long, long long, haina maana makabila mengine hawauwezi utangazaji bali Watanga ndio waliobobea zaidi.