Mhando amezusha hoja ya kufikirisha mahakama zetu. Hii hoja itafanya hata kesi ya msingi isahaulike. Na Kama mawakili wa serikali wali frame charges zao kwamba Mhando alimpendelea "MKE" wake kumpatia tenda itakuwa imekula kwao. Na kama hakuna official documents i.e marriage certificates (kwenye ofisi za vizazi na vifo) ndio itakuwa vigumu kabisa ku prove Eva ni mke wa Mhando. Kwasababu serikali itategemea ushahidi wa Mhando na Eva, ambao wao tayari wanakana sio MKE NA MME! Kweli ukishangaa ya Balali, bado ya akina Mhando.
Kama ni hivyo kwanini hati ya mashtaka isingeandikwa alimpa tenda hawara na sio kama ilivyoandikwa sasa kuwa alimpa tenda mkewe.Mkuu asante kwa sababu wewe umenielewa...
Mantiki ya swali langu hapo juu kulingana na mtoa mada ni hii.... Kama anadai sio mkewe na ni mpangaji wake, ina maana alizaa na mpangaji wake hivyo basi wana mahusiano ya kiuhawara. Ndio sababu iliyompelekea kumpa tenda kwa sababu ni hawara yake..
Kwi kwii Mke alisemaje pale alipokanwa hadharani mahakamani? Kama Eve naye amekubali/atakubari kirahisi, hiyo ina implication kubwa, baadaye katika mgawanyo wa mali in case of anything. Eve anaweza huko usoni asipate kitu kwenye mali za Mhando kama ataachia hili liende hivi hivi na mahakama iamue kwamba Eve kweli sio Mke wa Mhando. Hii inanikumbusha kesi ya jamaa mmoja aliyefunga ndoa "fake" na mwalimu mmoja kwa kusudi la kumsaidia ahamie shule za mjini. Bahati mbaya yule bwana akafariki, yule mwalimu aliyefunga ndoa "fake" na huyo jamaa akajitokeza baada ya kifo akidai mgawanyo wa mali, kwamba na yeye ni mke halali wa ndoa wa marehemu kwa kuonesha marriage certificate!
Hata kama wana watoto, sio kila mtu unayezaa naye ni mkeo. Cheti cha ndoa kiko wapi?
mkuu hebu kaa chini uteletee mchanyato kwa kina,.
Iweje ukurupuke na habari nyeti namna hii?
khaa!! Kwani Eve ni mchagga???Kwi kwii Mke alisemaje pale alipokanwa hadharani mahakamani? Kama Eve naye amekubali/atakubari kirahisi, hiyo ina implication kubwa, baadaye katika mgawanyo wa mali in case of anything. Eve anaweza huko usoni asipate kitu kwenye mali za Mhando kama ataachia hili liende hivi hivi na mahakama iamue kwamba Eve kweli sio Mke wa Mhando. Hii inanikumbusha kesi ya jamaa mmoja aliyefunga ndoa "fake" na mwalimu mmoja kwa kusudi la kumsaidia ahamie shule za mjini. Bahati mbaya yule bwana akafariki, yule mwalimu aliyefunga ndoa "fake" na huyo jamaa akajitokeza baada ya kifo akidai mgawanyo wa mali, kwamba na yeye ni mke halali wa ndoa wa marehemu kwa kuonesha marriage certificate!
Kuishi pamoja inaweza kuwa na maana pana. Vipi kama hawakuwa wakilala chumba kimoja...
Kaka hiki kitanzi kilimnasa katibu, kama na wewe unamuhukumu rejea za mahakama zitaleta utata mkubwa zaidi bora tuachie huko huko kwa pilato watu mpaka wana watoto lakini wanaruka kimanga.