Mhando amkana mkewe mahakamani

Mhando amkana mkewe mahakamani

Naomba kuliza wana jamvi...Kwani hawana watoto??

Mwanaume kuzaa na mwanamke hakuwafanyi wawe MME na MKE. A prime example ni mimi, nilizaa mtoto wa "majaribio" wakati ule wa ujana wangu, lakini huyo msichana/mwanamke sio mke wangu.
 
Mpangaji wake kwenye nyumba ya Tanesco? Uganda avenue 98??
 
Ha haaa!, Lakini sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inatambua mke wa ndoa katika sehemu tatu,kuwa na watoto,kuishi ndani ya nyumba kwa na watu kutambua kuwa mke walo,ndoa ya kimila,na kukaa na mwanamke kwa zaidi ya miezi mitatu.ndg yangu aliishi na hawara tu miezi mitatu skimpikia,walipoachana,akaenda kukana mahakamani kuwa sio mke wa ndoa lakini huyo dada alisema nimekuwa nae siku zote nikimpikia hivyo mme wsngu.Labda kwa kuwa tumeamua kuwa mafisadi,HAFUNGWI MTU HAPA!!!
 
Chezeya adha ya lupango Mkuu!! hukawii kumkana mkeo!!!!! Lakini pagumu hapa pa Mhando kumkana mkewe. Kama wana watoto basi DNA zitapimwa ili kuangalia wao ni wazazi wa hao watoto au la. Na kama ikithibitishwa kwamba ni watoto wao basi hili la kumkana mkewe waliyeishi naye miaka mingi litatupwa kule.

...bonge la trick,kwani definition ya ndoa/mke ni nini ? Kama walikuwa wakiishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili tayari ni mke na mume...
 
Mkuu maelezo hayo yote (kama hakuna official documents) kwamba alikuwa anampikia Mhando, kwamba walikuwa wanashiriki tendo la ndoa etc anayetakiwa kuyatoa mahakamani ni Eva, ambaye naye kwa bahati nzuri/mbaya anakubari kwamba Mhando sio mme wake.
 
Hapo ndipo umuhimu wa usalama wa taifa unatakiwa ufanye kazi,kwani nani hajui kama eva mumewe ni mhando mpaka wakataane wakati wa kesi
 
Chezeya adha ya lupango Mkuu!! hukawii kumkana mkeo!!!!! Lakini pagumu hapa pa Mhando kumkana mkewe. Kama wana watoto basi DNA zitapimwa ili kuangalia wao ni wazazi wa hao watoto au la. Na kama ikithibitishwa kwamba ni watoto wao basi hili la kumkana mkewe waliyeishi naye miaka mingi litatupwa kule.

Wakuu Bobuk na washwa washwa swali langu lililenga hii comment
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndipo umuhimu wa usalama wa taifa unatakiwa ufanye kazi,kwani nani hajui kama eva mumewe ni mhando mpaka wakataane wakati wa kesi

Mkuu, mahakamani ahakuna habari ya kujua, kuona, kusikia au kuambiwa----mahakamani zinatakiwa documents tu---ziwe written and signed, audio, audio-visual, nk. Kama huna ushahidi huo kesi imeisha na mtuhumiwa ataachiliwa huru.
 
Ha haaa!, Lakini sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inatambua mke wa ndoa katika sehemu tatu,kuwa na watoto,kuishi ndani ya nyumba kwa na watu kutambua kuwa mke walo,ndoa ya kimila,na kukaa na mwanamke kwa zaidi ya miezi mitatu.ndg yangu aliishi na hawara tu miezi mitatu skimpikia,walipoachana,akaenda kukana mahakamani kuwa sio mke wa ndoa lakini huyo dada alisema nimekuwa nae siku zote nikimpikia hivyo mme wsngu.Labda kwa kuwa tumeamua kuwa mafisadi,HAFUNGWI MTU HAPA!!!

Sawa. Ushahidi wa haya uko wapi? Unaweza kuutoa mahakamani?
 
Ngoja tusubiri tusikie jibu la hili swali, na kama itathibitika wana watoto watamtwisha kosa lingine la kutaka kuidanganya mahakama.

Naomba kuuliza wana jamvi...Kwani hawana watoto??
 
Mhando amezusha hoja ya kufikirisha mahakama zetu. Hii hoja itafanya hata kesi ya msingi isahaulike. Na Kama mawakili wa serikali wali frame charges zao kwamba Mhando alimpendelea "MKE" wake kumpatia tenda itakuwa imekula kwao. Na kama hakuna official documents i.e marriage certificates (kwenye ofisi za vizazi na vifo) ndio itakuwa vigumu kabisa ku prove Eva ni mke wa Mhando. Kwasababu serikali itategemea ushahidi wa Mhando na Eva, ambao wao tayari wanakana sio MKE NA MME! Kweli ukishangaa ya Balali, bado ya akina Mhando.

Na hiki ndicho kinamfanya hata FISADI Chenge (Mzee wa Vijisenti) aendelee kula bata mtaani. Kila mtanzania anajua fika kwamba Chenge anamiliki fedha haramu lakini ushahidi uko wapi wa kumfungulia mashitaka mahakamani? Chezea USHAHIDI wewe?
 
Ngoja tusubiri tusikie jibu la hili swali, na kama itathibitika wana watoto watamtwisha kosa lingine la kutaka kuidanganya mahakama.

Mkuu asante kwa sababu wewe umenielewa...

Mantiki ya swali langu hapo juu kulingana na mtoa mada ni hii.... Kama anadai sio mkewe na ni mpangaji wake, ina maana alizaa na mpangaji wake hivyo basi wana mahusiano ya kiuhawara. Ndio sababu iliyompelekea kumpa tenda kwa sababu ni hawara yake..
 
Mhando amkana kortini Eva Mhando kuwa siyo mkewe
Na Beatrice Shayo
14th June 2014

mhando.jpg
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (Tanesco), Bw William Mhando.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (Tanesco), William Mhando, amemkana Eva Mhando, anayedaiwa kumpatia zabuni ya usambazaji wa vifaa vya ofisini vya shirika hilo kuwa si mkewe.

Alikana mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.

Alipinga kuwa Eva si mkewe baada ya Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, kumsomea maelezo ya awali ya kesi inayomkabili pamoja na watu wengine watano akiwamo mkewe Eva.

Swai aliwasomea Mhandisi Mhando, Eva ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Santa Clara Supplies, inayodaiwa kupewa zabuni ya kusambaza vifaa hivyo. Wengine ni wahasibu wafawidhi wa Tanesco, France Mchalange na Sophia Misindai pamoja na Ofisa Ugavi, Naftali Kisinga.

Mbele ya Hakimu Mkazi Moshi, wakili huyo alidai kampuni hiyo ilishinda zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi vyenye thamani ya Sh. milioni 884 na kwamba Mhando akiwa na wadhifa huo alisaini mkataba kwa upande wa shirika hilo na mkewe Eva aliiwakilisha kampuni hiyo.

Swai alidai Mhando alijua kampuni ya Santa Clara inamilikiwa na familia yake, lakini alishindwa kuelezea maslahi binafsi wakati kampuni hiyo hiyo ilipoomba na kupewa zabuni hiyo. Alidai Eva na watoto wake walijaribu kuuza kampuni kwa mtu mwingine. Alidai Mhando alitumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kuelezea maslahi yake kwenye kampuni hiyo kwamba mkurugenzi wake ni mkewe na wanaye.

Swai alidai mshitakiwa huyo, pia alighushi nyaraka za uhamishaji wa hisa kuonyesha kwamba amehamisha hisa 200 ambazo kila moja ina thamani ya Sh. 10,000 kutoka kwa kampuni yake kwenda kwa Eveta John Shing'oma.
Alidai Eva aliwasilisha kwa Katibu wa Bodi ya Zabuni ya shirika hilo, ripoti ya ukaguzi wa fedha wa kampuni yake kuonyesha imeandaliwa na Finx Capital House.

Kadhalika alidai Eva akiwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo alijilipa Sh. milioni 31.7 kutoka shirika la umeme. Hata hivyo, baada ya kusomewa maelezo hayo, Mhando alikubali kwamba Eva alikuwa mwajiriwa shirika hilo.

Washitakiwa wengine nao walikubali kwamba walikuwa watumishi waTanesco na wajumbe wa kamati ya tathmini ya zabuni. Wakili Swai alisema Takukuru itawasilisha mashahidi 14 na vielelezo 18. Hakimu Moshi aliahirisha kesi hadi itakaposikilizwa tena Julai 29 na 30, mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE
 
Mkuu asante kwa sababu wewe umenielewa...

Mantiki ya swali langu hapo juu kulingana na mtoa mada ni hii.... Kama anadai sio mkewe na ni mpangaji wake, ina maana alizaa na mpangaji wake hivyo basi wana mahusiano ya kiuhawara. Ndio sababu iliyompelekea kumpa tenda kwa sababu ni hawara yake..

Amekana kwamba Eva sio mkewe na hakuwahi kuzaa naye. Utawalazimishaje watoto kwenda kupimwa DNA bila ridhaa yao (sheria hairuhusu) hata kama wanajulikana?
 
Kaka hiki kitanzi kilimnasa katibu, kama na wewe unamuhukumu rejea za mahakama zitaleta utata mkubwa zaidi bora tuachie huko huko kwa pilato watu mpaka wana watoto lakini wanaruka kimanga.

...bonge la trick,kwani definition ya ndoa/mke ni nini ? Kama walikuwa wakiishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili tayari ni mke na mume...
 
Chezeya adha ya lupango Mkuu!! hukawii kumkana mkeo!!!!! Lakini pagumu hapa pa Mhando kumkana mkewe. Kama wana watoto basi DNA zitapimwa ili kuangalia wao ni wazazi wa hao watoto au la. Na kama ikithibitishwa kwamba ni watoto wao basi hili la kumkana mkewe waliyeishi naye miaka mingi litatupwa kule.

Na wewe una kichwa kigumu! Ebu soma posts zilizotangulia kuhusu masuala ya ndoa.
 
Back
Top Bottom