Mhando amkana mkewe mahakamani

Mhando amkana mkewe mahakamani

Michepuko hiyo., ilianzishiwa kampuni, ikapewa zabuni., wakala bata kwa kwenda kushoto ~ kulia., sasa vinawatokea puani.. Si Mhando tu, wapo wengini nchi hii imeoza, ni ufisadi tu.
 
mbona issue nyepesi. Huyo Muhando aambiwe alete cheti cha ndoa yake. Mkewe aambiwe alete cheti cha ndoa yake(makazini huwa tunapeleka vyeti vya ndoa na vya kuzaliwa vya watoto kwa mafao flan flan). Kisha watoto waambiwe walete vyeti vyao vya kuzaliwa. Kisha wata cross check na ofisi ya vizazi na vifo na TANESCO HR data base. Kisha uchunguzi utaendelea toka hapo.
 
Good to go.
 
Kama hawajawahi kufunga ndoa watavipata wapi!! Labda watoto wapimwe DNA
 
kwani Eva mhando hawezi kuwa dadake ?
Ndio maana mkuu nikasema hapo juu,kutoa utata,mhando wa tanesco,eva mhando na watoto walete vyeti vyao vya ndoa na vya kuzaliwa kama walivyowahi peleka makazini/mashuleni long way back(kumbuka vyeti vya kuzaliwa vinaeleza majina ya mama,majina ya baba na majina ya mtoto. Vyeti vya ndoa vina majina halisi ya mke na mme). Na kumbuka,mhando alikua ni mwajiliwa wa siku nyingi tanesco hivyo kule mwanzoni asingekua na wazo la kupeleka vyeti feki kwani hata wazo la kuanzisha kampuni na mkewe halikuwapo.Na pia kule kazini asingepeleka vyeti feki vya kuzaliwa watoto wake kwani lengo huwa ni vimthibitishe yeye na mkewe ili apate mafao yake mbalimbali.Kinachobaki mna connect dots tu!.
 
Kama hawajawahi kufunga ndoa watavipata wapi!! Labda watoto wapimwe DNA
Ingawa simjui sana huyo mhando,lakini uzoefu unaonesha 90% ya wafanyakazi wa serikali au taasisi za umma huwa wanahakikisha wanafunga ndoa na kuwa na vyeti ili kujihakikishia mafao yalioainishwa ki sheria kwa wenye ndoa au watoto wao. Mhando alikua tanesco ambayo ni taasisi ya umma na masharti hayo yapo idara yao ya HR.
 
dah! yaani waendesha ashitaka wapeleke mahakamani dai kwamba eve ni mke wa mhando bila hata ya kuwa na vielelezo vya kuthibitisha dai linaloshikilia kesi! watakuwa watu wa ajabu sana, na kama ni hivyo sitashangaa wadau wengine wakidai waendesha mashitaka wamekula njama kuimaliza hii kesi.

Na ukosefu wa ushahidi huu (cheti cha ndoa) ndio utafanya kesi nzima ionekane baseless. Haya yote ni matunda ya serikali ya kifisadi ya CCM.
 
Duh!
Kwa hiyo watoto ni wa Mhando.
Then masilahi binafsi yanaanzia hapo kuwa Mhando angependa Watoto wake wafaidike kupitia Hawara wake.
Hapo upo?

USHAHIDI uko wapi?
 
Ikiwa upnde wa jamhuri watashundwa kuthibitisha kuwa eva ni mke wa muheshimiwa basi kesi ya msingi Imekufa....tehe tehe teheeee kweli Haki ipo mbinguni.

ndiyo maana yake....kutakuwa hakuna kesi hapo. na serikali itamlipa mhando mamilioni ya shilingi kwa kumsingizia uongo na kumpotezea muda mahakamani.
 
Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TANESCO, William Mhando, amemkana mkewe Eva Mhando mahakamani kwa kukataa kwamba Eva sio mke wake. Mkurugenzi huyo amefunguliwa kesi ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na moja ya mashtaka yanayomkabili ni kula njama za kufanya ufisadi akishirikiana na mkewe, Eva, anayedaiwa kupewa zabuni ya mabilioni ya walipakodi kinyemela.

Source: Raia Tanzania.

MAONI YANGU
Naona wakili wa mhando ameamua kufanya hii kesi iwe complicated na kuchukua muda mrefu huku fisadi Mhando akizidi kutafuna fedha za umma alizojichotea. Haya ndio matatizo ya mawakili 'waganga njaa' tuliokuwa nao ktk nchi hii. Mawakili kama hawa hawana hata chembe ya uzalendo.

Mpaka vyeti vya ndoa vije vipatikane ili kuthibitisha uanandoa kati ya Mhando na Eva, kesi itakuwa imemaliza karne kabla ya kuamuliwa. Hivi nchi hii tumerogwa na nani?
Wakili ni mfanyabiashara hivyo lazima afanye kila njia mteja wake ashinde na inaweza ikawa njia ya kupata wateja wengi! usimlaum ndo mfumo ulivyo
 
Nasoma
aliekuwa
mkurugenzi wa tanesco amkana mkewe eva

binafsi namjua mke wa william mhando ni eva

na mbaya wakati anakana watoto amesahau wakuruugenzi wa kaampuni

ya eva ni watoto wake

nasubiri awakane na watoto tumwite tasa..

Hawa watu awajui kuishinawatu vizuri ni kulanao pamoja yeye anapiga alonealone

loh

raha yamilele umpe ee bwana na mwanga wa segerea uwaangazie wapumzike kwa amani
.

una ushahidi gani kwamba hawa watoto wenye ubini wa 'Mhando' ni watoto wa William Mhando (huyo anayeshitakiwa)? Kwani watu hawafanani majina? Kwa maana hiyo unataka kusema kwamba Rose Mhando (mwimba injili) ni mtoto wa William Mhando kisa tu anatumia ubini wa Mhando kama hao watoto mnaotaka kumbabikiza William Mhando?

Mkuu, kinachotakiwa mahakamani ni USHAHIDI, sio POROJO wala SIASA? Hata kama ukitoa mkanda wa harusi ya ndoa kama ushahidi, bila kuwepo cheti halali cha ndoa, imekula kwako! Chezea ushahidi wewe!
 
mbona issue nyepesi. Huyo Muhando aambiwe alete cheti cha ndoa yake. Mkewe aambiwe alete cheti cha ndoa yake(makazini huwa tunapeleka vyeti vya ndoa na vya kuzaliwa vya watoto kwa mafao flan flan). Kisha watoto waambiwe walete vyeti vyao vya kuzaliwa. Kisha wata cross check na ofisi ya vizazi na vifo na TANESCO HR data base. Kisha uchunguzi utaendelea toka hapo.

Mkuu, nakala za vyeti hivyo huwa hazibaki ofisi za vizazi & vifo. ni vigumu sana kupata taarifa hizo. Hapa Mhando hana kesi ya kujibu...ataachiwa very soon.
 
Mwanaume kuzaa na mwanamke hakuwafanyi wawe MME na MKE. A prime example ni mimi, nilizaa mtoto wa "majaribio" wakati ule wa ujana wangu, lakini huyo msichana/mwanamke sio mke wangu.

Hahaha mtoto wa majaribio
 
Ndio maana mkuu nikasema hapo juu,kutoa utata,mhando wa tanesco,eva mhando na watoto walete vyeti vyao vya ndoa na vya kuzaliwa kama walivyowahi peleka makazini/mashuleni long way back(kumbuka vyeti vya kuzaliwa vinaeleza majina ya mama,majina ya baba na majina ya mtoto. Vyeti vya ndoa vina majina halisi ya mke na mme). Na kumbuka,mhando alikua ni mwajiliwa wa siku nyingi tanesco hivyo kule mwanzoni asingekua na wazo la kupeleka vyeti feki kwani hata wazo la kuanzisha kampuni na mkewe halikuwapo.Na pia kule kazini asingepeleka vyeti feki vya kuzaliwa watoto wake kwani lengo huwa ni vimthibitishe yeye na mkewe ili apate mafao yake mbalimbali.Kinachobaki mna connect dots tu!.

una uhakika kwamba file la mhando ( ambamo kuna vyeti hivyo) halijapotezwa? unadhani amemkana mkewe kabla hajajipanga kupoteza ushahidi? kumbuka mchakato wa kumkana ulianza kitambo, sio kwamba amekurupuka tu kumkana bila kujipanga. chezea FISADI wewe!
 
USHAHIDI uko wapi?

Hakuna ushahidi kweli.
Maana kama Chenge ni mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge !

Raia Mwema - Bosi wa TANESCO amtetea mkewe

Majibu ya Mhando
Katika kufafanua kuhusu suala hilo, Mhando alisema wakati akiwa TANESCO katika ngazi za chini alikuwa akifanya kazi katika shirika hilo na mkewe, Eva.
"Mke wangu aliacha kazi, lakini tulikuwa na kampuni hiyo ya stationary Kariakoo na kwa sababu biashara haikuwa nzuri kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, tuliuza kampuni hiyo mwaka jana. Mke wangu aliajiriwa tu katika kampuni hiyo baada ya kununuliwa ili waweze kutumia uzoefu wake katika kuiendesha.

"Sasa kwa nafasi ya mke wangu, yeye ni mtendaji wa hiyo kampuni lakini shughuli zote za kutafuta zabuni zinafanywa na wakurugenzi wa kampuni hiyo, si mke wangu. Kwa hiyo, walipoomba kazi TANESCO hatua zote zilifanyika kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria na kampuni hiyo ilishindanishwa na kampuni nyingine na hatimaye kushinda," alisema Mhando.
 
hadi anamkana mkewe duh.......
Wewe unamuoa kama mjinga eeh? Mwenzako ndo amechomoka hivyo, wewe endelea kumshagaa tu. Kuna mtu aliwahi kujihasi ili asipatikane na hatia ya kubaka, sembuse kumkana mke kwa dili !!!
 
Mkuu, nakala za vyeti hivyo huwa hazibaki ofisi za vizazi & vifo. ni vigumu sana kupata taarifa hizo. Hapa Mhando hana kesi ya kujibu...ataachiwa very soon.
si kweli. Copy ya cheti changu cha ndoa nikiitaka naipata muda wowote. Taarifa zilizomo kwenye vyeti vya kuzaliwa watoto wangu,naweza zipata muda wowote hata vyeti vyao vikipotea. Huyo Eva Muhando alikuwepo tanesco from 1982 to 2009. Lazima taarifa nyingikuhusu family life yake zipo pale hr,so do mr mhando!
 
Janja tu hapo, wizi kama kawaida ya nchi hii, kesi yenyewe kiini macho kama za kina Mramba, utaisikia kesi miaka kumi mpaka watu wanasahau, huu ni ulaghai wa kisiasa kuonyesha serikali inawapeleka mahakamani wabadhilifu kumbe 'behind the scene' ni tofauti na picha lenyewe, shauri yako kama unazifuatilia hizi kesi za kuuzia jina.
 
Back
Top Bottom