Wewe kada mfurukutwa wa CCM usiyetumia kichwa chako vizuri kufikiri ushajiuliza huyo Zitto amefanya nini jimbo alilokuwepo mbunge kwa miaka 10 kiasi kwamba afae kuwa mbunge wa Ubungo?
Kwa namna ulivyoandika hapa inaonesha wewe si mkazi wa Dar es Salaam na hata huo ukazi wa Ubungo umejipachika tu...
Tatizo la maji ndani ya manispaa za Dar es Salaam ni la muda mrefu na wala halijaanza wakati wa Mnyika wala mbunge yoyote wa sasa wa jimbo lolote hapo Dar...
Hizi ndizo sababu za uhaba wa maji Dar;
Ukuaji wa mji, ujenzi holela, uchakavu wa miundombinu ya mtandao wa maji, ujenzi wa barabara kuu ya Morogoro, uongozi mbovu wa DAWASCO/DAWASA na mwisho uongozi usio na weledi wa serikali ya CCM kupitia wizara ya maji...
Je huyo Mnyika unataka ayabadili yote hayo kwa mamlaka ipi aliyonayo?
Je yeye ndiye anayeweka mgao wa maji?
Hivi majimbo ya CCM hapo Dar ni yote yenye neema ya maji?
Kodi unayokatwa kila mwaka ya gari hilo unaloendesha inakusanywa na Mnyika au 'serikali yako sikivu' ya CCM?
Kodi ya kukurekebishia barabara uwape wengine, madai upeleke kwa mwingine...
Mbunge kazi yake ni kuwasemea wananchi kwa serikali na kuhakikisha aliyoyasema yanatekelezwa...
Yatatekelezwa lini? Hilo lipo nje ya uwezo wake kwa kuwa majibu ya CCM huwa ni "kadiri fedha zitakapopatikana"...
Shule ina shida gani na unataka ushirikiano gani?
Mbona unaandika kwa kutetemeka hivyo...!!!
Madaraja yaliyojengwa chini ya uongozi wa huyu jamaa ni zaidi ya yale yaliyojengwa wakati wote ambao CCM ilikuwa inakalia jimbo la Ubungo...
Takwimu zipo na kwa kuwa wewe ni mvivu utataka utajiwe...
Zile ajira milioni moja za ilani ya uchaguzi wa CCM ziliishia wapi?
Kazi ya Mwenyekiti wako wa Mtaa ni ipi?
[QUOTE!]niishie HP kiukweli ninamengi sana mbunge wangu amefeli mtihani czani tutampa tena nfasi. mh Zito njoo utuokoe sisi wakazi wa ubungo