Mh. Zitto tunakuomba ugombee jimbo la Ubungo

Mh. Zitto tunakuomba ugombee jimbo la Ubungo

Mijitu mingine mpfyuuuuu.kama barabara ni mbovu kwann wananchi msiirekebishe wenyewe Pamoja na diwan wenu?kama shule inamatatizo,diwan mnae,shule inakamati ya wazazi kwanini msitatue wenyewe?kila kitu mbunge afanye,si sahihi.keenja amekaa ubungo miaka yote ameshindwa kutatua kero ya Maj sembuse mnyika Wa miaka nne na nusu?cha msingi ni kushirikiana na mbunge wenu Pamoja mtatue matatizo ya jimbo lenu.tatizo la maji ni la nchi nzima na si tu ubungo.

mnyika hatumtaki tena aende zake mtihani tuliompa ameshindwa ivo octoba tutampa cheti chake akapumzike
 
Hata zitto mwenyewe anajua hamuwezi mnyika,zitto akili yake kaiweka mfukoni

By SimbaKibogoyo :
Wana Ukumbi,
Ni sawa kumnyonga mnyonge ila sio sawa
kumnyima haki yake!
Zitto leo hii amekuwa mnyonge mbele ya
Watanzania.
Mengi mabaya yamezushwa kuhusu yeye, tena
mbaya zaidi na baadhi ya alio wapigania wamo
humo humo katika kumzushia mabaya!
Itakumbukwa Mnyika aligombea pamoja na Zitto
nafasi ya ubunge mwaka 2005, lakini tofauti ni
kwamba Mnyika alipigwa chini na wana Ubungo
huku Zitto yeye akienda mjengoni.
Lakini kama ilivyo ada, kwa Zitto ule haukuwa
ushindi, yalikuwa ni majonzi kwa kukosa wana
CHADEMA wenzake bungeni, hivyo alikula kiapo
cha kuhakikisha 2010 watakuwa wengi bungeni!
Katika kutekeleza dhamira yake hiyo, ukiachana
na hoja zake za nguvu bungeni zilizo
mtambulisha kwa Watanzania na kumfanya
kuaminiwa, alihakikisha anapigana bega kwa
bega na Mnyika na wagombea wengine wa
CHADEMA ili waingie bungeni.
Katika uchaguzi mkuu wa 2010, Zitto alitumia
wiki moja tu jimboni kwake Kigoma kaskazini
(lengo lilikuwa kutanguliza maslahi ya chama
CHADEMA kwa kusaidia majimbo mengine
pamoja na Dr Slaa kupata urais).
Hivyo alimpigia kampeni ya nguvu Mnyika
(Mnyika alikuwa hawezi kujieleza vizuri wakati
huo) na ndio wana Ubungo wengi wakaonyesha
imani yao kwa Mnyika na matokeo wote
tunayajua.
Je, mtu ambae ameacha jimbo lake katika kipindi
cha kampeni kisa kusaidia wengine waingie
bungeni, ana staili kuitwa 'msaliti'!?!
Je, hiyo ndiyo haki kwa mtu Mnyonge aina ya
Zitto? tuwe na tabia ya kulipa fadhira kwa walio
tutendea mema! ujeuri sio mzuri. God is watching
us!
....Mnyika, Kumbuka ulipotoka; heshimu
waliokufanya uwe hapo ulipo...
Pichani: Zitto akimnadi Mnyika jimboni Ubungo
kwenye kampeni, 2010.
 
Ni lini mlikaa wananchi wote Wa jimbo hili mkakubariana kuwa zitto ndio mtu sahihi kwenu?matatizo ya kigoma ameyashindwa,ndio aje ubungo......
 
Wewe hamnazo kabisa!! Hiz ndio thread ambazo kila siku tunalalamika zinajaza server tu!! Kwanza nimuhimu kujua changamoto ulizozitaja hapo zipo nchi nzima (hata huko kwa Nyepesi), sio Ubungo pekee....
Ninachokijua akili za watanzania (kama wewe) zimefumbwa, hawajui majukumu ya Mbunge katika jimbo. Kwa taarifa yako anayeweza kufanya yote hayo ni serikali na sio Mnyika. Bila kupepesa macho Mnyika amefanya/ametimiza wajibu wake kama Mbunge kwa kuisimamia serikali na kuishauri. Kwa mfano mara kadhaa amepeleka hoja binafsi Bungeni akihoji juu ya upatikanaji wa maji katika Jimbo lake na DSM kwa ujumla, hapa unaona jitihada yake. Mnyika hakusanyi kodi wala hana vyanzo rasmi vya mapato, hivyo kutaka kuwaaminisha watu kwamba yeye ndiye majukumu ya kujenga barabara ni "UPUMBAVU" isiovumilika. Serikali ya CCM wanayo majibu juu ya matatizo haya ambayo kiuhalisia yapo nchi Nzima.
 
mimi na tamilia yangu yote tutampa kura mh. mnyika. tupo kimara baruti.

Hahahahaaaa.....sawa...wewe na tamilia mimi na wananchi wazalendo tutampa kura zetu mpiganaji zzk.Hatupendi ukabila sisi pasipo matokeo ya utekelezaji ahadi alizotoa wakati akiomba kura yangu.
 
Hahahahaaaa.....sawa...wewe na tamilia mimi na wananchi wazalendo tutampa kura zetu mpiganaji zzk.Hatupendi ukabila sisi pasipo matokeo ya utekelezaji ahadi alizotoa wakati akiomba kura yangu.

zzk mbunge mtarajiwa jimbo la Ubungo
 
mm nikiwa .mwananchi na mkazi wa Ubungo makoka nakuomba mh zito uje ugombee jimbo la Ubungo kutokans na kero hizi
1. mbunge wangu ameshindwa kwa kipindi cha miaka mitano ameshindwa kutatua matatizo ya maji. tunakaa mwez mzm hatuna maji ni mate so
2. barabara zetu mbovu hasa hii ya makoka Ubungo imefikia asubuhi nawskataa RAIA kenye gari yangu kwani barabara ni makorongo tupu na mbunge hatumuoni
3. shule yetu ya kata hapa inashida nyingi mbunge kapotea wala kutembelea kutoa ushirikiano
4. kuna shida ya daraja eneo la unyamwezini baafhi ya watu wamekufa mvua zinaponyesha kwa kupita juu ya Bomba la dawasko na mbunge hatujapta muona hats ck moja ni majanga
5. vijana wengi wa Ubungo ajira hawana wanapanga vitu jioni kwenye transfoma za umeme Ubungo mbumge ameshindwa kutoa njia mbadala ili vijana wasikae maeneo hatarishi

6. wananchi wa manzese wamesahau km wanambunge hajswahi tembelea ht ck moja. mitaro imeziba nyumba zimejaa maji kipindi hiki cha mvua mbunge wetu hana ht habari

niishie HP kiukweli ninamengi sana mbunge wangu amefeli mtihani czani tutampa tena nfasi. mh Zito njoo utuokoe sisi wakazi wa ubungo

Kwanini usigombee wewe uyamalize matatizo hayo? Usijiaibishe hivyo. Huoni kama unatuambia akili zako ni za kushikiwa?
 
kumbe ubunge Sikh hizi ni sawa na urais?haya zitto with huo ukamalize matatizo ya ubungo kama ulivyofutilia mbali ya kigoma kaskazini na kuifanya kama Dubai.
 
Ubungo? Zitto si mjinga kiasi hicho, bado anapenda kurudi mjengoni. Atarukaruka wee mwishowe atagombea kulekule kwao Kigoma kask.

Kumbuka kuwa hizi mbwembwe za kuwa kama anataka kugombea majimbo mengine alizifanya kabla, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010. Hatimaye akarudi kwao.
 
zito alishawaaga wanakigoma acha kupotosha ss ni zam yetu
 
mm nikiwa .mwananchi na mkazi wa Ubungo makoka nakuomba mh zito uje ugombee jimbo la Ubungo kutokans na kero hizi
1. mbunge wangu ameshindwa kwa kipindi cha miaka mitano ameshindwa kutatua matatizo ya maji. tunakaa mwez mzm hatuna maji ni mate so
2. barabara zetu mbovu hasa hii ya makoka Ubungo imefikia asubuhi nawskataa RAIA kenye gari yangu kwani barabara ni makorongo tupu na mbunge hatumuoni
3. shule yetu ya kata hapa inashida nyingi mbunge kapotea wala kutembelea kutoa ushirikiano
4. kuna shida ya daraja eneo la unyamwezini baafhi ya watu wamekufa mvua zinaponyesha kwa kupita juu ya Bomba la dawasko na mbunge hatujapta muona hats ck moja ni majanga
5. vijana wengi wa Ubungo ajira hawana wanapanga vitu jioni kwenye transfoma za umeme Ubungo mbumge ameshindwa kutoa njia mbadala ili vijana wasikae maeneo hatarishi

6. wananchi wa manzese wamesahau km wanambunge hajswahi tembelea ht ck moja. mitaro imeziba nyumba zimejaa maji kipindi hiki cha mvua mbunge wetu hana ht habari

niishie HP kiukweli ninamengi sana mbunge wangu amefeli mtihani czani tutampa tena nfasi. mh Zito njoo utuokoe sisi wakazi wa ubungo

Hizo changamoto zimetatuliwa na Ayattollah huko jimboni kwake kigoma kaskaz.
 
Back
Top Bottom