Wewe kada mfurukutwa wa CCM usiyetumia kichwa chako vizuri kufikiri ushajiuliza huyo Zitto amefanya nini jimbo alilokuwepo mbunge kwa miaka 10 kiasi kwamba afae kuwa mbunge wa Ubungo?
1. mbunge wangu ameshindwa kwa kipindi cha miaka mitano ameshindwa kutatua matatizo ya maji. tunakaa mwez mzm hatuna maji ni mateso
Kwa namna ulivyoandika hapa inaonesha wewe si mkazi wa Dar es Salaam na hata huo ukazi wa Ubungo umejipachika tu...
Tatizo la maji ndani ya manispaa za Dar es Salaam ni la muda mrefu na wala halijaanza wakati wa Mnyika wala mbunge yoyote wa sasa wa jimbo lolote hapo Dar...
Hizi ndizo sababu za uhaba wa maji Dar;
Ukuaji wa mji, ujenzi holela, uchakavu wa miundombinu ya mtandao wa maji, ujenzi wa barabara kuu ya Morogoro, uongozi mbovu wa DAWASCO/DAWASA na mwisho uongozi usio na weledi wa serikali ya CCM kupitia wizara ya maji...
Je huyo Mnyika unataka ayabadili yote hayo kwa mamlaka ipi aliyonayo?
Je yeye ndiye anayeweka mgao wa maji?
Hivi majimbo ya CCM hapo Dar ni yote yenye neema ya maji?
2. barabara zetu mbovu hasa hii ya makoka Ubungo imefikia asubuhi nawskataa RAIA kenye gari yangu kwani barabara ni makorongo tupu na mbunge hatumuoni
Kodi unayokatwa kila mwaka ya gari hilo unaloendesha inakusanywa na Mnyika au 'serikali yako sikivu' ya CCM?
Kodi ya kukurekebishia barabara uwape wengine, madai upeleke kwa mwingine...
Mbunge kazi yake ni kuwasemea wananchi kwa serikali na kuhakikisha aliyoyasema yanatekelezwa...
Yatatekelezwa lini? Hilo lipo nje ya uwezo wake kwa kuwa majibu ya CCM huwa ni "kadiri fedha zitakapopatikana"...
3. shule yetu ya kata hapa inashida nyingi mbunge kapotea wala kutembelea kutoa ushirikiano
Shule ina shida gani na unataka ushirikiano gani?
4. kuna shida ya daraja eneo la unyamwezini baafhi ya watu wamekufa mvua zinaponyesha kwa kupita juu ya Bomba la dawasko na mbunge hatujapta muona hats ck moja ni majanga
Mbona unaandika kwa kutetemeka hivyo...!!!
Madaraja yaliyojengwa chini ya uongozi wa huyu jamaa ni zaidi ya yale yaliyojengwa wakati wote ambao CCM ilikuwa inakalia jimbo la Ubungo...
Takwimu zipo na kwa kuwa wewe ni mvivu utataka utajiwe...
5. vijana wengi wa Ubungo ajira hawana wanapanga vitu jioni kwenye transfoma za umeme Ubungo mbumge ameshindwa kutoa njia mbadala ili vijana wasikae maeneo hatarishi
Zile ajira milioni moja za ilani ya uchaguzi wa CCM ziliishia wapi?
6. wananchi wa manzese wamesahau km wanambunge hajswahi tembelea ht ck moja. mitaro imeziba nyumba zimejaa maji kipindi hiki cha mvua mbunge wetu hana ht habari
Kazi ya Mwenyekiti wako wa Mtaa ni ipi?
[QUOTE!]niishie HP kiukweli ninamengi sana mbunge wangu amefeli mtihani czani tutampa tena nfasi. mh Zito njoo utuokoe sisi wakazi wa ubungo[/QUOTE]
Bora uishie hapo maana hoja huna...