Katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu aliulizwa ni lini Mh Sitta ataondoka kwenye nyumba ya Spika huko Masaki maana sio Spika tena. Kwa maelezo ya mbunge aliyeuliza swali ni kwamba serikali inatumia Tsh million 12 kila mwezi kwa nyumba ya huyu Spika. Lakini kama kawaida Mama Makinda alikurupuka na kujibu swali la serikali akisema kuwa hiyo ni stahiki ya Mh Sitta kama Spika mstaafu.
Wana-JF, Sasa nitawahoji, ni sahihi kwa Mh Sitta kuendelea kuishi kwenye nyumba ya Spika hata kama sio Spika? Na kwa mantiki hiyo Marais wastaafu wanatakiwa waendelee kuishi IKULU maana wanastahili? Sera ya kuangalia maslahi ya viongozi wakuu wastaafu inasemaje?
Msekwa alikuwa anakaa nyumba ya serikali baada ya kuinunua imekuwa ya kwake. Issue ya Sitta ni tofauti, bado ni mtumishi wa umma na wizara yake inawajibika kwa makazi yake. Kwanini kachagua kuitafuna Bunge? kwa sababu anafaidika na hiyo nyumba aliyojipangishia, wanagawana pasu pasu na mwenye nyumba kutokana na pango la kifisadi!Kwani P. Msekwa anakaa kwenye nyumba gani?
Hakuna nyumba ya Spika!
Nadhani kuna haja ya kabisa (it is in the public interest) kujuwa nani anagharamia matengenezo ya nyumba ya Mama Makinda Kijitonyama. Kama ni serikali je kwa sababu zipi, na kepengele gani katika sheria zetu kinaruhusu kufanya hivyo?
| ||
|
| ||
|