Mh. Sitta kuendelea kukaa kwenye nyumba ya Spika Masaki ni halali?

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,198
Katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu aliulizwa ni lini Mh Sitta ataondoka kwenye nyumba ya Spika huko Masaki maana sio Spika tena. Kwa maelezo ya mbunge aliyeuliza swali ni kwamba serikali inatumia Tsh million 12 kila mwezi kwa nyumba ya huyu Spika. Lakini kama kawaida Mama Makinda alikurupuka na kujibu swali la serikali akisema kuwa hiyo ni stahiki ya Mh Sitta kama Spika mstaafu.

Wana-JF, Sasa nitawahoji, ni sahihi kwa Mh Sitta kuendelea kuishi kwenye nyumba ya Spika hata kama sio Spika? Na kwa mantiki hiyo Marais wastaafu wanatakiwa waendelee kuishi IKULU maana wanastahili? Sera ya kuangalia maslahi ya viongozi wakuu wastaafu inasemaje?
 
Yaani we acha tu!!!!!!!!! halafu eti kodi ya mshahara wa Slaa inakuwa ndiyo ishu kuhusu ufujaji wa mali ya umma! It's just crazy!!!! Hilo linchi lina laana.
 
Hakuna nyumba ya Spika!

sheria ya mafao na benefits za viongozi wastaafu wa siasa hazitaji kuwa spika msataafu anapewa nyumba na serikali, zinataja atapewa gari moja ambalo atalihudumia mwenyewe na atapewa dereva, lita 70 za mafuta kwa wiki,maintanance allowance for motor vehicle at a rate equal to forty % of the allowance, nyumba haitajwi hapa
 
Nchi hii haina utaratibu wa maana,Ndio maana Nahodha kakaa hoteli miezi kibao,je nyumba aliyokuwa anakaa aliyetangulia alipewa nani au iliuzwa kinyemela.Nchi hii bana.
 
Unajua hawa viongozi wetu wanadhani akili zetu hazina uwezo wa kudadavua mambo.

Kwanza niseme tu kunautofauti juu ya kiongozi aliyestaatu wadhifa wake bila kupata wadhifa mwingine na yule aliyestaafu wadhifa wake halafu akapata wadhifa mwingine. Sasa kwa kuwa hoja si hiyo ya kwanza basi nitajikita kwenye kiongozi aliyestaafu wazifa wake akapata stahili zake zote na kisha akapewa/ akapata wadhifa mwingine. Na hawa wapo wengi mmoja wapo ni Sitta (Speaker Mstaafu), Nahodha ( waziri kiongozi mstaafu) n.k.

Hawa viongozi wa aina hii wanahaki ya kupata stahili zao kama wastaafu kwa nyadhifa zao, lakini si kupata treatment za awali kwenye nyadhifa zao MPYA ( ikiwepo hadhi ya nyumba ya awali) kwa hiyo si haki kwa waziri sita kuendelea kutumia nyumba ya SPEAKER ya masaki, wakati yeye ni waziri tu kama mawaziri wengine.

Mbona Mkapa (rais mstaafu) ni mkuu wa Chuo cha UDOM na hakai IKULU wala hapati treatment zote alizokuwa akipata awali. Huu nao ni mzigo kwa wlipa kodi wa nchi. Nikionacho mimi ni kwamba viongozi wetu wengi wanapenda MONEY, POWER & RESPECT na si kutumikia wananchi, na ndiyo maana wanang'ang'ania vitu kama hivyo. Juzi juzi hapa hata nahodha alikataa kuhamia kwenye nyumba yake eti kwa kuwa haina hadhi ya Waziri Kiongozi Mstaafu
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hakuna nyumba ya Spika!

@ Zitto, Wether imejengwa au imekodishwa na serikali kama makazi ya Spika basi defination sahihi inakuwa 'nyumba ya Spika' maana inatumiwa na serikali kwa ajili ya Spika. tujadili.
 
Kwani yeye hakupata ule mgao wa nyumba za umma za Oysterbay? Au anapangisha!! Tusubiri KATIBA MPYA (kama mchakato hautachakachuliwa) ndio itaondoa loopholes hizi za kishenzi. God bless bongoland
 
Katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu aliulizwa ni lini Mh Sitta ataondoka kwenye nyumba ya Spika huko Masaki maana sio Spika tena. Kwa maelezo ya mbunge aliyeuliza swali ni kwamba serikali inatumia Tsh million 12 kila mwezi kwa nyumba ya huyu Spika. Lakini kama kawaida Mama Makinda alikurupuka na kujibu swali la serikali akisema kuwa hiyo ni stahiki ya Mh Sitta kama Spika mstaafu.

Wana-JF, Sasa nitawahoji, ni sahihi kwa Mh Sitta kuendelea kuishi kwenye nyumba ya Spika hata kama sio Spika? Na kwa mantiki hiyo Marais wastaafu wanatakiwa waendelee kuishi IKULU maana wanastahili? Sera ya kuangalia maslahi ya viongozi wakuu wastaafu inasemaje?

ana nyumba nyingine kinondoni sasa anajigawaje kuishi kote kote?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tukienda mbali zaidi inawezekana nyumba inayojengwa Kijitonyama inayojengwa ka kodi zetu na itakuwa mali binafsi ya spika wa sasa kwa tafsiri ya spika mstaafu. Mtu anapata TShs. 7 million plus, anapewa na nyumba ya bure; anayepata TShs. 135,000 huyo hana haki yoyote ndani ya nchi yake
 
Nadhani kuna haja ya kabisa (it is in the public interest) kujuwa nani anagharamia matengenezo ya nyumba ya Mama Makinda Kijitonyama. Kama ni serikali je kwa sababu zipi, na kepengele gani katika sheria zetu kinaruhusu kufanya hivyo?
 
Ni ubadhirifu mwingine wa mali za walipakodi, Anabembelezwa na CCM ili wamtumie katika kuchakachua KATIBA MPYA.
 
Yaani we acha tu!!!!!!!!! halafu eti kodi ya mshahara wa Slaa inakuwa ndiyo ishu kuhusu ufujaji wa mali ya umma! It's just crazy!!!! Hilo linchi lina laanaa.

Nchi yetu Tukufu Tanzania IMEBARIKIWA,
Navunja laana hiyo unayoisema katika Jina la Yesu Kristo. Amen.
 
Kwa kweli hii nchi niaelekea kubaya sana, viongozi wamezidi kuondoka na mali za uma, wanapewa stahili nyingi sana but still hawatosheki, hivi hawajui hizo stahili kwa mwananchi wakawaida ni hela nyingi, TUBADILIKE jamani!
 
Katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu aliulizwa ni lini Mh Sitta ataondoka kwenye nyumba ya Spika huko Masaki maana sio Spika tena. Kwa maelezo ya mbunge aliyeuliza swali ni kwamba serikali inatumia Tsh million 12 kila mwezi kwa nyumba ya huyu Spika. Lakini kama kawaida Mama Makinda alikurupuka na kujibu swali la serikali akisema kuwa hiyo ni stahiki ya Mh Sitta kama Spika mstaafu.Wana-JF, Sasa nitawahoji, ni sahihi kwa Mh Sitta kuendelea kuishi kwenye nyumba ya Spika hata kama sio Spika? Na kwa mantiki hiyo Marais wastaafu wanatakiwa waendelee kuishi IKULU maana wanastahili? Sera ya kuangalia maslahi ya viongozi wakuu wastaafu inasemaje?
Good point, kodi ya nyumba na malipo ya kustaafu?
 
Nchi yetu Tukufu Tanzania IMEBARIKIWA,
Navunja laana hiyo unayoisema katika Jina la Yesu Kristo. Amen.

Hicho Kidumu nacho ni laana maana anayedumu peke yake ni Mungu. Vunja na hiyo! Mlisema mtatawala daima na milele; Hiyo nayo laana! vunja. HAta hivyo utavunja na mwenge maana nao ni ngao ya watawala wako wa kidumu: vunja nako huko. CCM laana tupu: Utavunja na pia wizi wa EPA? maana Mungu haruhusu uibe halafu useme akusamehe huku ukijua hujarudisha! utavunja vingapi!??
 
Back
Top Bottom