Milioni 50 kila kijiji imekuwa kaa la moto kwa waziri wa fedha kwani sasa wabunge wa ccm imekuwa ndiyo hoja yao ya kumsulubu Mhe. Dr. Mpango.
Aisee, umenikumbusha hii kitu.....
Na kwa namna yoyote, 2015 wakati wa kampeni za uchaguzi, hakuna ahadi iliyo ring ktk masikio ya watu wa vijijini na mijini kama hii ya kila kijiji ama mtaa kuwa unapata Tshs. 50,000,000/= kila mwaka wa fedha kwa maendeleo !!
Wenye kuwaza maili nyingi mbele, tulijiuliza : How could that be possible ??
Asipoitekeleza hii (in reality, ameshashindwa kwa sbb tayari yuko mwaka wa tatu sasa na hakuna hata kijiji ama mtaa mmoja ambao ulishapokea hata senti tano) , ajiandae hiihii kuwa kichinjio chake yeye mwenyewe na wana CCM wenzake mwaka 2019 wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na wanamalizwa kabisa mwaka 2020 ktk uchaguzi mkuu!!
Wasidhani kuwa hizi mbinu zao za kijinga na kipuuzi za kuwabana watu ikiwemo kuwapa adhabu zisizo hata na kichwa wala miguu wabunge wetu akina John Mnyika, Easther Balaya na Halima Mdee, ama kupiga marufuku shughuli za kisiasa ama kuzima bunge lisirushwe "live" ktk vyombo vya habari itakuwa ni nafuu ya CCM...... never, ever....ni kujidanganya kwa herufi kubwa!!
Kwangu mimi nadhani, nafuu yao ipo ktk kutekeleza kila walichokiahidi wakati kampeni za uchaguzi 2015 hata wakalazimisha ushindi wa huyu ambaye ana dalili zote za kushindwa kuongoza nchi hata wakapora mchana kweupe ushindi wa Edward N. Lowassa (Tanganyika) na ule wa Maalim Seif Shariff Hamad (Zanzibar).....
Nafuu ya Magufuli na CCM yake haiko ktk uongozi wa kilaghai, uongo, vitisho na hadaa kwa sbb binadamu wa dunia ya leo, si wale wa zamani zile za zidumu fikra za mwenyekiti...... wa zama hizi ni wale wa kuhoji na kudadisi kila unaloamua na kufanya au kutokulifanya... na ni lazima utoe majibu sahihi na ndipo mtakapoenda nao sambamba, Vinginevyo utalia na kusaga meno.....
Kama Magufuli haelewi hili, It's simple.... amuulize mwenzake Donald Trump wa USA, aliiingia madarakani kwa mbwembwe nyingi akidhani kuongoza nchi ni kama kuongoza familia yake ama vikampuni vyake binafsi vya biashara, lakini sasa ndani ya miezi isiyozidi minne tu anatamani aachie ngazi yeye mwenyewe au apigwe chini kwa lazima (impeached) !!