Mh Rais yanayomshinda hayaongelei tena

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,841
2,000
Salam!
Nimekuwa nikiwaza mengi juu ya Rais wa URT kuwa amekuwa mjanja saana. Kuna Mambo aliyoyatamka hadharani na kuyaanzisha lakini akichemka huwa hayarudii tena!

Swala la Kwanza, Mahakama ya Mafisadi. Mpaka sasa binafsi hata sielewi iko wapi na inafanya nini pia imefunga wangapi ama kuwakamata. Hii ni dhahiri ilikuwa kuwafurahisha walewale Watanzania wanaoishi hata hawaelewi nini kinaendelea badala yake wanafanya kazi ya Kushangilia tu.

Pili, alisema Wapinzani hawatanusa pua katika Serikali atayounda: Hapa kubwa tunataka atushuhudie kuwa je, Kitila, Mghwira na Mrema hawakuwa Wanasiasa wa Upinzani?

Tatu: Aliahidi Kubana Matumizi na Kukusanya Mapato mengi. Hapa bila shaka kila mtu anaona Matumizi ndiyo yamekuwa makubwa zaidi. Mfano, nchi ina Wakurugenzi wa Halmashauri waliokuwa wanahudumu karibia 80% wameondolewa na wamewekwa wengine, na hawa walioondolewa kwenye Ukurugenzi bado wapo kwa RAS wanapiga tu LSSE zao kwa Kwenda mbili. Kwa maana hiyo kuna DEDs wawili katika Maslahi kwa Nchi hii. Pia, Watendaji wengi waondolewa kwenye Nafasi zao Ila bado wanaendelea kupata Maslahi yao. Kulikuwa na haja gani ya Kuwaondoa kama hawakuwa na Matatizo?

Nne: Aliahidi kutofukua Makaburi. Binafsi naona hata haina haja kuelezea maana kila jambo liko wazi, jamaa anakomaa naona anapambana na vitu vya Kale. Mathalani, swala la madini anapiga hesabu tangu kuanzishwa kwa Mikataba, pia anadeal na mambo ya Kale hususani Watumishi wa umma!

Na mengine mengi tu, nimeandika Machache tu.
Yeye anasema siyo mwanasiasa sasa mbona mengi yanamshinda tu aliyoyaahidi? Na Kwanini Siku hizi ameacha kusema mniombee, kaona nini tena?

Ahsanteni!
 

MASHANJARA

Senior Member
Apr 2, 2012
172
225
Kwangu mimi, suala la misafara mirefu ya viongozi naona ni aina nyingine ya matumizi mabaya ya pesa za umma. Kina ma rc huku wanatembea na vingora, polisi kibao na magari.

Nguvu kubwa ya kudhibiti upinzania halali inayoendana na matumizi makubwa ya rasilimali halali au pengine hali ya usalama wa viongozi ni tete ?
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,864
2,000
Huyu mambo yote yaliyomshinda huwa hayarudii tena..

Suala nyeti kama la bei ya sukari limemshinda rasmi.

Nipo Babati Sukari kilo 3500/ na inaonekana ni bei ya kawaida kabisa..

Sijamsikia Rais akizungumzia kabisa mfumuko wa bei za vyakula. Unga upo juu, maharage yapo juu, nk nk.

Yeye ni ujenzi wa ma flyover na reli ambazo hata hela hana.
 

South

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
3,483
2,000
Pumzi ishakata kwa saizi maana hakuna la maana alilofanya, mtaani hali mbaya gharama za kimaisha zipo juu na pesa hakuna
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom