Mh Rais yanayomshinda hayaongelei tena

Mh Rais yanayomshinda hayaongelei tena

Unaongea pumba, kudai hela zilizoibwa ni kufukua makaburi? Any criminal act haizeeki baba. Wala hakuna Rais anayekuwa juu ya sheria iwe JK or any!
 
Salam!
Nimekuwa nikiwaza mengi juu ya Rais wa URT kuwa amekuwa mjanja saana. Kuna Mambo aliyoyatamka hadharani na kuyaanzisha lakini akichemka huwa hayarudii tena!

Swala la Kwanza, Mahakama ya Mafisadi. Mpaka sasa binafsi hata sielewi iko wapi na inafanya nini pia imefunga wangapi ama kuwakamata. Hii ni dhahiri ilikuwa kuwafurahisha walewale Watanzania wanaoishi hata hawaelewi nini kinaendelea badala yake wanafanya kazi ya Kushangilia tu.

Pili, alisema Wapinzani hawatanusa pua katika Serikali atayounda: Hapa kubwa tunataka atushuhudie kuwa je, Kitila, Mghwira na Mrema hawakuwa Wanasiasa wa Upinzani?

Tatu: Aliahidi Kubana Matumizi na Kukusanya Mapato mengi. Hapa bila shaka kila mtu anaona Matumizi ndiyo yamekuwa makubwa zaidi. Mfano, nchi ina Wakurugenzi wa Halmashauri waliokuwa wanahudumu karibia 80% wameondolewa na wamewekwa wengine, na hawa walioondolewa kwenye Ukurugenzi bado wapo kwa RAS wanapiga tu LSSE zao kwa Kwenda mbili. Kwa maana hiyo kuna DEDs wawili katika Maslahi kwa Nchi hii. Pia, Watendaji wengi waondolewa kwenye Nafasi zao Ila bado wanaendelea kupata Maslahi yao. Kulikuwa na haja gani ya Kuwaondoa kama hawakuwa na Matatizo?

Nne: Aliahidi kutofukua Makaburi. Binafsi naona hata haina haja kuelezea maana kila jambo liko wazi, jamaa anakomaa naona anapambana na vitu vya Kale. Mathalani, swala la madini anapiga hesabu tangu kuanzishwa kwa Mikataba, pia anadeal na mambo ya Kale hususani Watumishi wa umma!

Na mengine mengi tu, nimeandika Machache tu.
Yeye anasema siyo mwanasiasa sasa mbona mengi yanamshinda tu aliyoyaahidi? Na Kwanini Siku hizi ameacha kusema mniombee, kaona nini tena?

Ahsanteni!

Ni wewe tu ndio umeshindwa kuelewa, mpaka sasa rais bado hajachagua wapinzani. Mrema (TLP), kitila na Mghwira (ACT) sio wapinzani, kwa maana ya kwamba hawamchallenge wala kumpinga kwa lolote, na hao ndio aina ya "wapinzani" utakao waona kwenye serikali yake.
 
Tunashukuru kwa kuwa tayari upo msemo (sina hakika kama ni Wahenga walisema ama ni Vitabu vya Dini vimeandikwa)

Wanasema AHADI NI DENI...

Nafsi yake inamsuta/itamsuta...

Vipi na lile AGIZO la MDOGO WAKE (P.Makonda) swala la walimu wa jijini Dar kupanda DALADALA bure....

Ama nae alikuwa anataka kutafuta KIKI.
Hakuna alilolianzisha akafanikisha mwishowe, ni Serikali ya Matamko hii!
 
Unaongea pumba, kudai hela zilizoibwa ni kufukua makaburi? Any criminal act haizeeki baba. Wala hakuna Rais anayekuwa juu ya sheria iwe JK or any!

Tuanze na wezi tuwashike ndipo tupige gharama za wizi wao!!
 
Hataki nchi iwe ombaomba ilihari ina resources kibao, matokeo yake anaombaomba mpk nchi za Afrika wenzetu.
 
Alikuwa anafikiri urais ni kuandaa mikakati ya kuwabana wapinzani (bunge) na kutafuta sifa kumbe alitakiwa atenge muda mwingi wa kujenga uchumi na kurahisisha maisha ya wananchi, nasikia analia sana kwanini aligomea kwa sababu atakuwa ni rais wa kwanza kufeli katika kila jambo - Mzee wa Chalinze omba sub uokoe jahazi
 
Janani nchi iko salama jana tumepokea malori mawili ya takataka (rubbish) au nyie hamkuyaona???
Sasa lini Nchi Ilikuwa Vitani ukiachia mbali ile ya Kagera ya 40 years ago?
 
Back
Top Bottom