Mh. Rais mrudishe Said Meck Sadick Dar es salaam

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,250
Naweza nisieleweke kwa sasa lakini kadri muda unavyokwenda mtanielewa.

Tanzania ni Dar na Dar ni Tanzania.

Jiji hili ni kila kitu, lina mchanganyiko wa fani zote unazozijua, kuanzia wasomi, wezi, bandari, mabenki, balozi, majeshi, ombaomba, majambazi, matapeli, wafanyakazi, wasio na kazi n.k, naweza kusema ni kama "reception" ya nchi.

Kuteteleka kwa uongozi wa mkoa huu ni kama kielelezo cha kuteteleka kwa uongozi wa nchi. Kwa maana hiyo mkoa huu unahitaji kiongozi mahili mwenye busara mission na vision ya kuuongoza.

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo jiji hili kama mkoa lilibahatika kuongozwa na Mh. Makamba, Mh. Kandoro, Mh Meck Sadick bila kumsahau Keenja aliyeliongoza Tume ya Jiji kwa mafanikio makubwa, pamoja na wakati huo jiji kuwa na vitendeakazi duni lakini lilionekana kuwa safi.

Nakumbuka vilevile operesheni mbalimbali za Makamba na Kandoro na Meck Sadick kuhusu machinga na ombaomba, walikuwa wakifukuzana na machinga mitaani lakini walikuwa na "alternative" kama vile kuanzishwa kwa Machinga Complex na mabasi kuhamia UBT.

Tofauti na mkuu wa mkoa wa sasa Mh. Paul Makonda, yeye tangu aanze kutoa matamko "operations" sijaona hata moja likifanikiwa, sina haja ya kuorodhesha hapa matamko yake.

Labda niseme ni kutokana na uzoefu wake kuwa mdogo au umri au ukosefu wa uwezo wa kubuni mbinu mpya za kutatua kero za jiji na mkoa huu ambazo ni nyingi au labda hajui JDs na uwezo wa cheo alichonacho.

Ni kutokana na hayo ndiyo maana nashauri aidha Mh. Rais amrudishe mkuu wa mkoa aliyepita Said Meck Sadick au Makonda atafutiwe msaidizi/mshauri mzoefu au jiji likabidhiwe kwa tume nyingine ya Jiji kama iliyokuwa ile ya Charles Keenja.

Bila kufanya hayo mapema na kwa wakati, kuna hatari ya Jiji kupoteza hadhi yake.

Naomba kuwasilisha.
 
Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,536
2,000
Unajua UFISADI WA MECK SADICK alikuwa anaufanya MRADI WA KIGAMBONI akiwa na mama jizi Tibaijuka..? KDA unaijua..? wakati Meck akiwa RC Dar unajua madudu yake ww..? Unajua AVIC town kigamboni ni ya nani au wana share na nani..? Mgogoro wa ardhi Kigamboni hadi Mh. Waziri Lukuvi sasa kaumaliza unajua nani alikuwa nyuma yake, Tibaijuka, na Meck ndio vinara...!! Acha ujinga

Tutoleee ukifafa hapa.. plse
 
Midumare Ngatuni Iwato

JF-Expert Member
Jul 13, 2016
1,656
2,000
Makonda nakukubali wee nikijana fanya makosa mengi ndio yatakayokufanya uwe kiongozi Mzuri.nionyesheni hapa Tanzania ukimtoa Makonda kiongozi gani hajawai kukosea,mkitaka nitasema,tatizo ni cheo cha Makonda na sio makonda tatizo,Mh Raisi.usiwasikilize hao watoto wakufikiri
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
12,214
2,000

Unajua UFISADI WA MECK SADICK alikuwa anaufanya MRADI WA KIGAMBONI akiwa na mama jizi Tibaijuka..? KDA unaijua..? wakati Meck akiwa RC Dar unajua madudu yake ww..? Unajua AVIC town kigamboni ni ya nani au wana share na nani..? Mgogoro wa ardhi Kigamboni hadi Mh. Waziri Lukuvi sasa kaumaliza unajua nani alikuwa nyuma yake, Tibaijuka, na Meck ndio vinara...!! Acha ujinga

Tutoleee ukifafa hapa.. plse
***
SASA AMEHAMISHIWA MOSHI ILI IWAJE?/ OVER!!!
 
EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,250

Unajua UFISADI WA MECK SADICK alikuwa anaufanya MRADI WA KIGAMBONI akiwa na mama jizi Tibaijuka..? KDA unaijua..? wakati Meck akiwa RC Dar unajua madudu yake ww..? Unajua AVIC town kigamboni ni ya nani au wana share na nani..? Mgogoro wa ardhi Kigamboni hadi Mh. Waziri Lukuvi sasa kaumaliza unajua nani alikuwa nyuma yake, Tibaijuka, na Meck ndio vinara...!! Acha ujinga

Tutoleee ukifafa hapa.. plse
Kwa hiyo rais kakosea kumteua fisadi Sadick kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro?
 
simanyane

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
2,246
1,500
Mtoa mada, ww wa UDOM nn..? If not, you hv linkage with them..!!

Unajua UFISADI WA MECK SADICK alikuwa anaufanya MRADI WA KIGAMBONI akiwa na mama jizi Tibaijuka..? KDA unaijua..? wakati Meck akiwa RC Dar unajua madudu yake ww..? Unajua AVIC town kigamboni ni ya nani au wana share na nani..? Mgogoro wa ardhi Kigamboni hadi Mh. Waziri Lukuvi sasa kaumaliza unajua nani alikuwa nyuma yake, Tibaijuka, na Meck ndio vinara...!! Acha ujinga

Tutoleee ukifafa hapa.. plse
Hii tabia ya kuwaita watu mafisadi baada ya kuondoka kwenye uongozi sijui mtaiacha lini.Inakuwaje watu mnao kwenye chama mnashindwa kuwawajibisha hao mafisadi ni siku nyingi watu tunamjua mzee Sadick kwamba ni mtu mwadilifu kumbe nyie mmeshajua alicho fisidi huku mkiogopa hata kumgusa
 
Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,556
2,000
Gezaulole ni lugha ya picha Great thinker jaribu kufikiri....

Kwenda Geza Ulole inareflect maamuzi yaliyowahi kufanywa miaka ilee ya Nyerere ya kukamata wazururaji na kuwapeleka Geza Ulole na maeneo mengine na hadi leo pamekosekana pa kulima.

Unapojiita GT inatakiwa u-stretch your imagination ....
Na wewe unapojiita GT pia uwe unajaribu kufikiri, yaani wapite nyumba kwa nyumba watafute wasio na kazi, kisha ndio waende huko "Gezaulole" kufanya nini?, kukaa bila kazi?

Nilitegemea kutoka kwako nione ushauri wa kutatua tatizo hilo la kukosa ajira na wala sio kuwa proud kwamba wewe una kazi na wenzio waende Geza, kuna watu wana degree ya kwanza mpaka mAsters na wanaangaika miaka kwa miaka bila kupata kazi

Think think think
 
Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,536
2,000
Kwa hiyo rais kakosea kumteua fisadi Sadick kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro?

Usiniwekee maneno mdomoni, ukanichonganisha na Rais wangu Magufuli naye muamini na kumpenda mno..!!

Ila ingekuwa mm ndio Rais, ningempiga chini Meck Sadick..!! haraka sana tu

Alafu you made big mistake.. Huwezi sema Tz ndio Dar na Dar ndio Tz.. where hv you been schooling that..? Hz shule za wapi..?

Clear statement with Logic is..

Dar ni Tanzania..✔✔✔✔✔
na Tanzania SIO Dar.. ❌❌❌❌❌
narudia tena Tanzania SIO DAR... ushindwe..!!❌❌❌❌❌❌❌❌❌
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom