EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Naweza nisieleweke kwa sasa lakini kadri muda unavyokwenda mtanielewa.
Tanzania ni Dar na Dar ni Tanzania.
Jiji hili ni kila kitu, lina mchanganyiko wa fani zote unazozijua, kuanzia wasomi, wezi, bandari, mabenki, balozi, majeshi, ombaomba, majambazi, matapeli, wafanyakazi, wasio na kazi n.k, naweza kusema ni kama "reception" ya nchi.
Kuteteleka kwa uongozi wa mkoa huu ni kama kielelezo cha kuteteleka kwa uongozi wa nchi. Kwa maana hiyo mkoa huu unahitaji kiongozi mahili mwenye busara mission na vision ya kuuongoza.
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo jiji hili kama mkoa lilibahatika kuongozwa na Mh. Makamba, Mh. Kandoro, Mh Meck Sadick bila kumsahau Keenja aliyeliongoza Tume ya Jiji kwa mafanikio makubwa, pamoja na wakati huo jiji kuwa na vitendeakazi duni lakini lilionekana kuwa safi.
Nakumbuka vilevile operesheni mbalimbali za Makamba na Kandoro na Meck Sadick kuhusu machinga na ombaomba, walikuwa wakifukuzana na machinga mitaani lakini walikuwa na "alternative" kama vile kuanzishwa kwa Machinga Complex na mabasi kuhamia UBT.
Tofauti na mkuu wa mkoa wa sasa Mh. Paul Makonda, yeye tangu aanze kutoa matamko "operations" sijaona hata moja likifanikiwa, sina haja ya kuorodhesha hapa matamko yake.
Labda niseme ni kutokana na uzoefu wake kuwa mdogo au umri au ukosefu wa uwezo wa kubuni mbinu mpya za kutatua kero za jiji na mkoa huu ambazo ni nyingi au labda hajui JDs na uwezo wa cheo alichonacho.
Ni kutokana na hayo ndiyo maana nashauri aidha Mh. Rais amrudishe mkuu wa mkoa aliyepita Said Meck Sadick au Makonda atafutiwe msaidizi/mshauri mzoefu au jiji likabidhiwe kwa tume nyingine ya Jiji kama iliyokuwa ile ya Charles Keenja.
Bila kufanya hayo mapema na kwa wakati, kuna hatari ya Jiji kupoteza hadhi yake.
Naomba kuwasilisha.