Mh Rais, achia pesa tunakufa njaa mitaani huku

Mh Rais, achia pesa tunakufa njaa mitaani huku

hivi raisi aliyepita alikuwa anagawa pesa sio
Mleta mada hakumaanisha hivyo. Ni kwamba rais aliepita aliachia semina na warsha zifanyike mahotelini na posho zilitolewa nje nje. Hizo ndizo zilisaidia kukuza sekta binafsi. Kwa sasa hoteli nyingi zinafungwa ama kupunguza watendaji, kwa sababu serikali ilikua ni sehemu ya wateja wakuu. No sekta myongi zimeathirika, sio mahoteli tu
 
Kwa muda sasa serikali imekuwa haiachii pesa iingie kwenye mzunguko kwa kigezo cha kubana matumizi. Pesa inakusanywa lakini hairudishwi mitaani ili mzunguko uendelee na uchumi ukue.

Serikali imebana sana au kuondoa kabisa matumizi ya fedha kama katika kutoa tenda mbali mbali, kukodi kumbi za mikutano na makongamano, n.k. Kwa ujumla serikali imeishikilia pesa.

Matokeo yake sisi watu masikini ndio tunaumia. Vibiashara vyetu vidogovidogo vimekosa mnunuzi, bia bar haziuki, n.k.

Kubana pesa na kwenda kuzinunulia ndege, au kujengea mabarabara sawa, lakini impact yake kwa sisi masikini ni ndogo. Kuhamia dodoma sawa, lakini impact yake kwa sisi masikini, machinga na mama ntilie ni ndogo.

Mh ebu achia pesa iingie kwenye mzunguko kama kawaida cha msingi tu matumizi sahihi yazingatiwe! Kuna tetesi kutoka Hazina kwamba umeamua kushikilia pesa kwa hofu eti ukiyoa mafungu kama budget ilivyopitisha zitaliwa na wafanyakazi hewa n.k! Inasemekana unalipa tu mishahara na kugharimia mahitaji ya lazima ya wizara, hela nyingine yote unaizuia.

Hebu pia kaa na wachumi wako mjaribu kutatua hii hali hii mapema. Wananchi watashindwa uvumilivu.

Hii hali ikiendelea usishangse watu wakaamua kuingia mitaani bila hata kuchochewa kulalamikia ugumu wa maisha. Haiwezeksni kila unayeongea naye analalamikia ugumu wa maisha.

Mh achia hayo matrilioni yaingie mitaani. Halafu baadaye utayakusanya tena yarudi serikalini. Ndivyo uchumi wa nchi maskini unavyoendeshwa. Hali ni mbaya huku mitaani, haviuziki, havinunuliki! Tutafika kweli? Unatuumiiza sisi maskini mheshimiwa.

Kama kuna kitu kitafanikisha UKUTA kwa kiasi kikubwa ni hili la ukata na ugumu wa maisha, ambalo wengi wanasema wewe ndio umesababisha, na wala sio hili la kuminya demokrasia! La kuminya demokrasia nalo ni kubwa lakini kwa sasa watu wengi wana hasira kwasababu ya ukata unaoaminika umesababishwa na sera zako za kukurupuka.
BADO MIAKA KIBAO..........................
 
Attachments

wacha waisome namba eeeeee ccm mbele kwa mbele.....naupenda huu wimbo hivi nani kaimba vile
 
Mzunguko wa pesa haukwepeki,lakini bahati mbaya pesa ilitokana serikali kulipia huduma hewa,au ambazo hazina umuhimu.Kwa lugha nyepesi mzunguko wa pesa hasa miji mikubwa kama Dar ulitokana na serikali kuchapa usingizi.Jibu ni kujipanga upya fanya kazi halali upate ujira halali
Mbona kwangu kipato kimeongezeka mara tatu? Niwape siri kama ukiamua kuacha kuishi tofauti na ulivyokuwa ukiishi awamu ya NNE lazima upige pesa, kwa kazi yangu ukifanya shift tatu za usiku unapata mapumziko siku nne, zamani hizo siku nne ilikuwa ni kula bata na kuwatembelea washkaji kijiweni na ka mchepuko langu, mchepuko niliupa kadi nyekundu siku JPM anaapishwa na hizi siku nne za mapumziko nakuwa au ziwani navua au shambani.....mboga na chakula sinunui kwani nalima mwenyewe ila neema iliyoje hii mboga ninayolima sasa hivi ndio imekuwa na soko kubwa! Hivi kuna kosa muuguzi kuwa mvuvi pia? Hapana ili mradi muda wa mwajiri wangu nautumia kufanya kazi zake.

Acha kuishi kimazoea sasa hivi yule uliyekuwa unamuomba hela ya nauli kazini naye kapigika.
 
Acha porojo,serikali haimwagi magunia ya pesa barabarani
Ukiona biashara hailipi nenda kalime,utatoka tu,watu wametajirika kwa mananasi na matikiti maji
Mnakaa mijini mnajazana ujinga tu,mliozea hela za kupiga na kukwepa kodi hizo tusahau
Mkuu usikariri kilimo,kila mtu akilima atamuuzia nani? Je hukusikia debe la nyanya (ndoo ya kilo 20) ya nyanya huko Mbigiri wilayani Kilosa ni sh. 700?. Sikatai wala sikubali moja kwa moja hoja hii ila Ukweli maana haiwezekani kila mtu alalamike.
 
Kweli hakaze,wale wanafunzi aliosema atawapatia mkopo kwa muda muafaka mpaka sasa awajapatiwa hela ya field na awajui n ln watapata. JPM shikilia hapo hapo mpaka tuingie mitaani kuandamanA
hakaze[emoji735]
Akaze[emoji736]
Ajawapatia[emoji735]
Hajawapatia[emoji736]
 
Be creative angalia upepo upo wapi, fanya biashara ya basic needs watakuja tu, usifanye biashara ya extra needs, maana itakuwa ni alternatives kwa mteja hata hasiponunua hana cha kupoteza.
Hasiponunua[emoji735]
Asiponunua[emoji736]
 
Kupata kitambulisho cha kura ilikuwa FOLEN KALI, kupiga kura ilikuwa FOLENI KALI, kusubiri matokeo ilikuwa ni lazima uwe na SIKIO REFU , ili uelewe matokeo plus mita mia mbili.

Pole sana ndg yangu, kijan ni watu wabaya.

Majipu ya kwao, na tumbuaji wa kwao ..
Bila ya DIRA madhubuti kuwepo kwenye nchi hii hatutasonga mbele hata siku moja,leo hii tunaambiwa nchi ya viwanda ni lazima na huu uongozi wa awamu ya tano, lakini uongozi wa awamu ya tatu waliuza viwanda vyote vilivyokuwepo na vingine kuvigawa bure,kwa hiyo unaweza kushangaa uongozi wa awamu ya sita au saba hivi wakaja na sera ya kubinafisisha tena vile viwanda vilivyojengwa na awamu ya tano kwa madai kwamba viko chini ya viwango vya kimataifa, kwa hiyo ni kubadili gia angani kama kawaida ni upuuzi ni utapeli wa hali ya juu .Hii habari ya kila rais kuja na mipango yake mfukoni kila baada ya kushinda uchanguzi ni mazingaombwe.Eti ilani,ilani ndo kitu gani ni kucheza na akili za watu,ni kucheza na akili za wandanganyika, upuuzi mtupu.Kwa hiyo uongozi huu unaharibu,unakuja uongozi mwingine unarekebisha kidogo,unakuja huu tena unafirisi nchi,unakuja huu tena unachangisha wananchi,unakuja huu tena unafisadi kila kitu,unakuja huu mnaanza upya tena,salaaaleh! si bora mungu aje aifute hii dunia tuanze upya maana tumetekwa.
 
Tulieni Mh. Anaandaa mazingira tuishi kama mbinguni. Mwenye njaa anywe maji miaaka kumi siyo mbali, kama hamtarithika badili maisha kwa kura ebo!
 
Mbinguni maisha ni raha mstarehe, maisha ni mteremko, ndo anayoandaa Mh. Kila mara ameomba tumuelewe, mimi sijamuelewa ila nasubiri nione, upo?
 
Nawaonea huruma wale wadada wawili niliowaajiri pale stationary kwangu.Natamani nibaki nao wote ila hali hairuhusu.Inabidi niwatimue nimweke mdogo wangu atakayeweza kunivumilia kuilinda ofisi kwa chochote atakachopata badala ya mshahara rasmi.No way.
 
Kwa muda sasa serikali imekuwa haiachii pesa iingie kwenye mzunguko kwa kigezo cha kubana matumizi. Pesa inakusanywa lakini hairudishwi mitaani ili mzunguko uendelee na uchumi ukue.

Serikali imebana sana au kuondoa kabisa matumizi ya fedha kama katika kutoa tenda mbali mbali, kukodi kumbi za mikutano na makongamano, n.k. Kwa ujumla serikali imeishikilia pesa.

Matokeo yake sisi watu masikini ndio tunaumia. Vibiashara vyetu vidogovidogo vimekosa mnunuzi, bia bar haziuki, n.k.

Kubana pesa na kwenda kuzinunulia ndege, au kujengea mabarabara sawa, lakini impact yake kwa sisi masikini ni ndogo. Kuhamia dodoma sawa, lakini impact yake kwa sisi masikini, machinga na mama ntilie ni ndogo.

Mh ebu achia pesa iingie kwenye mzunguko kama kawaida cha msingi tu matumizi sahihi yazingatiwe! Kuna tetesi kutoka Hazina kwamba umeamua kushikilia pesa kwa hofu eti ukiyoa mafungu kama budget ilivyopitisha zitaliwa na wafanyakazi hewa n.k! Inasemekana unalipa tu mishahara na kugharimia mahitaji ya lazima ya wizara, hela nyingine yote unaizuia.

Hebu pia kaa na wachumi wako mjaribu kutatua hii hali hii mapema. Wananchi watashindwa uvumilivu.

Hii hali ikiendelea usishangse watu wakaamua kuingia mitaani bila hata kuchochewa kulalamikia ugumu wa maisha. Haiwezeksni kila unayeongea naye analalamikia ugumu wa maisha.

Mh achia hayo matrilioni yaingie mitaani. Halafu baadaye utayakusanya tena yarudi serikalini. Ndivyo uchumi wa nchi maskini unavyoendeshwa. Hali ni mbaya huku mitaani, haviuziki, havinunuliki! Tutafika kweli? Unatuumiiza sisi maskini mheshimiwa.

Kama kuna kitu kitafanikisha UKUTA kwa kiasi kikubwa ni hili la ukata na ugumu wa maisha, ambalo wengi wanasema wewe ndio umesababisha, na wala sio hili la kuminya demokrasia! La kuminya demokrasia nalo ni kubwa lakini kwa sasa watu wengi wana hasira kwasababu ya ukata unaoaminika umesababishwa na sera zako za kukurupuka.
Pole sana! Hasikii huyo na ikitokea akakufahamu anakufungulia kesi ya makosa ya kimtandao kwamba umemkashfu!
 
Mbinguni maisha ni raha mstarehe, maisha ni mteremko, ndo anayoandaa Mh. Kila mara ameomba tumuelewe, mimi sijamuelewa ila nasubiri nione, upo?
Maisha ya mbinguni yanaletwa na mtu? we subiri hiyo mbingu ya viwanda kama utaiona.
 
Asipoionesha na ukata wa fedha ukawa kama hivi, baada ya miaka 5 tumtoe. Ndiyo tumtoe ili tuweze kuishi. Hivi anajua kama sisi tunaishi kwa kudura ya Mungu? Kama yeye anauhakika wa kula sisi kila kukicha ni bora ya Jana.
 
u

Utamtoaje mkuu wakati wewe huna jeshi.Uliona Ethiopia juzi, kazi ipo mkuu.
 
Back
Top Bottom