Mh Rais, achia pesa tunakufa njaa mitaani huku

Mh Rais, achia pesa tunakufa njaa mitaani huku

Mheshimiwa rais Magufuli, hakuna kulegeza kamba, wembe ni ule ule hata kama watu walie namna gani. Hata waisrael walipokuwa njiani kuelekea nchi ya ahadi walilia lia hivyo hivyo wakamlaumu Musa na hata kumnung'unikia mwenyezi mungu, lakini hatimaye walifika. NI HERI TUKAPATA SHIDA SASA NA HAPO BAADAYE TUKAISHI KWA RAHA. Mchumia juani hulia kivulini.
Hahahaha ule ulikua ni mpango wa Mungu na Mungu alifanya ishara nyingi mpk wao kupata kibali kamwe huezi fananisha uongozi wowote wa ubinafsi na mpango wa Mungu.
 
Kazana baba kazana usilegeze, usigeuke nyuma utakuwa jiwe washaanza kulia lia waliozoea za dezo ongeza speed tuko nyuma yako sisi tuliokupigia kura tunafurahishwa na jitihada zako za kubana matumizi na kutumbua waliokuwa wanafisadi nchi. Tutazidi kukuombea mola akulinde Na kila anaekusudia baya juu yako limpate mwenyewe. Usikubali mtu akucheleweshe nasisi wananchi tuliokupigia kura hatutakubali kuona mtu anakuchelewesha. Aluta continue. Tafuteni shughuli halali za kuongeza kipato

Kweli hakaze,wale wanafunzi aliosema atawapatia mkopo kwa muda muafaka mpaka sasa awajapatiwa hela ya field na awajui n ln watapata. JPM shikilia hapo hapo mpaka tuingie mitaani kuandamanA
 
Kweli hakaze,wale wanafunzi aliosema atawapatia mkopo kwa muda muafaka mpaka sasa awajapatiwa hela ya field na awajui n ln watapata. JPM shikilia hapo hapo mpaka tuingie mitaani kuandamanA
Na mkiandamana kisa hela ya field mnapigwa mabomu tu!!!! Na wilaya ikikumbwa na njaa hakuna kupewa chakura cha bure!!!! maisha yamekuwa magumu sana mitaani hata wale wamama waliokuwa wakiuza chapati asubuhi sasa hivi siwaoni tena!!! Nabaki kusikitika tu!!! Tuone huruma bas ewe mtukufu
 
Siku zote mfalme hakumbuki wananchi wake na anapenda sana akiwaona wanateseka.
 
Tupo kazini kaka tangu saa 12 ssubuhi mpaka saa tano usiku, ni kufukuza inzi na kupiga miayo tu, wateja hamna.
Be creative angalia upepo upo wapi, fanya biashara ya basic needs watakuja tu, usifanye biashara ya extra needs, maana itakuwa ni alternatives kwa mteja hata hasiponunua hana cha kupoteza.
 
Be creative angalia upepo upo wapi, fanya biashara ya basic needs watakuja tu, usifanye biashara ya extra needs, maana itakuwa ni alternatives kwa mteja hata hasiponunua hana cha kupoteza.
Huu ushauri wako unáashiria nini? Nani kakuambia nafanya biashara ya extra needs! yaani badala ya kunishauri kwenda mbele unanishauri niridhike na basic needs? You must be ..basi tu, wacha nikuhifdhi kwanza! Nyie wanalumumba sijui akili mmeziazima wapi!
 
Katika kuji adjust kwenye utawala wa Magu nimefanya haya:-

... Nikienda Bar naagiza ama Soda au Bapa ndogo la Konyagi.

...Kula kuku na mishikaki imekuwa anasa hivyo mwendo ni chips dry au mikate ya Temeke tu.

...Kunyoa kwa wiki mbili mara moja kwa sasa. Zamani nilikuwa nafanya massage na kunyoa kila wiki.

...Sikumbuki mara ya mwisho nilikanyaga lini kununua nguo za dukani tangu Magu aapishwe.

...Gari nafikiria kupaki nyumbani na nimeanza taratibu za kununua kadi ya mwendokasi ili nibane matumizi ya Petrol.

...Ndugu kwa sasa wanasema nina roho mbaya kisa sitoi ushirikiano wa michango kama ya harusi nk.

...Vitoto vya kijijini nilivyo viahidi kuvileta mjini ili nivisomeshe vimeanza kuniona tapeli.

Haya ni kwa uchache tu ila kuna adjustment nyingi nimezifanya za kubana matumizi.
 
Ee bhanae! Hamy D za siku ndugu yangu. Umepotea sana hapa jukwaani. Km na wewe ccm kindakindaki umeona hayo basi Ngosha ana hatihati kupata kipindi chs pili come 2020, km atafika huko!
 
Mheshimiwa rais Magufuli, hakuna kulegeza kamba, wembe ni ule ule hata kama watu walie namna gani. Hata waisrael walipokuwa njiani kuelekea nchi ya ahadi walilia lia hivyo hivyo wakamlaumu Musa na hata kumnung'unikia mwenyezi mungu, lakini hatimaye walifika. NI HERI TUKAPATA SHIDA SASA NA HAPO BAADAYE TUKAISHI KWA RAHA. Mchumia juani hulia kivulini.
Waliwakuta wapalestina, mpaka leo vurugu
 
Huu ushauri wako unáashiria nini? Nani kakuambia nafanya biashara ya extra needs! yaani badala ya kunishauri kwenda mbele unanishauri niridhike na basic needs? You must be ..basi tu, wacha nikuhifdhi kwanza! Nyie wanalumumba sijui akili mmeziazima wapi!
akili yako wewe ndio ipo unavyofikiri, soma tena uelewe nina maana gani husikurupuke, husichangwanywe na maisha ukaona double. Nimekuambia fanya biashara ambayo ni basic needs, mtu lazima anunue unachouza kwani ni hitaji muhimu, hila ukiuza extra needs kama nguo sasa hela hatuna za honoraria na safari za nje, hatwendi na fashion, tunazo tulishafanya shopping Dubai, hapo labda utaelewa what I meant biashara ya basic na extra needs
 
Sugu aliongelea hilo swala mwanzoni kabisa lakini watu hawakumuelewaa,wenye akili kubwaz tulimuelewa sana,Kuzuia flow iliyokuwa inaenda kikawaida gafla lazima italeta impact angeanza taratibu huku anatafuta alternative,unabana kwenye semina unaachia kwenye tender sasa ukibana kote kote ni shida...One Man Army haifai maana issue nyingi ni mtambuka lazima upate ushauri kwa wadau wote nchi ni ya watu wote na sio ya mapadlock.
Sugu alikuwa anapigia chapuo hotel yake.
 
Huu ushauri wako unáashiria nini? Nani kakuambia nafanya biashara ya extra needs! yaani badala ya kunishauri kwenda mbele unanishauri niridhike na basic needs? You must be ..basi tu, wacha nikuhifdhi kwanza! Nyie wanalumumba sijui akili mmeziazima wapi!
Huyo kajichanganya,Hajui kuwa kuna watu Kilosa wanauza nyanya Lita 20 kwa Tsh.7000/-
 
Hata hivyo kiasi kilichopatikana mwezi wa saba kwa Tra dhidi ya Kodi iliyokusanywa nadhani sii kweli huenda wamerudi kile kiasi cha Mkwele.
 
Kupata kitambulisho cha kura ilikuwa FOLEN KALI, kupiga kura ilikuwa FOLENI KALI, kusubiri matokeo ilikuwa ni lazima uwe na SIKIO REFU , ili uelewe matokeo plus mita mia mbili.

Pole sana ndg yangu, kijan ni watu wabaya.

Majipu ya kwao, na mtumbuaji wa kwao ..
Hiyo ndn demokrasia ya Lumumba. uongo ndo ukweli na ukweli ndo uongo. Hawa ni zaidi ya 666
 
Tatizo ni makosa tuliyoyafanya miaka kumi iliyipita.
Amna uongozi bora "mambo yataenda kiasara.

Penye uongozi wenye mwangaza "watu wanalalamika amna pesa .
Tatizo sisi wenyewe tumeshajizoesha kuishi kiasala + kukalili
 
fanya kazi acha kulialia weye, badili mbinu acha kuganda kwenye mbinu moja tu ya uzalishaji. Mfano kama pesa imebanwa kwenye ukodishaji wa kumbi za mikutano lazima kuna mahali pengine imepelekwa, fanya assignment yako ya kujua wapi imepelekwa na wewe jichanganye huko pesa ilipoenda. Mfano kama pesa imepelekwa kwenye kilimo nenda kalime, anzisha biashara zinahusiana na kilimo n.k. Kipindi hiki cha awamu ya tano hakuna pesa za ujanjaujanja na misheni town bali ni ubunifu, kutumia profession, na kufanya kazi kwa bidii na maharifa ndio kunakupatia fedha. Chumi zote za kisasa ndio zinavyoendeshwa, serikali ikiacha pesa izagae mtaani mfumuko wa bei lazima uongezeke na hapo maisha yanakuwa magumu zaidi.

Mkuu hebu usijaribu kuongea hiyo kitu nikalia kwa hasira, mimi nimelima heka 3.5 ya nyanya, nimetumia zaidi ya milioni 2 kutunza hizo heka, leo hii nauza crate 1 kwa shilingi 18,000, mbali ya hiyo bei wala hazitoki kwa hivyo, hivyo kuna uwezekano wa zaidi ya nusu kuharibika. Sidhani hata kama nitapa milioni moja. Hasara hii serekali haihusiki, lakini usishangae mtendaji wa kijiji akinifuata siku chache zijazo nichangie maabara. Ukiongea na viongozi wa kijiji ambao ndio mabingwa wa kufuata michango ni nini kifanyike kwenye hali kama hii hawana la kukwambia zaidi ya pole. Sasa najiuliza serekali inaposema watu wakafanye kazi wakati hawako tayari kushiriki changamoto kama hizi wanamaanisha nini? Sasa katika mazingira kama haya nitaweza vipi kumshawishi mtu anayecheza pooltable ya kamari aje alime? Haya ndio maisha yetu wakulima huenda ndio maana wanasiasa wanatumia umaskini huu tunaokutana baada ya kuvuja jasho kuturubuni kwamba wataboresha mazingira yetu, lakini wakipata kura wanapita hivi.
 
Back
Top Bottom