Mh Rais, achia pesa tunakufa njaa mitaani huku

Mh Rais, achia pesa tunakufa njaa mitaani huku

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,452
Reaction score
3,152
Kwa muda sasa serikali imekuwa haiachii pesa iingie kwenye mzunguko kwa kigezo cha kubana matumizi. Pesa inakusanywa lakini hairudishwi mitaani ili mzunguko uendelee na uchumi ukue.

Serikali imebana sana au kuondoa kabisa matumizi ya fedha kama katika kutoa tenda mbali mbali, kukodi kumbi za mikutano na makongamano, n.k. Kwa ujumla serikali imeishikilia pesa.

Matokeo yake sisi watu masikini ndio tunaumia. Vibiashara vyetu vidogovidogo vimekosa mnunuzi, bia bar haziuki, n.k.

Kubana pesa na kwenda kuzinunulia ndege, au kujengea mabarabara sawa, lakini impact yake kwa sisi masikini ni ndogo. Kuhamia dodoma sawa, lakini impact yake kwa sisi masikini, machinga na mama ntilie ni ndogo.

Mh ebu achia pesa iingie kwenye mzunguko kama kawaida cha msingi tu matumizi sahihi yazingatiwe! Kuna tetesi kutoka Hazina kwamba umeamua kushikilia pesa kwa hofu eti ukiyoa mafungu kama budget ilivyopitisha zitaliwa na wafanyakazi hewa n.k! Inasemekana unalipa tu mishahara na kugharimia mahitaji ya lazima ya wizara, hela nyingine yote unaizuia.

Hebu pia kaa na wachumi wako mjaribu kutatua hii hali hii mapema. Wananchi watashindwa uvumilivu.

Hii hali ikiendelea usishangse watu wakaamua kuingia mitaani bila hata kuchochewa kulalamikia ugumu wa maisha. Haiwezeksni kila unayeongea naye analalamikia ugumu wa maisha.

Mh achia hayo matrilioni yaingie mitaani. Halafu baadaye utayakusanya tena yarudi serikalini. Ndivyo uchumi wa nchi maskini unavyoendeshwa. Hali ni mbaya huku mitaani, haviuziki, havinunuliki! Tutafika kweli? Unatuumiiza sisi maskini mheshimiwa.

Kama kuna kitu kitafanikisha UKUTA kwa kiasi kikubwa ni hili la ukata na ugumu wa maisha, ambalo wengi wanasema wewe ndio umesababisha, na wala sio hili la kuminya demokrasia! La kuminya demokrasia nalo ni kubwa lakini kwa sasa watu wengi wana hasira kwasababu ya ukata unaoaminika umesababishwa na sera zako za kukurupuka.
 
Sugu aliongelea hilo swala mwanzoni kabisa lakini watu hawakumuelewaa,wenye akili kubwaz tulimuelewa sana,Kuzuia flow iliyokuwa inaenda kikawaida gafla lazima italeta impact angeanza taratibu huku anatafuta alternative,unabana kwenye semina unaachia kwenye tender sasa ukibana kote kote ni shida...One Man Army haifai maana issue nyingi ni mtambuka lazima upate ushauri kwa wadau wote nchi ni ya watu wote na sio ya mapadlock.
 
Mh alitakiwa aplay very smart katika nia yake ya kujaribu kurekebisha mambo. Hii nchi naweza kuifananisha na mgonnjwa aliyekuwa na homa kali! Sasa wewe daktari badala ya kuchukua hatua za kushusha homa yake pokepole kwsnza, unakurupuka na kumpiga sindano za kwinini, kwa nini asife?
 
Biashara imedorora, maana hakuna watu wa kununua, pesa hakuna. Watu wanafirisiwa kwa kushindwa kulipa mikopo. Watu wanafunga biashara na wengine wanakufa kwa stress.
Ukusanyaji wa kodi na kubana matumizi sawa. Ila baada ya muda lengo halitafikiwa maana biashara nyingi itafungwa.
Yapaswa kujenga mazingira ya kuwezesha wananchi waongeze uzalishaji ili walipe kodi na wao kunufaika. Siyo wakate tamaa na kufunga biashara ambayo ni tegemeo lao ktk maisha yao.
 
Sugu aliongelea hilo swala mwanzoni kabisa lakini watu hawakumuelewaa,wenye akili kubwaz tulimuelewa sana,Kuzuia flow iliyokuwa inaenda kikawaida gafla lazima italeta impact angeanza taratibu huku anatafuta alternative,unabana kwenye semina unaachia kwenye tender sasa ukibana kote kote ni shida...One Man Army haifai maana issue nyingi ni mtambuka lazima upate ushauri kwa wadau wote nchi ni ya watu wote na sio ya mapadlock.
Kweli Mkuu nakumbuka sugu aliongea, sasa aya ndo majibu
 
Wakati wa kupiga kura ulikua mstari wa mbele kupigia chama cha kijani ukijua upinzani pekee wataisoma namba. Sasa namba tunaisoma wote..Vumilia tu mkuu
Acha ujinga! Nani awapigie kura hawa wanamajipu?
 
Kazana baba kazana usilegeze, usigeuke nyuma utakuwa jiwe washaanza kulia lia waliozoea za dezo ongeza speed tuko nyuma yako sisi tuliokupigia kura tunafurahishwa na jitihada zako za kubana matumizi na kutumbua waliokuwa wanafisadi nchi. Tutazidi kukuombea mola akulinde Na kila anaekusudia baya juu yako limpate mwenyewe. Usikubali mtu akucheleweshe nasisi wananchi tuliokupigia kura hatutakubali kuona mtu anakuchelewesha. Aluta continue. Tafuteni shughuli halali za kuongeza kipato
 
Dah inasikitisha sana kwa kweli!! Wanafunzi wa vyuo vikuu wamenyimwa hela za field....
 
Naijutia kura yangu vibaya mno

Kupata kitambulisho cha kura ilikuwa FOLEN KALI, kupiga kura ilikuwa FOLENI KALI, kusubiri matokeo ilikuwa ni lazima uwe na SIKIO REFU , ili uelewe matokeo plus mita mia mbili.

Pole sana ndg yangu, kijan ni watu wabaya.

Majipu ya kwao, na mtumbuaji wa kwao ..
 
Mm nilikuwa namkubali sana jamaa mwanzoni na nikifika kijiweni nikikuta watu wanamponda nilikuwa napambana nao kwa hoja mpaka nilikuwa nawashinda, ila kwa sasa jamaa kaniangusha sana na mwenendo wake anapoelekea hasa hasa alivyozuia ajira zetu ndo kabisaa sijamuelewa yani sasa hivi nikifika kijiweni mm nakuwa mpole tu sina la kusema washikaji wananiambia haya kipo wapi sasa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
COamoTFUYAABRI4.jpg
 
Back
Top Bottom