Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Ritz, hivi katika sakata hili tunafuata legal instrument gani kuthibitisha mpaka? Mkutano wa Berlin au Heligoland Treaty?Malawi wanapoteza muda wanaleta usumbufu tu mkutano wa mwaka 1884 uliofanyika Berlin lazima kila nchi iheshimu mipaka iliyowekwa na wakoloni.
Waziri Benard Membe ameweka wazi kuhusu mpaka wa Tanzania na kubainisha kuwa mpaka unapita katikati ya ziwa Nyasa!
Na amebainisha kuwa mipaka hiyo iliwekwa kwakipindi hicho nyasa ikiitwa Nyasaland nahivyo wamalawi wamekuwa wakijua Nyasa ni yao na Tanzania inaishia pwani ya ziwa Nyasa!
Na amesema tatizo ni la mda mrefu tangu miaka ya 1960... Na hili tatizo lilishindikana kutatuliwa kwakuwa Kiongozi wa Malawi Kamuzu Banda Kuwa na urafiki na makaburu.. Hivyo Tanzania kwakuwa ilikuwa inaendesha harakati za ukombozi mwa afrika kusini hivyo haikuwa rahisi kwa Tanzania kukaa kitikimoja na Malawi kwakuwa Malawi iliwakumbatia Makaburu.
UPDATE:
Serikali imetoa tamko rasimi kuanzia sasa kuondoka,kuanzia sasa na serikali haitaruhusu utafiti huu kuendele mpaka makubaliano yatakapokuwamepatiwa muafaka....Na serikali iko tayari kulinda mipaka kwa gharama yoyote ile na imeitahadharisha serikali ya malawi kuondoka mara moja na kusitisha shughuli zozote zile za utafiti ndani ya Ziwa Nyasa.
Hivi nyie mnaodhani malawi "itapigika kirahisi" mnadhani kinachopigana vita ni ukubwa wa ardhi...au ni watu wakitumia utaalamu pamoja na vifaa!?Kuipiga Malawi hakuna hata kuiambia dunia kuwa tuna vita na wamalawi.
palalisote kumbe shuhuli imeashaanza!!??
Wewe unaijua nchi inayoitwa Tanzania? Brabra zipo uraiani na kwenye majukwaa ya kisiasa siyo JWTZ.Nina wasi wasi na uwezo wa nchi yetu na jeshi letu kwa ujumla!
Maana naona blah blah nyingi je kama bado wanaendelea na utafiti mtafanyaje?maana ata speed boat za kusua sua
Mkeshaji ni muhimu ukazingatia kutulinganisha na wenzetu wa nchi za kiafrika, na hapo utakubaliana nami kwamba kwa upande wa kijeshi tuko vyema sana.Hivi nyie mnaodhani malawi "itapigika kirahisi" mnadhani kinachopigana vita ni ukubwa wa ardhi...au ni watu wakitumia utaalamu pamoja na vifaa!?
Ingekuwa ukubwa wa ardhi ndo kigezo cha kushinda vita basi tz ina uwezo wa kuzishinda nchi nyingi sana za ulaya ikiwemo wingereza!
Tujiulize kwanza, ni kwa nini wamalawi wamejiamini sana!?
Haka kanchi ni kabaya kwa mambo ya kiuchumi lakini siyo kwenye mambo kugombea mipaka. Kama wamalawi hawakajui, basi waendelee na chokochoko zao. Watafumuliwa na mama yao atakimbilia Afrika Kusini awaache wanalia peke yao.
Unajua hapa sasa magamba watatumia hii kama mtaji wakisiasa kwa kuiingiza nchi vitani na malawi kwa hapa malawi wamepatikana ole wao wakaidi agizo kalolaiti ya nape itawaishia migongoni.Pia watanzania wenzangu jueni kwamba maisha yatakua magumu na jamaa wa magharibi simnajua wameungana na malawi baada ya kuukubali ushoga nategemea watapewa kila aina ya msaada wa kijeshi na marekani na uingereza na hapo ndipo uraniumu itachimbwa bure kama mafuta kule iraq!Kwa ufupi vita imeanza kati ya Tanzania na Malawi hata kama tutapatana na malawi!Nani kasema ukiibiwa vitu ndani ya nyumba yako na majambazi unasusa na kuacha kununua chochote nyumbani kwako???
makosa au kasoro zinazilalamikiwa kuwa serikali haijalinda vya kutosha raslimali zetu sio msingi wa kususa ziwa Nyasa na kwaachia wamalawi ni wendawazimu.
palalisote kumbe shuhuli imeashaanza!!??
Good show!!!!
Uchokozi wa Malawi nauona katika jambo moja tu hata kama ziwa Nyasa ni la kwao na sisi tunasema hapana tuna sehemu yetu ...... Hawana budu kuwa waungwana kumaliza mgogoro mezani hata ikibidi kuitumia jumuia ya kimataifa kuliko kupuuza mazungumzo na kuendeleza miradi ndani ya ziwa.............. Hizi ni dharau hata kwa Rais mnayemuita ni dhaifu hawezi kuvumilia ubinafasi huu.
kama kweli malawi wana ushahidi kwa kutosha kwa nini hawakimbilii kusuluhishwa na jirani yao (Tanzania) wao wanakimbilia kuingiza makampuni ya utafiti wa mafuta ziwani?
Vita sio suluhisho. Ni kutumia njia mbadala za kutatua tatizo
Hakuna haja ya kupiga Jaramba kwa sababu ya hisia, swala la kwamba Ziwa Nyasa kuna mafuta ndio linalowatoa viongozi wetu mapovu, kama kweli viongozi wetu wako makini katika kuhakikisha interest za Tanzania hazichezewi, waanze kutuonyesha kwa vitendo kwa kuhakikisha kwamba tunapata a reasonable share kwenye mapato ya madini, waanze kutuonyesha kwa vitendo kwamba viongozi wazembe, wala rushwa na mafisadi wanachukuliwa hatua.
Watanzania tusiwe tayari kutengenezewa maadui wengine wakati serikali hii hii imeshindwa kudhibiti Maralia kwenye makazi yetu badala yake inasubiri misaada kutoka nje.
Kama unataka kupiga Jaramba, anza kupiga Jaramba sasa kama meseji kwa CCM kwamba comes 2015 wasipokuwa tayari kuachia madaraka kwa mujibu wa matakwa ya UMA wa Tanzania basi wajiandae kwa lolote.
Acheni kusumbuana na Poor Malawi, kwanza wanamatatizo yao mengi tu ndio maana wao kupewa hadithi ya mafuta wameona kama vile uchimbaji umeanza. sisi hatuhitaji exploration, it is confirmed kwamba dhahabu, uranium,Tanzanite, Diamond etc zimejaa chini ya ardhi yetu. Kama vipi tupige Jaramba kuyalinda haya kwanza.
Tanzania inategemea general international law inayosema kwamba nchi mbili zinazopakana na water body zita-share hiyo body na mpaka utakuwa katikati ya water body husika. Malawi wanajibu wanasema sheria hiyo inatumika kusipokuwa na treaty, hivyo kwa Ziwa Nyasa kwa kuwa kuna hiyo treaty sheria ya kimataifa hai-apply. Sijui Tz tuna argument gani zaidi?
Nina wasi wasi kama Tanzania tuna a credible legal basis (document) to back our claims kuwa mpaka upo katikati ya Ziwa